settings icon
share icon
Swali

Je, kweli kuna Mbinguni?

Jibu


Mbinguni kwa kweli ni mahali halisi. Biblia inatuambia kwamba mbinguni ni kiti cha enzi cha Mungu (Isaya 66:1, Matendo 7:48-49, Mathayo 5:34-35). Baada ya kufufuka kwa Yesu na kuonekana kwake duniani kwa wanafunzi wake, "Alichukuliwa mbinguni akaketi mkono wa kuume wa Mungu" (Marko 16:19, Matendo 7:55-56). "Kwa sababu Kristo katika hakuingia palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni has, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu" (Waebrania 9:24). Yesu hakuingia kabla yetu tu pekee, kuingia kwa niaba yetu, bali yeye yu hai na ana huduma sasa hivi mbinguni, akihudumu kama kuhani wetu mkuu katika ile hema ya kweli iliyotengezwa na Mungu (Waebrania 6:19-20; 8:1-2).

Pia tunaambiwa na Yesu mwenyewe kwamba kuna vyumba vingi nyumbani mwa Mungu, na kwamba Yeye amekwenda mbele yetu kuandaa mahali kwa ajili yetu. Tuna uhakika wa neno lake kwamba siku moja atarudi duniani na kutupeleka ambapo kwenye yeye ako sasa mbinguni (Yohana 14:1-4). Imani yetu katika makao ya milele mbinguni msingi wake uu katika ahadi kamili ya Yesu. Mbinguni dhahiri zaidi ni mahali halisi. Mbinguni kwa kweli ipo.

Wakati watu hukana kuwepo kwa mbinguni, hawalikatai neno la Mungu tu lililoandikwa, bali pia hukataa tamaa za ndani ya mioyo yao wenyewe. Paulo alisungumzia suala hili katika barua yake kwa Wakorintho, na kuwahamasisha kushikamana na matumaini ya mbinguni ili waziweze kupoteza matumaini. Ingawa sisi "tunaugua na wanaougua" katika hali yetu ya dunia, tuna matumaini ya mbinguni mbele yetu na siku zote tutathamani kufika huko (2 Wakorintho 5:1-4). Paulo aliwahimiza Wakorintho kulenga mbele katika makao yao ya milele mbinguni, mtazamo ambao atawawezesha kuvumilia matatizo na kukatishwa tamaa katika maisha haya. "Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatuafanyia utukufu wa milele izidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele"(2 Wakorintho 4:17-18).

Kama vile Mungu ameweka katika mioyo ya watu maarifa kuwa yeye yuko (Warumi 1:19-20), hivyo sisi "tuliyoumbwa" kuwa na hamu ya mbinguni. Ni mandhari ya vitabu visivyoweza hesabika, nyimbo na kazi ya sanaa. Kwa bahati mbaya, dhambi zetu zimezuia njia ya kwenda mbinguni. Tangu mbinguni ni makaazi ya Mungu mtakatifu na mkamilifu, dhambi haina mahali huko, wala hawezi kuvumiliwa. Kwa bahati nzuri, Mungu ametoa kwa ajili yetu ufungua wa milango ya mbinguni, Yesu Kristo (Yohana 14:6). Wote wanaoamini yeye na kutafuta msamaha kwa dhambi hupata milango ya mbinguni imefunguliwa wazi kwa ajili yao. Na iwe kuwa utukufu ujao wa makao yetu ya milele utuhamasishe sisi wote kumtumikia Mungu kwa uaminifu na kwa moyo wote. "Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliy mpya, iliyo hai, ipitiayo katika pazia, yaani, mwili wake; na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; na tukaribie wenye moyo wa kweli kwa ukamilifu wa imani, hali tumenyunyiziziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi" (Waebrania 10:19-22).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kweli kuna Mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries