settings icon
share icon
Swali

Ufasiri wa ndoto wa kikristo? Je! Ndoto zetu zatoka kwa Mungu?

Jibu


Gotquestion.org si huduma ya kufasiri ndoto za kikristo. Hatufasiri ndoto. Kwa dhati tunaamini kuwa ndoto ya mtu na maana ya ndoto hizo zi kati yao na Mungu peke. Je! Mungu bado ananena kupitia kwa ndoto? Mungu alinena na watu mara nyingi sana kwa maandiko kupitia kwa ndoto. Kwa mfano Yusufu, mwana wa Yakobo (Mwanzo 37:5-10); Yusufu, mumewe Mariamu (Mathayo 2:12-22); Suleimani ( 1 Wafalme 3:5-15); na wengine wengi (Danieli 2:1; 7:1; Mathayo 27:19). Pia kunao unabii wa nabii Yoeli (Yoeli 2:28), umenukuliwa na mtume Petro katika Matendo Ya Mitume 2:17, ambao wataja kutumika kwa ndoto. Kwa hivyo jibu rahisi ni, naam, Mungu anaweza na huzungumza kupitia kwa ndoto.

Ingawa, kunayo tofauti jinsi tunavyo tumia kweli hiyo hii leo. Lazima tukumbuke kwamba, Bibilia imekamilika, baada ya kufunua kila kitu tunastahili kujua tangu sasa hadi milele. Hii si kusema kwamba Mungu hatendi miujiza au kunena kupitia kwa ndoto hii leo, lakini cho chote Mungu anasema hata kama ni ndoto, maono, picha, au “sauti ya chini,” tunakubaliana kabisa na chenye kimekwisha funuliwa katika neno lake. Ndoto haziwezi wekwa katika nafasi ya mamlaka kupita maandiko.

Kama uko na ndoto na unahisi kwamba Mungu alikupa hiyo ndoto, kwa maombi lichunguze neno la Mungu na akikisha ndoto yako inakubaliana na maandiko. Kama ni hivyo, kwa maombi kichukulie kile Mungu angekutaka ufanye kulingana na ndoto yako (Yakobo 1:5). Katika maandiko, popote mtu yeyote alipata ndoto kutoka kwa malaika, au kupitia kwa mtume (Mwanzo 40:5-11; Danieli 2:45, 4:19). Wakati Mungu ananena nasi, Anaakikisha kuwa ujumbe wake umeeleweka vizuri.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ufasiri wa ndoto wa kikristo? Je! Ndoto zetu zatoka kwa Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries