settings icon
share icon
Swali

Ninawesaje kuwa Mkristo?

Jibu


Hatua ya kwanza ya kuwa Mkristo ni kuelewa maana ya neno “Mkristo” lamaanisha nini. Mwanzo wa neno “Mkristo” ni katika mji wa Antiokia katika karne ya kwanza baada ya Yesu kuzaliwa (A.D) (angalia Matendo ya Mitume 11:26). Kuna uwezekano kuwa, kwanza neno “Mkristo” lilinuiwa kuwa la kutukana. Hilo neno kimsingi laamanisha “Kristo mdogo.” Ingawa katika karne nyingi, wamwaminio Kristo wamelichukua neno “Mkristo” na kulitumia kwa kujitambulisha wao wenyewe kama wafuasi wa Kristo. Fasili rahisi ya Mkristo ni mtu ambaye anaomfuata Kristo.

Ni kwa nini niwe Mkristo?
Yesu Kristo alisema ya kwamba “hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Marko 10:45). Basi swali lajibuka ni- Ni kwa nini tuliitaji kufidiwa? Dhana ya fidia ni malipo ambayo ni lazima yafanyike katika kumwachilia mtu. Dhana ya fidia mara nyingi yatumika katika matukio ya utekaji nyara, wakati mtu ametekwa nyara na kuzuiliwa mateka hadi fidia ilipwe kwa huyo mtu aachiliwe.

Yesu alilipa fidia yetu ili atuweke huru kutoka utumwa! Utumwa wa nini? Utumwa wa dhambi na madhara yake, kifo cha kimwili ambacho kinafuatwa na ule utengano wa milele na Mungu. Ni kwa nini Yesu aliitajika kulipa fidia hii? Ni kwa sababu wote tumeadhirika na dhambi (Warumi 3:23), na kwa hiyo hukumu yatufaa kutoka kwa Mungu (Warumi 6:23). Yesu aliilipaje fidia yetu? Kwa kufa msalabani ili alipe hukumu yetu ya dhambi (1Wakorintho 15:3; 2Wakorintho 5:21). Kifo cha Yesu kingewezaje kulipa deni ya dhambi zetu kikamilifu? Yesu alikuwa Mungu katika mwili wa binadamu, Mungu alikuja duniani ili awe pamoja nasi ili ajitambulishe nasi na afe kwa ajili ya dhambi zetu. (Yohana 1:1,14). Kama Mungu, kifo cha Yesu dhamani yake ni ya milele, ambayo yatosha kulipa deni ya dhambi ya dunia yote (1Yohana 2:2). Kufufuka kwa Yesu baada ya kifo chake kulionyesha kuwa mauti yake ni dhabihu ya kutosha, ya kwamba hakika aliyashinda mauti na dhambi.

Ninawezaje sasa kuwa Mkristo?
Hii ni sehemu muhimu sana. Kwa sababu ya upendo wake kwetu, Mungu ameendelea kufanya rahisi njia ya kuwa Mkristo. Chenye unastahili kufanya ni kumpokea Yesu kama Mwokozi wa maisha yako, kukubali kikamilifu kuwa kifo chake ni dhabihu ya dhambi zako (Yohana 3:16), kumtumainia kikamilifu yeye mwenyewe kama mwokozi wako (Yohana 14:6; Matendo Ya Mitume 4:12). Kuwa Mkristo si hali ya kuwa na tamaduni, kwenda kanisani, au kufanya mambo fulani huku ukijizuia kutoka kwa mengine. Kuwa Mkristo ni hile hali ya kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo, kupitia kwa imani, ndicho kitu kinachomfanya mtu kuwa Mkristo.

Je! Uko tayari kuwa Mkristo?
Kama uko tayari kuwa Mkristo kwa kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako, chenye unastahili kufanya ni kuamini. Je! Unaelewa na kuamini kuwa umefanya dhambi na wastahili hukumu kutoka kwa Mungu? Waelewa na kuamini kwamba Yesu aliibeba adhabu yako yeye mwenyewe akafa kwa ajili yako? Je! Waelewa na kuamini ya kuwa kifo chake ni dhabihu yatosha kufidia dhambi zako? Kama jibu lako kwa maswali haya ni, Naam, basi kwa ufupi iweke tumaini yako kwa Yesu kama mwokozi wako. Mpokee, kwa imani, na kumwamini kwa hali yote yeye pekee. Hayo yote ndio yanayohitajika kuwa Mkristo.

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawesaje kuwa Mkristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries