settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Wayahudi na Waarabu/Waislamu wanawachukia?

Jibu


Kwanza, ni muimu kuelewa kwamba si Waarabu wote ambo ni Waislamu, na si kila Mwislamu ni Mwaraabu. Huku kukiwa kuwa wengi wa Waarabu ni Waislamu, kuna Waarabu wengi ambao si Waislamu. Zaidi, kuna Waarabu wengi sana wa muimu ambao si Waislamu katika mataifa kama Indonesia na Malaysia kuliko vile walipo Waislamu Waarabu. Pili, ni muimu kukumbuka kwamba si Waarabu wote wanawachukia Wayahudi, si Waislamu wote wanawachukia Wayahudi, si Wayahudi wote wanawachukia Waislamu. Lazima tuwe macho ili tuepuke kuwabagua watu. Ingawa, kwa kuzungumza kijumla, Waarabu na Waislamu ile chuki na kutokuwa na imani na Wayahudi.

Kama kunao elezo kamilifu la kibibilia kwa uadui huu, elezo hilo larudi nyuma hadi Abrahamu. Wayahudi ni uzao wa Isaka mwana wa Abrahamu. Waarabu ni uzao wa Ishmaeli mwana wa Abrahamu. Ishmaeli kuwa mwana wa mke mtumwa (Mwanzo 16:1-16) na Isaka kuwa mwana wa ahadi ambaye ataridhi baraka za Abrahamu (Mwanzo 21:1-3), kawaida kutakuwa na uadui kati ya hao wana wawili. Kwa ajili ya Ishmaeli kumkejeri Isaka (Mwanzo 21:9), Sara akamwambia Abrahamu awafukuze Haga na Ishmaeli (Mwanzo 21:11-21). Pengine hii ilileta kutoridhika moyoni mwa Ishmaeli kwa nduguye Isaka. Malaika alitabiria Haga kuwa Ishmaeli “ataishi kwa uadui na nduguze wote”(Mwanzo 16:11-12).

Dini ya Kiislamu, ambayo wengi wa Waarabu wanaifuata, imeleta uadui huu kuwepo. Qurán iko na maelezo ya utata kwa Waislamu kuhusu Wayahudi. Kwa upande mmoja inawaamrisha Waislamu kuwachukulia Wayahudi kama ndugu na wakati mwingine yawaamrisha Waislamu kuwakabili Wayahudi wanaokataa kugeuka kuwa Waislamu. Qur’an pia yawaziliza mfutano kuwa kwa wana wa Abrahamu ni nani alikuwa mwanawe halisi wa ahadi. Bibilia ya Kiibrania yasema ni Isaka. Qur’an yasema ni Ishmaeli. Qur’an yafunza kuwa ni Abrahamu alikuwa karibu kumtoa kama sadaka kwa Mungu, si Isaka (hii yahitilafiana na Mwanzo 22). Mjadala kuhusu ni nani aliyekuwa mwana wa ahadi wachangia uadui hii leo.

Hata hivyo asili ya uchungu kati ya Isaka na Ishmaeli haielezi uadui wote kati ya Wayahudi na Waarabu hii leo. Kwa kweli kwa maelifu ya miaka historia ya Bara Asia, Wayahudi na Waarabu waliishi kwa amani na tofauti miongoni mwao. Chanzo halisi cha uadui uko ni sawa na asili ya uadui wa hivi sasa. Baada ya vita vya II vya dunia, wakati nchi za Umoja wa Mataifa zilitoa sehemu ya ardhi ya Waisraeli na kuwapa Wayahudi, ardhi ilikuwa wakati huo ilikuwa imechukuliwa na Waarabu (Wapalestina). Waarabu wengi walifanya maandamano kupinga taifa la Israeli kukaa katika ardhi yao. Nchi za kiarabu ziliungana pamoja na kuwafamia Waisraeli kwa jaribio la kuwafukuza kutoka kwa nchi yao, lakini walishindwa. Tangu wakati huo kumekuwa na uadui kati ya Waisraeli na majirani wao Waarabu. Israeli inakaa katika ardhi ndogo sana amboyo imezungukukwa na mataifa makubwa ya Kiarabu kama Jordani, Siria,Saudi Arabia, Iraq na Misri. Ni mtazamo wetu kuwa, kunena kibibilia, Israeli iko na haki ya kuishi kama taifa katika nchi yao ambayo Mungu aliwapa uzao wa Yakobo, wajukuu wa Abrahamu. Kwa wakati huo huo, tunaamini kwa dhati kuwa Israeli lazima itafute amani na kuonyesha heshima kwa mataifa jirani ya Kiarabu. Zuburi 122:6 yasema, “Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wekupendao.”

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Wayahudi na Waarabu/Waislamu wanawachukia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries