settings icon
share icon
Swali

Je, sisi wote tulirithi dhambi ya Adamu na Hawa?

Jibu


Naam, watu wote walirithi dhambi ya Adamu na Hawa, hasa kutoka kwa Adamu. Dhambi ni kama ilivyoelezwa katika Biblia kuwa ni uvunjaji wa sheria ya Mungu (1 Yohana 3:4) na uasi dhidi ya Mungu (Kumbukumbu 9:7; Yoshua 1:18). Mwanzo 3 inaeleza uasi wa Adamu na Hawa dhidi ya Mungu na amri yake. Kwa sababu ya kutotii kwa Adamu na Hawa, dhambi imekuwa "urithi" kwa uzao wao wote. Warumi 5:12 inatuambia kwamba, kwa njia ya Adamu, dhambi iliingia ulimwenguni na hivyo mauti yakawa kwa watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi. Hii dhambi ambayo imepitishwa inajulikana kama dhambi ya kurithi. Kama sisi tu hurithi tabia ya kimwili kutoka kwa wazazi wetu, sisi hurithi asili yetu ya dhambi kutoka kwa Adamu.

Adamu na Hawa waliumbwa katika sura na mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27; 9:6). Hata hivyo, sisi pia tu katika sura na mfano wa Adamu (Mwanzo 5:3). Wakati Adamu alianguka katika dhambi, matokeo yake ilikuwa ni kila mmoja wa uzao wake pia utaathirika na "kuambukiziwa" dhambi. Daudi aliomboleza kwa ukweli huu katika mojawapo ya Zaburi zake: "Tazam mimi naliumbwa katika hali ya ouvu; maama yangu alinichukua mimba hatiani" (Zaburi 51:5). Hii haina maana kwamba mama yake alimzaa kimakosa; badala yake, mama yake alikuwa amerithi asili ya dhambi kutoka kwa wazazi wake, na hao kutoka kwa wazazi wao, na kadhalika. Daudi alirithi dhambi kutoka kwa wazazi wake, vile sisi wote hufanya. Hata kama sisi huishi maisha bora, sisi bado tu wenye dhambi kama matokeo ya dhambi ya urithi.

Jinsi tumezaliwa kwa ndambi matokeo ni kwamba sisi sote tu wenye dhambi. Tafakari vile inavyoendelezwa katika Warumi 5:12: dhambi iliingia duniani kupitia kwa Adamu, kifo kifuata dhambi, mauti huja kwa watu wote, watu wote hutenda dhambi kwa sababu ya kurithi dhambi ya Adamu. Kwa sababu "wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23), tunahitaji sadaka kamili, na isiyo ya dhambi kwa uosho wa dhambi zetu, jambo ambalo hatuna nguvu ya kufanya sisi wenyewe. Shukrani nyingi, Yesu Kristo ni Mwokozi wa dhambi! Dhambi zetu zimesulubiwa juu ya msalaba wa Yesu, na sasa "katika Yeye huyo kwa damu yake tuano ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawaswa na wingi wa neema yake" (Waefeso 1:7). Mungu, katika hekima yake isio na mipaka, ametoa dawa ya dhambi ya urithi wetu, na dawa ambayo ni inapatikana kwa kila mtu: "Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi" (Matendo 13:38).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, sisi wote tulirithi dhambi ya Adamu na Hawa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries