settings icon
share icon

Kitabu cha 2 Wafalme

Mwandishi: Kitabu cha 2 Wafalme hakimtaji mtunzi wake. Utamaduni ni kwamba nabii Yeremia ndiye alikuwa mwandishi wa Wafalme ya 1 na 2.

Tarehe ya Kuandikwa: Kitabu cha 2 Wafalme, pamoja na 1 Wafalme, kuna uwezekano kiliandikwa kati ya 560 na 540 BC

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha 2 Wafalme ni mfuatano wa Kitabu cha 1 Wafalme. Kinaendeleza hadithi ya wafalme juu ya Ufalme uliotawanyika (Israeli na Yuda.) Kitabu cha 2 Wafalme kinamalizia kutawaliwa kwa mwisho na kufukuzwa kwa watu wa Israeli na Yuda hadi Ashuru na Babeli, mtawalia.

Mistari muhimu: 2 Wafalme 17: 7-8. "Yalitukia hayo kwa sababu wana wa Israeli walikuwa wametenda dhambi juu ya Bwana, Mungu wao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri watoke chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri, Wakawaacha miungu mingine. Wakaziendea sheria za mataifa, ambao Bwana aliwafukuza mbele ya wana wa Israeli, na sheria za wafalme wa Israeli walizozifanya. "

2 Wafalme 22: 1a-2: "Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala, akatawala miaka thelathini na mmoja katika Yerusalemu; Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, akaenda katika njia yote ya Daudi baba yake, wala hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto. "

2 Wafalme 24: 2: "Naye Bwana akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neon la Bwana alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii. "

2 Wafalme 8:19: "Walakini BWANA hakupenda kuiharibu Yuda, kwa ajili ya Daudi mtumishi wake, kama alivyomwahidia akasema, kuwa atampa taa, yeye na wazao wake siku zote. "

Muhtasari kwa kifupi: Wafalme ya pili inaonyesha anguko la ufalme uliogawanyika. Manabii wanaendelea kuwaonya watu kwamba hukumu ya Mungu imekaribia, lakini hawawezi kutubu. Ufalme wa Israeli unatawaliwa mfululizo na wafalme waovu, na hata ingawa wachache wa wafalme wa Yuda ni wazuri, wengi wao wanawapotosha watu mbali na ibada ya Yehova. Hawa watawala wachache wazuri, pamoja na Elisha na manabii wengine, hawawezi kuzuia kuanguka kwa taifa. Ufalme wa kaskazini wa Israeli hatimaye unaharibiwa na Waashuru, na takribani miaka 136 baadaye ufalme wa kusini ya Yuda unaharibiwa na Wababeli.

Kuna mada tatu maarufu sasa katika Kitabu cha 2 Wafalme. Kwanza, Bwana atawahukumu watu wake wakati wanaasi na kumwacha. Kutokuwa waaminifu kwa Waisraeli kulidhihirishwa katika ibada mbaya ya sanamu na wafalme na ilisababisha Mungu kutekeleza ghadhabu yake ya haki dhidi ya uasi wao. Pili, neno la manabii wa kweli wa Mungu daima huja kutimia. Kwa sababu Bwana daima hutimiza neno lake, hivyo pia maneno ya manabii wake daima ni kweli . Tatu, Bwana ni mwaminifu. Alikumbuka ahadi yake kwa Daudi (2 Samweli 7: 10-13), na licha ya uasi wa watu na wafalme waovu waliowatawala, Bwana hakuimaliza familia ya Daudi.

Ishara: Yesu anatumia hadithi ya mjane wa Sarepta kutoka kwa 1 Wafalme na Naamani katika 2 Wafalme kuelezea ukweli mkubwa wa huruma ya Mungu kwa wale ambao Wayahudi waliona hawastahili neema ya Mungu -maskini, wadhaifu, waliodhulumiwa, watoza ushuru, wasamaria , watu wa mataifa. Kwa kuangazia mifano ya mjane maskini na mwenye ukoma, Yesu alijionyesha mwenyewe kuwa Mganga mkuu anayeponya na kuhudumu kwa walio katika haja kubwa ya neema tukufu ya Mungu. Ukweli huu ndio uliokuwa msingi wa siri ya mwili wa Kristo, kanisa lake, ambalo litatolewa kutoka kwa ngazi zote za jamii, wanaume na wanawake, matajiri na maskini, Wayahudi na Mataifa (Waefeso 3: 1-6).

Miujiza mingi ya Elisha iliashiria ile ya Yesu Mwenyewe. Elisha alimfufua mwana wa mwanamke Mshunami (2 Wafalme 4: 34-35), akamponya Naamani ukoma (2 Wafalme 5: 1-19), na kuzidisha mikate ili kulisha watu mia na mingine ikabakia (2 Wafalme 4:42 -44).

Vitendo Tekelezi: Mungu anachukia dhambi na hataziruhusu kudumu milele. Ikiwa sisi ni wake, tunaweza kutarajia adabu yake wakati tunamwasi. Baba mwenye upendo anawarekebisha watoto wake kwa manufaa yao na kuthibitisha kwamba kwa kweli ni wake. Wakati mwingine Mungu anaweza kutumia makafiri ili kurekebisha watu wake, na anatupa onyo kabla ya kutoa hukumu. Kama Wakristo, tuna Neno lake kutuongoza na kutuonya wakati tunapotoka njia yake. Kama manabii wa zamani, Neno lake ni la kuaminika na daima linasema ukweli. Uaminifu wa Mungu kwa watu wake kamwe hautashindwa, hata wakati sisi tunashindwa kuwa waaminifu.

Hadithi za mjane na mwenye ukoma ni mifano kwetu kuhusu Mwili wa Kristo. Tu kama Elisha alikuwa na huruma kwa haya kutoka kwa ngazi ya chini katika jamii, tunapaswa kuwakaribisha wote ambao ni wa Kristo katika makanisa yetu. Mungu hana "upendeleo" (Matendo 10:34) nasi pia hatupaswi kuwa na upendeleo.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha 2 Wafalme
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries