settings icon
share icon
Swali

Je, biblia kweli ni neno la Mungu?

Jibu


Jibu letu katika swali hili halitagusia tu mtazamo wetu juu ya biblia na umuhimu wake maishani mwetu bali pia hatimaye litakuwa na mguso wa milele maishani mwetu. Kama biblia kweli ni neno la Mungu, basi natulifurahie, tulisome, tulitii na kuliamini. Kama biblia ni neno la Mungu basi kulikataa ni kumkataa Mungu.

Kupatiwa kwetu biblia na Mungu ni kithibitisho cha kuwa Mungu anatupenda. Neno “ufunuo” lina maana ya kuwa Mungu aliwasiliana na mwanadamu jinsi alivyo na ni kwa jinsi gani tunaweza kupata ushirika mwema naye. Haya ni mambo ambayo hatungeweza kuyajua kama Mungu hangekuwa ameyawasilisha kwetu katika biblia. Ijapokuwa ufunuo wa Mungu katika biblia umetolewa kwa mfululizo ndani ya takriban miaka 1500 umehifadhi kila kitu mwanadamu anahitaji kumjua Mungu ili awe na ushirika mwema naye. Kama biblia ni neno la Mungu kweli basi ndiyo mamlaka ya mwisho katika mambo ya kiimani, dini na wema.

Swali ambalo sharti tujiulize ni tunawezaje kujua bibilia ni neno la Mungu wala si kitabu tu? Ni kitu gani maaluum ndani ya biblia ambacho huifanya biblia iwe kitabu maalum mbali na vitabu vyengine vya dini Je, kuna ushahidi kuwa biblia ni neno la Mungu kweli? Haya ndiyo baadhi ya maswali ambayo yanahitajika kuangaliwa kama ni tunahitaji kujua kweli biblia ni neno al Mungu, lilitoka kwake na lenye kujitosheleza katika mambo yote ya kiimani.

Hakuwezi kuwa na shaka katika swala la kuwa biblia ni neno la Mungu. Haya yanapatikana katika aya kama Timotheo wa pili 3:15-17, inayosema, “… Kutoka utotoni mmeyajua maandiko matakatifu, yenye uwezo wa kuwafanya ninyi werevu kwa ajili ya wokovu kupitia imani iliyo katika Kristo Yesu. Maandiko yote yametolewa kwa pumzi ya Mungu na yanafaa kwa mafundisho, kwa kuonya, kwa kurekebisha, kwa kuelekeza katika hakii ili mtu wa Mungu akamilishwe kwa ajili ya kila kazi njema.”

Ili tuyajibu maswali haya kwa usahihi, lazima tutazame ushahidi wa ndani na nje wa kuwa kweli biblia ni neno la Mungu. Ushahidi wa ndani ya biblia ni yale maandiko ambayo yanaelezea kuhusu chanzo cha kuweko kwake. Ushahdi wa kwanza ni katika ule umoja wake biblia. Ingawa ina vitabu sitini na sita vilivyoandikwa katika mabara matatu kwa lugha tatu tofauti ndani ya takriban miaka 1500 na waandishi zaidi ya 40 (waliotoka katika taaluma mbalimbali), biblia inabaki kitabu chenye kuhifadhi umoja kutoka mwanzo mpaka mwisho bila kujipinga chenyewe. Hali hii ni maalum kulinganisha na vitabu vyengine na inathibitisha kuweko kwa sauti ya Mungu ikinakiliwa na wanadamu.

Lengine katika ushahidi wa ndani, lapatikana katika unabii ulioorodheshwa ndani ya kurasa za biblia. Humu tunapata unabii juu ya mataifa binafsi kama vile Israeli, unabii wa miji Fulani, unabii wa maisha ya wanadamu na hata wa kuja kwake masihi, mwokozi si wa Israeli tu bali hata kwa wale pia watakaomwamini. kinyume cha unabii unaopatikana katika vitabu vyengine ama ule uliofanywa na Nostradamus, unabii wa kibiblia unatimia. Kuna unabii zaidi ya mia tatu kuhusu Yesu kristo katika Agano la kale pekee. Haikutabiriwa tu atazaliwa wapi na atakuwa wa jamii gani lakini pia ya kuwa angekufa na kufufuka siku ya tatu. Hakuna njia mwafaka ya kuelezea ni kwa uwezo gani unabii huu ulitimizwa ispokuwa kukiri ni kwa uwezo wa Mungu. Hakuna kitabu chenginecha dini chenye unabii unaodhihirika kama Biblia.

Ushahidi wa tatu unapatikana katika uweza na mamlaka ya Biblia. Hili si jambo dogo la kupuuzwa. Biblia ina mamlaka kuliko vitabu vyovyote vyengine. Uwezo huu unaonekana katika maisha ya wanadamu kama vile watu wasiohesabika wameweza kubadilishwa kwa kusoma biblia. Wenye kutumia mihadharati wameponywa na biblia, wahalifu sugu pia wamebadilishwa na biblia, wenye dhambi hukaripiwa na biblia na chuki kubadilishwa kuwa upendo kwa kulisoma biblia. Biblia ina uwezo wa kubadilisha maisha ya mtu kwa kuwa ni neno la Mungu.

Mbali na ushahidi wa ndani ya biblia, kuna ushahidi wa nje ya biblia unaothibitisha kuwa biblia kweli ni neno la Mungu. Umakini wa historia kama inavyoelezewa katika biblia ni ushahidi pia. Kupitia watafiti wa mabaki ya vitu vya kale na vitabu vyengine vilivyoandikwa, ratiba ya kihistoria katika biblia imehakikishwa mara kwa mara kuwa ya kweli. Watafiti hao pamoja na majarida wanayoyaandika husema ya kwamba biblia ndicho kitabu chenye kuongoza vyema katika historia sahihi ya maeneo mbalimbali. Jinsi biblia ilivyohifadhi histiria sahihi ya vizazi mbalimbali ni thibitisho ya kuwa ni kitabu cha ukweli pia katika kushughulikia maswala ya dini na mafundisho yake. Hili pia huthibitisha ya kuwa hili kweli ni neno la Mungu.

Jambo lengine ni kwamba heshima ya waandishi wa habari hizi za biblia. Mungu aliwatumia watu wa tabaka mbalimbali kuandika habari hizi. Tukuchunguza maisha ya watu hawa na ya kwamba walikuwa tayari hata kufa kwa ajili ya uaminifu wao kwa Mungu kwa ajili ya yale waiyoyaamini; Inathibitisha kuwa, watu hawa wanyonge na waaminifu walikuwa na uhakika kwamba Mungu kweli alikuwa amezungumza nao. Wale waliondika agano jipya na mamia ya waumini wengine (Wakorintho wa kwanza 15:6) walijua ukweli wa ujumbe wao kwa kuwa walikuwa wamemuona na kushirikiana na Yesu kristo baada ya kufa. Mabadiliko ya kumuona kristo aliyefufuka yalipokewa na uzito mkuu na watu hawa. Walibadilika kutoka kwa uoga wa kujificha na kuwa watu ambao hawaogopi kufa kwa ajili ya ujumbe wa Mungu uliokuwa umefunuliwa kwao. Maisha yao na vifo vyao vinathibitisha ya kwamba kweli biblia ni Neno la Mungu.

Ushahidi mwengine ni katika ile hali ya kutokuharibiwa kwa biblia. Kwa sababu ya umuhimu wake na kwamba ni neno la Mungu, biblia imepitia mapambano hatari mengi katika majaribio ya kuliharibu biblia kuliko kitabu chochote chengine katika historia Kutoka watawala wa jadi wa kirumi kama Diocletian, kupitia madikteta wa kikomiunisti na wale wasioamini kuna Mungu wanaoisho siku hizi, biblia imedhibiti hali yake na kudumu zaidi ya wapinzani wake. Hata sasa ndicho kitabu kinachochapishwa kwa wingi duniani.

Vizazi vyote na nyakati zote duniani,wapinzani wamekuwa wakipuuza biblia na kusema ni hadithi tu za watu lakini watafiti wa kihitoria wadumu wakithibitisha ya kuwa biblia ni kitabu cha kweli. Pia wapinzani wake wameshutumu mafundisho yake kuwa ya kijadi nayaliyopitwa na wakati lakini wema wake na mfumo wake wa kisheria umekubalika katika jamii na mila mbalimbali duniani kote. Inaendelea kushambuliwa na sayansi, saikologia, na vyama vya kisiasa na bado biblia inabaki na umuhimu sawa na ule iliyokuwa nao wakati ikiandikwa. Ni kitabu kilichobadilisha maisj\ha na tamaduni kwa muda wote wa miaka 2000 iliyopita. Haijalishi wapinzani wake wanapambana ki vipi, biblia inabaki ikiwa ni kitabu chenye nguvu, kweli na umuhimu sawa na ule kilichokuwa nao kabla kupigwa vita. Kuhifadhika kwa hali yake ya asili hata baada ya mashambulizi haya yote ni ishara ya kuwa biblia ni neno la Mungu. Isitushangaze ile hali ya kuwa bilia inapigwa vita na kuibuka bado mshindi bila madhara yoyote. Kumbuka Yesu alisema, “ Mbingu na dunia vitapita, lakini neno langu halitapita kamwe” (Marko 13:31). Baada ya kupitia ushahidi huu mtu bila shaka anaweza kusema “kweli Biblia ni Neno la Mungu.”

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, biblia kweli ni neno la Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries