settings icon
share icon

Kitabu cha 1 Wakorintho

Mwandishi: 1 Wakorintho 1: 1 kinamtambua mwandishi wa kitabu cha 1 Wakorintho kama mtume Paulo.

Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha 1 Wakorintho kiliandikwa katika takriban 55 BK.

Kusudi la Kuandika: Mtume Paulo alianzisha kanisa katika Korintho. Miaka michache baada ya kuondoka kwa kanisa, Mtume Paulo alisikia baadhi ya ripoti za kusumbua kuhusu kanisa la Korintho. Walijawa na kiburi na walitetea usherati. Vipawa vya kiroho vilitumiwa vibaya, na kulikuwa na kutoelewa kuliosambaa kwa mafundisho muhimu ya Kikristo. Mtume Paulo aliandika barua yake ya kwanza kwa Wakorintho katika jaribio la kurejesha kanisa la Korintho kwa msingi wake-Yesu Kristo.

Mistari muhimu: 1 Wakorintho 3: 3: "Kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana ikwa kwenu kuna husuda na fitina, Je, si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? "

1 Wakorintho 6: 19-20: "Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. "

1 Wakorintho 10:31: "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu."

1 Wakorintho 12: 7: "Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana."

1 Wakorintho 13: 4-7: "Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. "

1 Wakorintho 15: 3-4, "Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko, na ya kuwa alizikwa, na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko. "

Muhtasari kwa kifupi: kanisa la Korintho lilikumbwa na mgawanyiko. Waumini wa kule Korintho walikuwa wanajigawanya katika makundi yaaminifu kwa baadhi ya viongozi wa kiroho (1 Wakorintho 1:12; 3: 1-6). Paulo aliwahimiza waumini wa Korintho kuwa na umoja kwa sababu ya kumwabudu Kristo (1 Wakorintho 3: 21-23). Wengi katika kanisa walikuwa kimsingi wakiidhinisha mahusiano mabaya (1 Wakorintho 5: 1-2). Paulo aliwaamuru kufukuza mtu mbaya kutoka kwa kanisa (1 Wakorintho 5:13). Waumini Wakorintho walikuwa wakipelekana mahakamani (1 Wakorintho 6: 1-2). Paulo aliwafundisha Wakorintho kwamba itakuwa bora kupuuzwa kuliko kuharibu ushuhuda wao wa kikristo (1 Wakorintho 6: 3-8).

Paulo alitoa maelekezo kwa kanisa la Korintho juu ya ndoa na useja ( sura 7), vilivyotolewa sadaka kwa sanamu (sura ya 8 na 10), uhuru wa Kikristo (Sura ya 9), jinsi wanawake wanapaswa kuvaa (1 Wakorintho 11: 1-16), Meza ya Bwana (1 Wakorintho 11: 17-34), zawadi ya kiroho (sura 12-14), na ufufuo (sura ya 15). Paulo alipanga kitabu cha 1 Wakorinto kwa kujibu maswali amabayo waumini Wakorintho walikuwa wamemwuliza na kwa kukabiliana na mwenendo mbaya na imani potofu waliyokuwa wamekubalia.

Mashirikisho: Katika sura ya 10 ya kitabu cha 1 Wakorinto, Paulo anatumia hadithi ya kuzunguka kwa waisraeli jangwani ili kuonyesha waumini Wakorintho upumbavu wa matumizi mabaya ya uhuru na hatari ya kujiamini kupita kiasi. Paulo alikuwa amewaonya Wakorintho kuhusu ukosefu wao wa nidhamu (1 Wakorintho 9: 24-27). Anaendelea kuelezea Waisraeli ambao, licha ya kuona ile miujiza ya Mungu na malezi kwao- kutawanywa kwa Bahari ya Shamu, muujiza wa utoaji wa mana kutoka mbinguni na maji kutoka kwenye mwamba-walitumia vibaya uhuru wao, waliasi dhidi ya Mungu, na wakaanguka katika usherati na kuabudu sanamu. Paulo anahimiza kanisa la Korintho kutoa mfano wa Waisraeli na kuepuka na tamaa na usherati (mst 6-8.) Na kuweka Kristo kwa majaribu na kulalamika (mst. 9-10). Angalia Hesabu 11: 4, 34, 25: 1-9; Kutoka 16: 2, 17: 2, 7.

Vitendo Tekelezi: Matatizo mengi na maswali ambayo kanisa la Korintho lilikuwa linashughulikia bado yapo katika kanisa siku hizi. Makanisa siku hizi bado yanapambana na mgawanyiko, na usherati, na pamoja na matumizi ya vipawa vya kiroho. kitabu cha 1 Wakorinto vizuri sana kingeweza kuandikwa kwa kanisa siku hizi na tungeweza kufanya vizuri kutia maanani maonyo ya Paulo na kuyatekeleza kwetu wenyewe. Licha ya laana zote na marekebisho, 1 Wakorintho huleta mtazamo wetu nyuma ambapo unapaswa kuwa-kwa Kristo. Upendo halisi wa Kikristo ni jibu kwa matatizo mengi (sura ya 13). Uelewa sahihi juu ya ufufuo wa Kristo, kama ilivyofunuliwa katika sura ya 15, na hivyo kuelewa halisi kwa ufufuo wetu wenyewe, ni tiba kwa kinachotugawanya na kutushinda.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 1 Wakorintho
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries