settings icon
share icon
Swali

Je! Mfumo wa dini ni wa kibibilia?

Jibu


Mfumo wa dini ni mpangilio wa kiteolojia ambao uko na misingi miwili tofauti. 1) Kwa patano la fafanuo/fasiri ya maandiko, hasa unabii wa kibibilia. 2) Tofauti kati ya Israeli na kanisa katika mpango wa Mungu.

Mfumo wa dini washikilia kuwa kanuni yao ya fasiri ya Bibilia ni ile ya fasiri ya neno kwa neno ambayo yamaanisha kulipa kila neno maana ambayo litakuwa nalo kila litumikapo. Alama, tamathali ya usemi na kila aina zote simefafanuliwa kiuuwazi katika mtindo huu, na hii haitilafiani na ile tafsiri ya neno kwa neno. Kila alama na tamathali ya usemi ziko na fasiri ya neno kwa neno maana ikiwa imefichika.

Kuna hasa sababu tatu ni kwa nini huu ndio mtazamo mzuri wa kuangalia maandiko. Kwanza, kifalsafa, lengo la lugha yenyewe yaonekana kuhitaji kufafanuliwa neno kwa neno. Lugha ilipeanwa na Mungu kwa lengo la kuwa na uwezo wa kuwasiliana na mwanadamu. Sababu ya pili ni ya kibibilia. Kila unabii kuhusu Yesu Kristo katika Agano La Kale ulitimia. Kuzaliwa kwa Yesu, huduma ya Yesu, kifo cha Yesu, na kufufuka kwa Yesu vyote vilitendeka vile ilikuwa imetabiriwa katika Agano La kale. Hakuna hata neno moja ambalo halijatimizwa la unabii huu katika Agano Jipya. Hii uhojiana kwa kuegemea fasiri ya neno kwa neno. Kama fasiri ya neno kwa neno haitumiki katika kuchunguza maandiko, kwa hivyo hakuna kiwango kamili kinachotumika kuelewa Bibilia. Kila mtu ataweza kufasiri bibilia jinsi ameona yafaa. Fasiri ya kibibilia utaibua swali kama, “huu ujumbe wasema nini kwangu…” badala ya “Bibilia inasema…” cha kusikitisha hii ndio hali katika wingi wa fasiri ya bibilia hii leo.

Teolojia ya mfumo wa dini wafunza kuwa kuna aina mbili tofauti ya watu wa Mungu: Israeli na kanisa. Mfumo wa dini waamini kuwa wokovu umekuwa kila wakati kwa imani-katika Mungu katika Agano La Kale na hasa katika Mungu mwana katika Agano Jipya. Mfumo wa dini washikilia kuwa kanisa halijachukua nafasi ya Israeli katika mpango wa Mungu na ahadi za Agano La Kale hazichahamishiwa kanisa. Wanaamini kuwa ahadi za Mungu alizowaahidi Waisraeli (ahadi) katika Agano La Kale hatimaye hizo zitatimizwa kwa kipindi cha miaka 1000 amboyo imezungumziwa katika Ufunuo Wa Yohana mlango wa 20. Mfumo wa dini waamini kwamba vile Mungu ako katika kizazi hiki akilitazama kanisa, pai siku za husonni atawaangazia Waistraeli (Warumi 9-11).

Kwa kutumia mpangilio huu kama msingi, anayeamini mfumo wa dini anaielewa bibilia kuwa imepangwa katika mifumo saba: kutojua (Mwanzo 1:1-3:7), ufahamu (Mwanzo 3:8-8:22), serikali ya mwanadamu (Mwanzo 9:1-11:32), ahadi (Mwanzo 12:1-Kutoka 19:25), sheria (Kutoka 20:1-Matendo Ya Mitume 2:4), neema (Matendo Ya Mitume 2:4-Ufunuo Wa Yohana 20:3), ufalme wa kipindi cha miaka elfu moja (Ufunuo Wa Yoha 20:4-6). Pia, hii mifumo ya dini si njia za wokovu, bali ni namna ambayo Mungu anasimuliana na mwanadamu. Mfumo wa dini kama mpangilio, umetokea kwa fasiri ya miaka elfu moja kabla Yesu arudi mara ya pili na fasiri ya taabu kabla ya unyakuzi. Kwa mkhutasari, mfumo wa dini ni mpangilio wa teolojia ambao wasizitiza fasiri ya neno kwa neno ya unabii wa bibilia, watambua tafauti kati ya Israeli na kanisa, na kupanga bibilia kwa vikundi vya mifumo inayowakilisha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mfumo wa dini ni wa kibibilia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries