settings icon
share icon
Swali

Kwa nini tunahitaji kukiri dhambi zetu kama tayari zimekwisha samehewa 1 Yohana 1:9)?

Jibu


Mtume Paulo aliandika, "Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huhu Mpendwa. Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujizi" (Waefeso 1:6-8). Msamaha huu unamaanisha wokovu, ambao Mungu amechukua dhambi zetu na kuondolewa kwao kutoka kwetu "mbali kama mashariki ilivyo mbali na magharibi" (Zaburi 103:12). Huu ni msamaha wa mahakama kwamba Mungu anatupa juu ya kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi. Dhambi zetu zote za zamani, sasa, na baadaye zimesamehewa kwa misingi ya kimahakama, kwa maana ya kuwa sisi huteseka hukumu ya milele kwa dhambi zetu. Bado sisi kila huadhiriwa na na madhara ya dhambi wakati tuko hapa duniani, hata hivyo, ambayo inatufanya tunajiuliza maswali.

Tofauti kati ya Waefeso 1:6-8 na 1 Yohana 1:9 ni kwamba yohana anashughulika na kile tunachokiita msamaha wa "kimahusiano," au "familia," kama ule wa baba na mwana. Kwa mfano, kama mwana akifanya makosa kwa baba- kukosa kufikia matarajio yake au sheria - mtoto huyo ameuzuia ushirika wake na baba yake. Yeye bado ni mtoto wa baba yake, lakini uhusiano anaadhirika. Ushirika wao utakuwa wa mpaka hadi mwana akubali kwa baba yake kwamba amefanya kosa. Hiyo na sawa na Mungu; ushirika wetu pamoja naye utaadhirika hadi tukiri dhambi zetu. Wakati sisi hukiri dhambi zetu kwa Mungu, ushirika utarejeshwa. Huu ni msamaha wa mahusiano.

Msamaha wa "nafasi", au msamaha wa mahakama, ni ule ambao unapatikana kwa kila muumini katika Kristo. Katika msimamo wetu kama viungo vya mwili wa Kristo, tumekwisha samehewa kila dhambi ambazo tumetedna au milele kufanya. Bei ya iliyolipwa na Kristo juu ya msalaba imeridhisha hasira ya Mungu dhidi ya dhambi, na hakuna sadaka zaidi au malipo ambayo ni muhimu. Wakati Yesu aliposema, "Imekwisha ," Yeye alimaanisha. Msamaha wetu wa nafasi ulipatikana kisha na pale.

Ungamo la dhambi utasaidia kutuepusha kutoka kwa nidhamu ya Bwana. Kama tunashindwa kukiri dhambi, nidhamu ya Bwana kwa hakika itakuja hadi pale tutakapo kiri kwake. Kama nilivyosema hapo awali, dhambi zetu zimesamehewa ile saa ya wokovu (msamaha kwa nafasi hii), lakini ushirika wetu wa kila siku na Mungu unahitaji kukaa katika msimamo mzuri (msamaha wa mahusiano). Ushirika sahihi na Mungu haiwezi kutokea kwa kuungama dhambi katika maisha yetu. Kwa hiyo, tunahitaji kuungama dhambi zetu kwa Mungu kwa haraka pindi tu tunapofahamu kwamba tumefanya dhambi, ili kudumisha ushirika wa karibu na Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini tunahitaji kukiri dhambi zetu kama tayari zimekwisha samehewa 1 Yohana 1:9)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries