settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu alimwamuru Ibrahimu kumtoa Isaka kafara?

Jibu


Ibrahimu alikuwa amemtii Mungu mara nyingi katika kutembea kwake pamoja naye, lakini hakuna jaribio ambalo lingekuwa kali zaidi kuliko lililo katika Mwanzo 22 Mungu aliamuru, "Akasema, umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria,ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia" (Mwanzo 22: 2a). Hili lilikuwa ombi imara kwa sababu Isaka alikuwa mwana wa ahadi. Jinsi gani Ibrahimu alijibu? Kwa kutii mara moja; mapema asubuhi iliyofuata, IbrahImu alianza safari pamoja na watumishi wawili, punda na mwana wake mpendwa Isaka, na kuni kwa ajili ya sadaka.Kutii kwake kwa amri ya Mungu inayokanganya bila kuuliza kulimpa Mungu utukufu anaostahili na ni mfano kwetu jinsi ya kumtukuza Mungu. Tunapotii kama Ibrahamu, tukiamini kwamba mpango wa Mungu ndio bora zaidi,tunainua sifa zake na kumsifu. Kutii kwa Ibrahimu katika mtazamo wa amri hii ya kuangamiza kuliinua upendo huru wa Mungu, uaminifu wake, na wema wake, na alitoa mfano kwatu sisi kufuata. Imani yake katika Mungu alikuwa amemjua na upendo ulimweka Ibrahimu katika hekalu la miungu yote ya mashujaa waaminifu katika Waebrania 11.

Mungu anatumia imani ya Ibrahimu kama mfano kwa wote waliokuja baada yake kama njia pekee ya wokovu. Mwanzo 15: 6 inasema, "Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki." Ukweli huu ni msingi wa imani ya kikristo, kama ilivyorudiwa kusemwa katika Warumi 4: 3 na Yakobo 2:23. Haki ambayo ilikuwa sifa kwa Ibrahimu ni haki sawa na ile tuliyopewa wakati sisi tulipokea kwa imani sadaka abayo Mungu aliitoa kwa ajili ya dhambi zetu - Yesu Kristo. "Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye" (2 Wakorintho 5:21).

Hadithi ya Agano la Kale kuhusu Ibrahimu ni msingi wa mafundisho ya Agano Jipya ya upatanisho,toleo la sadaka ya Bwana Yesu juu ya msalaba kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu. Yesu alisema, karne nyingi baadaye, "Ibrahimu baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi "(Yohana 8:56). Zifuatazo ni baadhi ya tofauti kati agano mbili za Biblia:

• "Chukua mwanao, mwana wako wa pekee, Isaka" (v 2.); "Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwana wake wa pekee ..." (Yohana 3:16).

• "Nenda mkoa wa Moria.mtoe sadaka huko ... "(v 2.); inaaminika kwamba eneo hili ndipo mji wa Yerusalemu ulijengwa miaka mingi baadaye, mahali ambapo Yesu alisulubiwa nje ya kuta zake (Waebrania 13:12)

• "mtoe sadaka hapo kama sadaka ya kuchomwa" (v 2.); "Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na Maandiko" (1 Wakorintho 15: 3).

• "Ibrahimu akazichukua kuni za sadaka ya kuchomwa na kuziweka juu ya mwana wake Isaka" (mstari 6.); Yesu, "akibeba msalaba wake mwenyewe. . . "(Yohana 19:17).

• "Lakini ipo wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuchomwa?" (V 7.);yohana akasema, "Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, achukuaye dhambi za ulimwengu!" (Yohana 1:29).

• Isaka, mwana, alifanya kwa imani kwa baba yake katika kuwa sadaka (v 9.); Yesu akaomba, "Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kinipite. Hata hivyo si kama mimi nitakavyo, bali kama wewe utakavyo "(Mathayo 26:39).

• Kufufuka - Isaka (kitaswira) na Yesu kwa ukweli: "Kwa imani Ibrahimu, alipojaribiwa na Mungu, alimtoa mwanae Isaka kama sadaka. Yeye ambaye alikuwa amepokea ahadi alikuwa karibu kumtoa sadaka mwanaye mmoja wa kipekee, ingawa Mungu alikuwa amenena kwake kwamba, 'Ni kupitia kwa Isaka watoto wako watahesabiwa.'Ibrahimu alidhani kwamba Mungu atamfufua mfu, na kuongea kitaswira ,alimpokea Isaka kutoka kwa mauti "(Waebrania 11: 17-19);. Yesu, "kwamba alizikwa, na kwamba alifufuliwa siku ya tatu kulingana na maandiko" (1 Wakorintho 15: 4).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu alimwamuru Ibrahimu kumtoa Isaka kafara?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries