settings icon
share icon
Swali

Uariani ni nini?

Jibu


Uariani umepewa jina kwa ajili Arius, mwalimu katika karne ya 4 A.D. Mojawapo ya hoja muhimu zaidi ya mjadala kati ya Wakristo wa kwanza ilikuwa juu ya uungu wa Kristo. Alikuwa kweli Yesu kweli alikuwa Mungu katika mwili au Yesu alikuwa kiumbe? Yesu alikuwa Mungu au kama Mungu tu? Arius ulishikilia kwamba Yesu aliumbwa na Mungu kama tendo la kwanza la viumbe, kwamba Yesu alitwikwa taji ya utukufu ya viumbe vyote. Uariani, basi, ni mtazamo kwamba Yesu alikuwa kiumbe na sifa ya Mungu, lakini hakuwa Mungu katika nafsi yake.

Waariani wanakosa kuelewa marejeo ya Yesu kuwa na uchovu (Yohana 4:6) na kutojua tarehe ya kurudi kwake (Mathayo 24:36). Naam, ni vigumu kuelewa jinsi Mungu anaweza kuwa amechoka na / au akose kujua kila kitu, lakini kumdunisha Yesu hadi kiumbe siyo jibu. Yesu alikuwa Mungu kamili, lakini pia alikuwa mwanadamu kamili. Yesu hakuwa mwanadamu hadi wakati alipokuwa na mwili. Kwa hiyo, mapungufu ya Yesu kama binadamu hayana madhara kwa asili yake ya kiungu au umilele wake.

Tafsiri ya pili baya katika Uariani ni maana ya "mzaliwa wa kwanza" (Warumi 8:29; Wakolosai 1:15-20). Waariani huelewa "mzaliwa wa kwanza" katika mistari hii kuwa na maana ya kwamba Yesu "alizaliwa" au "kuumbwa" kama tendo la kwanza la viumbe. Hii si kesi. Yesu mwenyewe alitangaza kuwepo kwake binafsi na Umilele (Yohana 8:58; 10:30). Yohana 1:1-2 inatuambia kwamba “Yesu alikuwa na Mungu katika mwanzo na Mungu.” Katika nyakati za Biblia, mzaliwa wa kwanza wa familia aliheshika pakubwa sana (Mwanzo 49:3 "katika mwanzo na Mungu."; Kutoka 11:5; 34:19 na Hesabu 3:40, Zaburi 89:27; Yeremia 31:9). Ni katika maana hii ambayo Yesu ni mzaliwa wa kwanza wa Mungu. Yesu ni mwanachama fahari wa familia ya Mungu. Yesu ni mtiwa wakivu wa Mungu, "Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani" (Isaya 9:6).

Baada ya karibu karne ya mjadala mbalimbali katika baraza la kanisa la mapema, Kanisa la Kikristo kirasmi lilikataa Uariani kama mafundisho ya uongo. Tangu wakati huo, Uariani haijawahi kukubaliwa kama mafundisho faida ya imani ya Kikristo. Uariani haujakufa, hata hivyo. Uariani umekuwa ukiendelea katika karne tofauti. Mashahidi wa Yehova na Wamormoni wa leo hushikilia sana msimamo kama ule wa Uariani kuhusu mwili wa Kristo. Kama vile Kanisa la kwanza lilifanya, sisi pia lazima tukemee mashambulizi yoyote yale kwa Uungu wa Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Uariani ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries