settings icon
share icon

Kitabu cha 1 Wafalme

Mwandishi: Kitabu cha 1 Wafalme hakimtaji bayana mtunzi wake. Utamaduni ni kwamba kiliandikwa na Nabii Yeremia.

Tarehe ya Kuandikwa: Kitabu cha 1 Wafalme kina uwezekano kuwa kiliandikwa kati ya 560 na 540 BC

Kusudi la Kuandika: Kitabu hiki ni mfuatano kwa Samweli ya 1 na 2 na kinaanza kwa kufuatilia kupanda kwa Sulemani kwa utawala wa kifalme baada ya kifo cha Daudi. Hadithi inaanza na ufalme ulio na umoja, lakini inaishia katika taifa lililogawanyika katika falme mbili, zinazojulikana kama Yuda na Israeli. Wafalme wa 1 na 2 zimejumuhishwa pamoja katika kitabu kimoja katika Biblia ya Kiebrania.

Mistari muhimu: 1 Wafalme 1:30, "hakika yake nitafanya leo kama vile nilivyokuapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli, nikasema, kwa yakini Sulemani mwanao atamiliki baada yangu, naye ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi badala yangu. "

1 Wafalme 9: 3, "Bwana akamwambia: 'Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote. "

1 Wafalme 12:16, "Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao"

1 Wafalme 12:28, "Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng’ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama hii ndiyo miungu yenu,enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri"

1 Wafalme 17: 1, "Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu. '"

Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha 1 Wafalme kinaanza na Sulemani na kuishia na Elija. Tofauti kati yao inakupa wazo kwa yale yaliyomo kati yao. Sulemani alizaliwa baada ya kashfa ya kasri/hekalu kati ya Daudi na Bathsheba. Kama baba yake, alikuwa na udhaifu kwa wanawake ambayo ungeweza kumuangusha. Sulemani alifanya vizuri mwanzoni, kuomba kupewa hekima na kujenga hekalu kwa Mungu aliyochukua miaka saba. Lakini baadaye alitumia miaka 13 kujijengea kasri lake mwenyewe. Wingi wa wake zake ulimfanya kuabudu sanamu zao, na kumpeleka mbali na Mungu. Baada ya kifo cha Sulemani, Israeli ilitawaliwa na mfululizo wa wafalme, ambao wengi wao walikuwa waovu na waabudu sanamu. Kutokana na haya, taifa lilipotoshwa mbali na Mungu na hata mahubiri ya Elija hayangeweza kuwarejesha kwa Mungu. Miongoni mwa wafalme waovu zaidi ni Ahabu na malkia wake, Yezabeli, ambaye alileta ibada ya Baali kwa kiwango kikubwa katika Israeli. Elija alijaribu kuwarudisha waisraeli kwa ibada ya Yehova, hata kwa luwapa changamoto makuhani walioabudu sanamu ya Baali kwa kutangaza nguvu za Mungu katika mlima wa Karmeli. Bila shaka Mungu alishinda. Hili lilimfanya Malkia Yezebeli akasirike (kusema machache). Yeye aliamuru Elija auwawe hivyo kumfanya Elija kukimbia na kujificha jangwani. Akihuzunika na kuchoka, alisema, "Na nife." Lakini Mungu alituma chakula na faraja kwa nabii na kumuongeleza kwa sauti tulifu ya upole, na katika harakati hizo akaokoa maisha yake kwa ajili ya kazi zaidi.

Ishara: Hekalu lililoko Yerusalemu, ambapo Roho wa Mungu atakaa katika Patakatifu pa Patakatifu, linaashiria waumini katika Kristo ambao Roho Mtakatifu anakaa ndani yao kutoka wakati wa wokovu wetu. Tu kama Waisraeli walipaswa kuziacha sanamu, hivyo pia sisi tunapaswa kuweka mbali chochote ambacho hututenganisha kutoka kwa Mungu. Sisi ni watu wake, hekalu la Mungu aliye hai. 2 Wakorintho 6:16 inatuambia, "Tena pana mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; Kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. "

Eliya nabii alikuwa mtangulizi wa Kristo na Mitume wa Agano Jipya. Mungu alimwezesha Elija kufanya miujiza ili kuthibitisha kwamba kweli alikuwa mtu wa Mungu. Alifufua kutoka kwa wafu mwana wa mjane wa Sarepta, na kumfanya kukiri, "" Sasa najua ya kuwa wewe ni mtu wa Mungu na kwamba neno la Bwana kutoka mdomo mwako ni kweli. " Kwa njia hiyo hiyo, watu wa Mungu ambao walizungumza maneno yake kwa nguvu zake wamedhihirishwa katika Agano Jipya. Si tu kwamba Yesu alifufua Lazaro kutoka kwa wafu, bali pia alimfufua mwana wa mjane wa Nain (Luka 7: 14-15) na binti wa Yairo (Luka 8: 52-56). Mtume Petro alimfufua Dorkasi (Matendo 9:40) na Paulo alimfufua Eutiko (Matendo 20: 9-12).

Vitendo Tekelezi: Kitabu cha 1 Wafalme kina mafunzo mengi kwa Waumini. Tunaona onyo kuhusu marafiki tukuwao nao, na hasa katika suala la uhusiano wa karibu na ndoa. Wafalme wa Israeli ambao, kama Sulemani, walioa wanawake wageni walijitoza wenyewe na watu waliotawala kwa dhambi. Kama waumini katika Kristo, lazima tuwe makini sana kwa wale tunaochagua kama marafiki, washirika wa kibiashara, na wapenzi katika ndoa. "Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema" (1 Wakorintho 15:33).

Uzoefu wa Elija katika jangwa pia unafundisha funzo muhimu. Baada ya ushindi wake wa ajabu juu ya manabii 450 wa Baali kwenye Mlima Karmeli, furaha yake iligeuka kuwa huzuni wakati aliposakwa na Yezebeli na ikambidi kukimbia kuokoa maisha yake. Uzoefu kama huo wa juu ya mlima mara nyingi unafuatiwa na sikitiko na huzuni na kuvunjwa moyo kutakaofuata. Lazima tuwe macho kwa uzoefu wa aina hii katika maisha ya Kikristo. Lakini Mungu wetu ni mwaminifu na kamwe hatatuacha. Sauti tulivu, yenye upole iliyomtia moyo Eliya itatutia moyo.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 1 Wafalme
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries