settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje juu ya vyakula tunapaswa kula (kosher)? Je, kuna vyakula Mkristo anapaswa kuepuka?

Jibu


Mambo ya Walawi sura ya 11 inaorodhesha vikwazo vya vyakula Mungu alilipa taifa la Israeli.Sheria za vikwazo vya vyakula ni pamoja na makatazo dhidi ya nyama ya nguruwe, samakigamba, wadudu wengi,ndege wala mizoga, na wanyama wengine mbalimbali.Sheria za vikwazo vya vyakula hazikutarajiwa kamwe kutumika kwa mtu yeyote ila tu waisraeli pekee.Lengo la sheria za vyakula lilikuwa kuwafanya waisraeli kujitenga na mataifa mengine yote. Baada ya kusudi hili kumalizika, Yesu alikiri vyakula vyote kuwa safi (Marko 7:19). Mungu alimpa mtume Petro maono ambayo kwayo alikiri kwamba wanyama ambao hawakuliwa mwanzoni watakuwa wakiliwa: "Usikitaje chochote ambacho Mungu amekifanya kuwa safi kwamba ni kichafu" (Matendo ya mitume 10:15). Wakati Yesu alikufa msalabani, Alitimiza sheria za Agano la Kale (Warumi 10: 4; Wagalatia 3: 24-26, Waefeso 2:15). Hizi ni pamoja na sheria kuhusu vyakula safi na visivyokuwa safi.

Warumi 14: 1-23 inatufundisha kwamba si kila mtu amekomaa katika imani kwa kukubali ukweli halisi kwamba vyakula vyote ni safi. Matokeo yake,ikiwa tuko na atakayeudhishwa na kula kwetu "vyakula chafu", tunapaswa kutamaukwa haki yetu ya kufanya hivyo,ili tusimuudhi huyo mtu. Tuna haki ya kula chochote tutakacho, lakini hatuna haki ya kuwaudhi watu wengine, hata kama wamekosea. Kwa Mkristo katika umri huu, ingawa,tuna uhuru wa kula chochote tunataka bora kisimfanye mtu yeyote yule kuyumbayumba kwa imani yake.

Katika Agano Jipya la neema, Biblia imehusika sana na ni kiasi gani tunachokula kuliko kile tulacho. Tamaa ya kimwili ni uwezo wetu wa kale kujidhibiti sisi wenyewe. Kama hatuwezi kudhibiti tabia yetu ya kula,vivyo hivyo pia hatuwezi kudhibiti tabia zingine kama vile zile za akili (tamaa ya mwanamke, tamaa ya mali ya wengine, chuki na hasira visivyo adilifu) na hatuwezi kuzuia midomo yetu kutoka uvumi au ugomvi.Hatufai kuruhusu tamaa zetu kutudhibiti ; badala yake,tusidhibiti sisi (Kumbukumbu 21:20, Mithali 23: 2; 2 Petro 1: 5-7; 2 Timotheo 3: 1-9; 2 Wakorintho 10: 5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje juu ya vyakula tunapaswa kula (kosher)? Je, kuna vyakula Mkristo anapaswa kuepuka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries