settings icon
share icon
Swali

Je Yesu alisulubiwa siku ya Ijumaa?

Jibu


Bibilia haitaja kikamilifu ni siku gani ya juma Yesu alifufuka. Siku mbili zinazo kisiwa sana ni Ijumaa na Jumatano. Ingawa wengine hutumia dhana ya Ijumaa na Jumatano na kusema Alhamisi ndio siku sawa.

Yesu alisema katika Mathayo Mtakatifu 12:40, “Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi” wale wanaoshikilia kuwa Ijumaa ndio ilikuwa siku ya kusulubiwa, wanasema kuna hali halisi amboyo Yesu anakisiwa kuwa kaburini siku tatu. Katika fikira ya Kiyahudi katika karne ya kwanza, sehemu ya siku ilichukuliwa kuwa siku nzima. Jinsi Yesu alikuwa kaburini sehemu ya siku ya Ijumaa, Jumamosi nzima na sehemu ya siku ya Jumapili anachukuliwa kuwa kaburini siku tatu. Mojawapo ya dhana kuu ya Ijumaa inapatikana katika Mariko Mtakatifu 15:42, ambayo inasema kuwa Yesu alisulubiwa “siku iliyo kabla ya sabato” Kama hiyo ilikuwa sabato ya kila juma, kwa mfano Jumamosi, kwa hivyo hiyo hoja huasiria Ijuma kuwa siku halisi ya kusulubiwa. Funzo lingine kuhusu siku ya Ijumaa lasema kifungo kama Mathayo Mtakatifu 16:21 na Luka Mtakatifu 9:22, za funza kwamba Yesu angefufuka siku ya tatu; kwa hivyo, hangehitaji kuwa kaburini siku tatu mchana na usiku. Tafusiri zingine zinapotafusiri “katika siku ya tatu” kwa hizi aya, si zote, na si kila mmoja anakubaliana kwamba “siku ya tatu” ndio njia nzuri ya kutafusiri aya hizi. Zaidi ya hayo, Mariko Mtakatifu 8:31 yasema kwamba Yesu atafufuliwa “baada” ya siku tatu.

Wanaoshikilia siku ya Alhamisi wanafafanua dhana ya Ijumaa na wanapinga kwamba kuna matukio mengi (wengine wanahesabu hadi ishirini) yaliotokea kati ya kuzikwa kwa Yesu na Jumapili asubuhi kutoka Ijumaa jioni hadi Jumamosi asubuhi. Wanaoiunga dhana ya mtazamo wa Alhamisi, wanaichukulia hii kuwa shida wakati siku nzima pekee kati ya Ijumaa na Jumapili ilikuwa Jumamosi. Mawakili wa Alhamisi wasema: ikiwa hujamwona rafiki tangu Jumatatu jioni. Wakati mwingine utakapomwona ni Alhamisi asubuhi na useme, “Sijakuona yapata siku tatu sasa” hata kama ingekuwa ni saa 60 zilikuwa zimepita (siku 2.5). kama Yesu alisulubiwa siku ya Alhamisi, mfano huu waonyesha vile inaweza chukuliwa siku tatu

Wazo la Jumatano lasema kwamba kulikuwa na sabato mbili katika juma hilo. Baada ya lile la kwanza (lile lilo tokea ile jioni ya kusulubiwa [Mariko 15:42; Luka 23:52-54]), wamama walinunua manukato, si eti waliyanunua baada ya sabato (Mariko 16:1). Wanaoshikilia Jumatano wanasisitiza ya kwamba hii “sabato” ilikuwa pasaka (soma Mambo ya Nyakati 16:29-31, 23:24-32, 39 mahali ambapo siku kuu si lazima ni ile ya saba ya juma tunaambiwa kwamba ni sabato). Sabato ya pili ilikuwa ile ya kawaida ambayo ni siku ya saba ya juma. Kumbuka kwamba, katika Luka 23:56 wanawake waliokwisha nunua manukato katika sabato ya kwanza walirudi na kufanya kuwa tayari manukato na baadaye wakapumzika “siku ya sabato” (Luka 23:56). Katika jadilio lao husema hawangeweza kununua manukato baada ya sabato, na wakafanya tayari hayo manukato kabla ya sabato, labda kuwe kulikuwa na sabato mbili. Na hiyo dhana ya sabato mbili, kama Yesu alisulubiwa siku ya Alhamisi, kwa hivyo sabato takatifu (pasaka) ingekuwa imeanza Alhamisi jioni na kuisha Ijumaa jioni mwanzo wa kila sabato ya juma (Jumamosi). Kununua manukato baada ya sabato ya kwanza (pasaka) ingemaanisha waliyanunua Jumamosi walipokuwa wamemaliza sabato.

Kwa hivyo, kulingana na mtazamo wa Jumatano, elezo pekee ambalo halivunji matukio ya bibilia ya wanawake na manukato unashikilia kuelewa juu juu Mathayo 12:40 ya kwamba Kristo alisulubiwa Jumatano. Sabato ambayo ilikuwa siku kuu (pasaka) ilitukia Alhamisi, ambayo wanawake walinunua manukato (baada ya hiyo) siku ya Ijumaa walirudi na kuyatarisha manukato hayo siku hiyo, wakapumzika siku ya Jumamosi ambayo ilikuwa sabato ya juma, kisha wakaleta manukato kaburini Jumapili asubuhi. Yesu alizikwa yapata saa za jioni siku ya Jumatano, ambayo kwa kalenda ya Kiyahudi ilikuwa inaanza Alhamisi. Kwa kutumia kalenda ya Kiyahudi tuko na usiku wa Alhamisi (usiku wa kwanza), Alhamisi mchana (mchana wa kwanza), Ijumaa usiku (usiku wa pili), Ijumaa mchana (mchana wa pili), Jumamosi usiku (Usiku wa watatu), Jumamosi mchana (mchana wa tatu). Hatujui kamili wakati alifufuka, lakini tunajua ni kabla ya jua kuchomoka siku ya Jumapili (Yohana 20:1, Mariamu Magdalene akaja “alfajiri, kungali giza bado” kwa hivyo alifufuka mapema baada ya jua kutua baada ya Jumamosi jioni, ambayo ilianza siku ya kwanza ya juma kulingana na wayahudi.

Shida inayoweza ambatana na mtazamo wa siku ya Jumatano wanafunzi waliotembea na Yesu barabarani kuelekea Hekaluni “siku ile” alifufuka (Luka 24:13). Wanafunzi hao hawakuweza kumtambua Yesu, wanamwelezea juu ya ufufuo wa Yesu, na wanasema kwamba “leo siku ya tatu tangu haya mambo yatokee” (24:22) Jumatano hadi Jumapili ni siku nne. Maelezo yanayoweza kuwa kweli ni kwamba pengine walianza kuhesabu kwanzia Jumatano jioni baada ya kuzikwa kwa Yesu, ambayo yaanza Alhamisi kulingana na kalenda ya Kiyahudi na Alhamisi hadi Jumapili inaweza hesabika siku tatu.

Katika mpangilio wa siri wa jumla wa vitu, si kitu cha muimu kujua ni siku gani ya juma Kristo alisulubiwa. Kama ilikuwa ya maana,hivyo ulimwengu wa Mungu ungetangaza wasi wasi siku na kadirio la muda. Kilicho cha maana ni, alikufa kifo cha kawaida, mwili wake ukafufuliwa kutoka kwa wafu. Kilicho cha maana sawa ni sababu iliyokufia- ili achukue adhabu amboyo wenye dhambi wote wanastahili. Yohan Mtakatifu 3:16 na 3:36 zote zatangaza ya kwamba kuweka imani yako kwake yaleta uzima wa milele. Huu ni ukweli sawa hata kama alisulubiwa Jumatano, Alhamisi ama Ijumaa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je Yesu alisulubiwa siku ya Ijumaa? Kama ni hivyo, ni namna gani alimaliza siku tatu kaburini kama alifufuka Jumapili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries