settings icon
share icon

Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati

Mwandishi: Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati hakimtaji bayana mtunzi wake. Utamaduni ni kwamba Mambo ya Nyakati ya 1 na 2 ziliandikwa na Ezra.

Tarehe ya Kuandikwa: Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati kina uwezekano kiliandikwa kati ya 450 na 425 BC

Kusudi la Kuandika: Vitabu vya Mambo ya Nyakati ya 1 na 2 vinashughulikia zaidi ujumbe sawa kama Samweli ya 1 na 2 na Wafalme ya 1 na 2.Vitabu vya Mambo ya Nyakati ya 1 na 2 vinazingatia zaidi juu ya suala la kikuhani kwa kipindi cha muda. Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati kimsingi ni tathmini ya historia ya dini ya taifa .

Mistari muhimu: 2 Mambo ya Nyakati 2: 1, "Basi Sulemani alikusudia kujenga nyumba kwa Jina la Bwana, na kuujengea ufalme wake nyumba."

2 Mambo ya Nyakati 29: 1-3, "Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka ishirini na kenda; na jina la mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Daudi babaye. Yeye katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, katika mwezi wa kwanza, aliifungua milango ya nyumba ya Bwana, akaitengeneza. "

2 Mambo ya Nyakati 36:14, "Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakaza katika Yerusalemu."

2 Mambo ya Nyakati 36:23, "Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi: 'Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee. "

Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati Kinatoa historia ya ufalme wa kusini ya Yuda, kutoka utawala wa Sulemani hadi hitimisho la uhamisho wa Babeli. Mwanguko wa Yuda ni wa kuudhi, lakini msisitizo unatolewa kwa waleta mabadiliko wa kiroho ambao kwa bidii wanajitahidi kuwarejesha watu kwa Mungu. Machache yamesemwa kuhusu wafalme wabaya au ya kushindwa kwa wafalme wazuri; wema tu ndio umesisitizwa. Kwa kuwa 2 Mambo ya Nyakati inachukua mtazamo wa kikuhani, ufalme wa kaskazini wa Israeli umetajwa kidogo sana kwa sababu ya ibada yake ya uongo na kukataa kukiri Hekalu la Yerusalemu. 2 Mambo ya Nyakati inamalizia kwa uharibifu wa mwisho wa Yerusalemu na hekalu.

Ishara: Kwa marejeleo ya wafalme na mahekalu katika Agano la Kale, tunaona katika yao urejeo wa Mfalme wa kweli wa Wafalme, Yesu Kristo-na wa Roho Mtakatifu wa hekalu la –watu wake. Hata ubora wa wafalme wa Israeli ulikuwa na makosa ya watu wote wenye dhambi na waliongoza watu isiyo. Lakini wakati Mfalme wa Wafalme anakuja kuishi na kutawala juu ya nchi katika milenia, atajiimarisha mwenyewe juu ya kiti enzi cha dunia yote kama mrithi halali wa Daudi. Hapo tu ndipo tutakuwa na Mfalme kamili atakayetawala katika haki na utakatifu, jambo bora ambalo wafalme wa Israeli wangeota kuhusu.

Vile vile, hekalu kubwa lililojengwa na Sulemani halikuundwa kudumu milele. Miaka 150 baadaye,liliitaji kukarabatiwa kutokana na kuoza na kuchafuliwa na vizazi vijavyo ambavyo vilianza kuabudu sanamu (2 Wafalme 12). Lakini hekalu la Roho Mtakatifu-wale walio wa Kristo-wataishi milele. Sisi tulio wa Yesu ndio hekalu hilo, ambao tuliundwa si kwa mikono bali kwa mapenzi ya Mungu (Yohana 1: 12-13). Roho ambaye anaishi ndani yetu kamwe ataondoka kutoka kwetu na atatuwazilisha salama katika mikono ya Mungu siku moja (Waefeso 1:13; 4:30). Hakuna hekalu la kidunia lina ahadi hiyo.

Vitendo Tekelezi: Msomaji wa Mambo ya Nyakati amealikwa kutathmini kila kizazi kutoka zamani na kutambua ni kwa nini kila kizazi kilibarikiwa kwa utiifu wao au kuadhibiwa kwa uovu wao. Lakini pia tunapaswa kulinganisha hatma ya vizazi hivi na yetu wenyewe, kwa ushirika na binafsi. Ikiwa sisi au taifa letu au kanisa letu linakabiliwa na ugumu, ni kwa faida yetu kulinganisha imani yetu na jinsi tutendavyo juu ya imani hizo na uzoefu wa Israeli chini ya wafalme mbalimbali. Mungu anachukia dhambi na hatazivumilia. Lakini ikiwa rekodi zitatufundisha kitu chochote, ni kwamba Mungu anataka kusamehe na kuponya wale ambao kwa unyenyekevu wataomba na kutubu (1 Yohana 1: 9).

Ikiwa ungekuwa na chochote ulitaka kutoka kwa Mungu, ungeomba nini? Je, ni mali ya ajabu? Je, ni afya bora kwako na kwa uwapendao? Je, ni uwezo juu ya uzima na kifo? Inashangaza sana kufikiri juu yake, sivyo? Lakini ajabu zaidi ni kwamba Mungu alimpa Sulemani ombi hilo na hakuchagua chochote kati ya haya. Kile alichoomba ni hekima na maarifa ili akamilishe kazi ambayo Mungu alikuwa amempa na kuifanya vizuri. Funzo kwetu ni kwamba Mungu amempa kila mmoja wetu wajibu wa kutimiza na baraka kubwa zaidi tunaweza kutafuta kutoka kwa Mungu ni uwezo wa kufanya mapenzi yake kwa maisha yetu. Kwa hivyo, tunahitaji "hekima inayotoka juu" (Yakobo 3:17) ili kupambanua mapenzi yake, vile vile kuelewa na ujuzi wa ndani wake ili kututia moyo kufanya mapenzi ya Kristo katika matenda na tabia (James 3:13) .

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 2 Mambo ya Nyakati
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries