settings icon
share icon
Swali

Je! Yamaanisha nini kuwa Yesu aokoa?

Jibu


“Yesu aokoa” ni mustari unaupata katika sehemu za gari, alama katika matukio ya riadha, hata mabango ya kufutwa hewani na zile ndege ndogo. Cha kuhuzunisha, wachache waonao ujumbe “Yesu aokoa” kwa kweli wanaelewa na kujua inamaanisha nini. Kuna wingi wa nguvu ambazo zimewekwa katika maneno hayo.

Yesu aokoa, lakini huyu Yesu ni nani?
Watu wengi wanaelewa kuwa Yesu alikuwa mt ambaye aliishi Israeli miaka 2000 iliyopita. Takribani kila dhehebu ulimwenguni lamchukulia Yesu kama mwalimu mwema/nabii. Huku hayo mambo yakiwa kweli kuhusu Yesu, hayaangazii kabisa Yesu kwa ni nani, ama kuelezea jinzi au kwa nini Yesu aokoa. Yesu ni Mungu katika mwili wa binadamu (Yohana 1:1,14). Yesu ni Mungu, alikuja ulimwenguni kama mwanadamu wa kweli (1Yohana 4:2). Mungu alikuja akawa mwanadamu katika Yesu ili atuokoe. Hiyo yaleta swali lifuatalo: Ni kwa nini tunaitaji kuokolewa?

Yesu aokoa, lakini ni kwa nini tunahitaji kuokoka?
Biblia yatangaza kuwa kila mwanadamu ambaye amewai ishi ametenda dhambi (Mhubiri 7:20; Warumi 3:23). Kusini ni kutenda jambo baya, hata kama ni kupitia mawazo, maneno au tendo ambalo lahitilafiana na tabia kamilifu ya Mungu. Kwa sababu ya dhambi zetu, wote tunastahili hukumu kutoka kwa Mungu (Yohana 3:18,36). Kwa ukamilifu Mungu ni mwenye haki, kwa hivyo hawezi kuruhusu dhambi na uovu viende huru bila kuadhibiwa. Jinsi Mungu anaishi milele, na jinsi dhambi zote ni kinyume na Mungu (Zaburi 51:4), hukumu ya milele ndio pekee inazifaa. Mauti ya milele ndio hukumu ya haki kwa dhambi. Ndio sababu tunastahili kuokoka.

Yesu aokoa, lakini anaokoa namna gani?
Kwa sababu tumenda dhambi kinyume na Mungu aishiye milele, pengine mtu (sisi) asiyeishi milele atalipa karama ya dhambi zetu kwa wakati usio na kadirio, au mtu aishiye milele (Yesu) lazima alipie dhambi zetu wakati mmoja. Hamna njia nyingine mpadala. Yesu atuokoa kwa kufa kwa ajili yetu. Katika utu wa Yesu Kristo, Mungu alijitolea yeye mwenyewe kama dhabihu kwa niapa yetu, kwa kulipia adhabu ya milele ambayo ni Yeye pekee angeweza kuilipa (1Wakorintho 5:21; 1Yohana 2:2). Yesu alichukua hukumu ambayo tunastahili ili atuokoe kutoka hatima mbaya sana ya milele, haki ya kweli ya madhara ya dhambi zetu. Kwa sababu ya wingi wa upendo wake, Yesu aliyatoa maisha yake (Yohana 15:13), na kulipa adhabu ambayo tulijichukulia, lakini hatungeweza kuilipa. Yesu hapo akafufulia kuonyesha kuwa kifo chake kilitosha kweli kulipa hukumu ya dhambi zetu (1Wakorintho15)

Yesu aokoa, lakini anaokoa nani?
Yesu anawaokoa wale wote wanaopokea tuzo lake la wokovu. Yesu anawaokoa wale wote wanaomwamini katika dhabihu yake pekee kama fidia ya dhambi (Yohana 3:16; Matendo 16:31). Huku Yesu kama dhabihu ilikuwa kamilifu na yatosha kulipia dhambi zote za binadamu, Yesu pekee ndiye aweza kuokoa wale pekee wanaoipokea zawadi yake (Yohana 1:12)

Kama sasa unaelewa yamaanisha nini Yesu aokoa, na unataka kuweka imani kwake kama mwokozi wa maisha yako, akikisha kwamba unaelewa na kuamini yafuatayo, na kama hatua ya imani, nena maneno yafuatayo, “Mungu, ninajua mimi ni mwenye dhambi, na ninajua yakwamba kwa sababu ya dhambi zangu ninastahili kutenganishwa milele na Wewe. Hata kama sistahili, asante kwa kunipenda na kutoa dhabihu ya dhambi zangu kupitia kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo. Ninaamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zangu, na ninaamini kwake pekee aniokoe. Kutoka wakati huu sasa na kuendelea, nisaidie niishi maisha kwa ajili yako badala ya dhambi. Nisaidie kuishi maisha yangu yote kwa furaha kwa wokovu wa ajabu ambao umeutoa. Asante Yesu kwa kuniokoa!”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Yamaanisha nini kuwa Yesu aokoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries