settings icon
share icon
Swali

Kanisa ni nini?

Jibu


Watu wengi siku hizi wanaelewa kanisa kumaanisha jengo. Huku si kuelewa kibibilia maan ya kanisa. Neno “kanisa” maana ya asili yatoka kwa neno la Kiyunani ekklesia lili lo na maana ya “kusanyiko” au “walioitwa.” Maana ya asili ya “kanisa” sio ile ya jingo, bali ni watu. Ni kinaya kwamba unapowauliza watu ni kanisa gani wanashiriki, mara nyingi huwa wanajihushisha na jingo. Warumi 6:5, yasema, “…salimia kanisa linalokutana kwa nyumba.” Paulo anaashiria kanisa lilo katika nyumba yao- si jengo la kanisa bali mwili wa washiriki.

Kanisa ni mwili wa Kristo, ambapo ye ndie kichwa. Waefeso 1:22-23 yasema, “Akivitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” Mwili wa Kristo umejengwa na wanaoamini katika Yesu Kristo toka siku ya Pentekosti (Matendo Ya Mitume 2) hadi Kristo arudi. Mwili wa Kristo uko na sehemu mbili:

1) Kanisa lote kwa ujumula ambalo ni wale wote wako na uhusiano na Kristo. “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni Upendo” (1 Wakorintho 12:13). Aya hii inasema yeyote atakaye amini in sehemu ya mwili wa Kristo na ameupokea Roho wa Kristo ni ushaidi. Kanisa la jumla la Mungu ni wale wote ambao wamepokea wokovu kwa imani katika Yesu

2) Lile Kanisa ya nyumbani vile emeelezwa katia Wagalatia 1:1-2: “Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), na ndugu wote walio pamoja name, kwa makanisa ya Galatia.” Hapa tunaona kwamba katika mkoa (mji) wa Galatia kulikuwa na makanisa mengi chenye tunaita makanisa ya nyumbani. Kanisa la Kibaptisiti, Kilutheri, Katholiki na mengine, si kanisa, vile iilvyo katika kanisa la ujumla, bali haya ni makanisa ya nyumbani (Mshambani/Mjini), ule mwili wa nyumbania wa waumini. Kanisa la jumla linajumlisha wale wote ni wa Kristo na wamemwamini kwa wokovu. Washirika wa kanisa la jumla lazima watafute kuwa na ushirika na kujengana wakiwa katika lile kanisa la nyumbani.

Kwa ufupi, kanisa si jingo ama dini. Kulingana na Bibilia, kanisa ni mwili wa Krsito-wale wote wameweka imani yao kwa Yesu Kristo kwa wokovu (Youhana 3:16; 1 Wakorintho 12:13). Kanisa la nyumbani ni kusanyiko la Wakristo wa kanisa la jumla. Kanisa la nyumbani ni mahali ambapo washirika wa kanisa la jumla wanaweza kutumia nguz0 ya “mwili” ya 1 Wakorintho 12: himizana, funzaneni, na kujengana ninyi kwa ninyi katika hekima na neema ya Bwana Yesu Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kanisa ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries