settings icon
share icon

Kitabu cha Ufunuo

Mwandishi: Ufunuo 1: 1,4,9 na 22: 8 hasa inatambua mwandishi wa kitabu cha Ufunuo kama mtume Yohana.

Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha Ufunuo huenda kiliandikwa kati ya 90 na 95 BK.

Kusudi la Kuandika: Ufunuo wa Yesu Kristo ulitolewa kwa Yohana na Mungu "kuonyesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee hivi karibuni." Kitabu hiki kimejazwa na siri kuhusu mambo yajayo. Ni onyo la mwisho kwamba dunia hakika itaisha na hukumu itakuwa hakika. Kinatupa tazamo la kuona mara moja kidogo sana la mbinguni na utukufu wote unaowangojea wanaotunza mavazi(mioyo safi) yao meupe. Ufunuo unatuchukua kupitia kwa matatizo pamoja na majonzi yake yote, na moto wa mwisho ambao makafiri wote watakabiliwa nao milele. Kitabu kinarudia kuanguka kwa Shetani na hukumu/maangamizi ambayo yeye na malaika wake wamewekewa. Tumeonyeshwa majukumu ya viumbe vyote na malaika wa mbinguni na ahadi za watakatifu ambao wataishi milele na Yesu katika Yerusalemu Mpya. Kama Yohana, ni vigumu kupata maneno ya kuelezea tunayosoma katika kitabu cha Ufunuo.

Mistari muhimu: Ufunuo 1:19, "Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo."

Ufunuo 13: 16-17, "Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. "

Ufunuo 19:11, "Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu wa Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita."

Ufunuo 20:11 "Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana."

Ufunuo 21: 1, "Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena."

Muhtasari kwa kifupi: Ufunuo ni tele katika maelezo ya rangi ya maono ambayo yanatutangazia siku za mwisho kabla ya kurudi kwa Kristo na kuikaribisha mbingu mpya na dunia mpya. Ufunuo unaanza na barua kwa makanisa saba ya Asia Ndogo, kisha unaendelea kufumbua mfululizo wa uharibifu unaomwagwa juu ya nchi; alama ya mnyama, "666"; hali ya vita vya Armageddoni, kufungwa kwa Shetani, utawala wa Bwana; Hukumu kuu ya Kiti Kikubwa cha Enzi; na asili ya mji wa milele wa Mungu. Unabii kuhusu Yesu Kristo unatimizwa na wito kwetu wa kuhitimisha kwa Ubwana wake unatuhakikishia kwamba Yeye atarudi hivi karibuni.

Mashirikisho: kitabu cha Ufunuo ni kilele cha unabii kuhusu nyakati za mwisho, kuanzia Agano la Kale. Maelezo ya mpinga Kristo aliyetajwa katika Danieli 9:27 yamekuzwa kikamilifu katika sura ya 13 ya Ufunuo. Nje ya Ufunuo, mifano ya matangazo/maelezo ya kutabiri hali ya maafa makubwa katika Biblia ni Danieli sura 7-12, Isaya sura 24-27, Ezekieli sura 37-41, na Zekaria sura 9-12. Unabii huu wote unakuja pamoja katika kitabu cha Ufunuo.

Vitendo Tekelezi: Je, umemkubali Kristo kama mwokozi wako? Kama ni hivyo, huna lolote la kuogopa kutokana na hukumu ya Mungu ya ulimwengu kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Ufunuo. Mwamuzi yu katika upande wetu. Kabla ya hukumu ya mwisho kuanza, lazima tuwashuhudie marafiki na majirani kuhusu toleo la Mungu la uzima wa milele katika Kristo. Matukio katika kitabu hiki ni ya kweli. Lazima tuishi maisha yetu kama tunavyoamini ili wengine watambue furaha yetu kuhusu siku zetu za mbeleni na watake kujiunga nasi katika mji huo mpya na tukufu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Ufunuo
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries