settings icon
share icon
Swali

Je, binadamu kweli ana mapenzi hiari?

Jibu


Kama "hiari" ina maana kwamba Mungu huwapa wanadamu nafasi ya kufanya uchaguzi ambao kwa dhati huathiri hatima yao, basi naam, binadamu wana mapenzi ya hiari. Sasa hali ya dhambi ya duniani moja kwa moja inahusishwa na uamuzi uliofanywa na Adamu na Hawa. Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake mwenyewe, na hiyo ni pamoja na uwezo wa kuchagua.

Hata hivyo, mapenzi hiari haina maana kwamba mwanadamu anaweza kufanya kitu chochote atakavyo. Uchaguzi wetu ni mdogo kulingana na hali yetu ya asili. Kwa mfano, mtu anaweza kuamua kutembea katika daraja au kutotembea juu yake, chenye anaweza kuamua kutofanya ni kuruka juu ya daraja hiyo- asili yake humzuia kuruka. Katika njia sawa, mtu hawezi kuchagua kujifanya kuwa mwema - asili yake ya (dhambi) humzuia kufuta hatia yake (Warumi 3:23). Kwa hiyo, mapenzi hiari yamezuiliwa na asili.

Tatizo hili halipunguzi uwajibikaji wetu. Biblia ii wazi kwamba si uwezo wa kuchagua tuko nao pekee, pia tuko na wajibu wa kuchagua kwa busara. Katika Agano la Kale, Mungu alichagua taifa (Israeli), lakini watu ndani ya hilo taifa bado walikua na wajibu wa kuchagua kumtii Mungu. Na watu binafsi nje ya Israeli walikuwa na uwezo wa kuchagua kuamini na kumfuata Mungu vile vile (kwa mfano, Ruth na Rahabu).

Katika Agano Jipya, wenye dhambi wameamurishwa tena na tena "kutubu" na "kuamini" (Mathayo 3:2; 4:17; Matendo 3:19, 1 Yohana 3:23). Kila wito wa kutubu ni wito wa kuchagua. Amri ya kuamini yachukulia kwamba msikilizaji anaweza kuchagua kutii amri.

Yesu alitambua tatizo la baadhi ya wasioamini wakati Aliwaambia, "Nyinyi mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima" (Yohana 5:40). Ni wazi, wangeweza kuja kama wangetaka, tatizo lao lilikuwa kwamba waliamua kinyume. "Mtu huvuna kile alipanda" (Wagalatia 6:7), na wale walio nje ya wokovu hawana "udhuru" (Warumi 1:20-21).

Lakini ni jinsi gani mwanadamu, tuliyezuiliwa na asili ya dhambi, milele kuchagua jambo jema? Ni kupitia tu kwa neema na nguvu ya Mungu kwamba mapenzi hiari yanakuwa "huru" kwa maana ya kuwa na uwezo wa kuchagua wokovu (Yohana 15:16). Ni Roho Mtakatifu ambaye anafanya kazi katika na kwa mapenzi ya mtu humfanya upya mtu huyo (Yohana 1:12-13) na kutoa hali mpya "kuumbwa kuwa kama Mungu katika haki na utakatifu wa kweli yake"(Waefeso 4:24). Wokovu ni kazi ya Mungu. Wakati huo huo, nia yetu, tamaa, na vitendo ni hiari, na sisi tutawajibika kwa ajili yao.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, binadamu kweli ana mapenzi hiari?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries