settings icon
share icon
Swali

Je, Mkristo anafaa kusikiliza muziki wa kidunia?

Jibu


Wakristo wengi wanapambana na swali hili. Wanamuziki wengi wa miziki ya kidunia ni wenye vipaji. Muziki wa kidunia unaweza kuwa wa kuburudisha sana. Kuna nyimbo nyingi za muziki wa kidunia ambazo zina sauti za kuvutia,utambuzi wa kimawazo, na ujumbe bayana. Katika kuamua ikiwa au la utasikiliza muziki wa kidunia, kuna mambo matatu ya msingi ya kuzingatia: 1) Madhumuni ya muziki, 2) mtindo wa muziki, na 3) maudhui ya maneno ya wimbo.

1) Madhumuni ya muziki.Je, muziki umeundwa tu kwa ajili ya ibada, au Mungu alitazamia pia muziki kuwa wa kupembeleza na / au wa kuburudisha? Mwanamuziki maarufu katika Biblia, Mfalme Daudi, kimsingi alitumia muziki kwa lengo la kuabudu Mungu (tazama Zaburi 4: 1, 6: 1, 54, 55; 61: 1; 67: 1; 76: 1). Hata hivyo, wakati Mfalme Sauli alikuwa anasumbuliwa na roho mbaya,alimwita Daudi ili apige kinubi kwa mnajili wa kumpembeleza (1 Samweli 16: 14-23). Waisraeli pia walitumia vyombo vya muziki kuonya kuhusu hatari (Nehemia 4:20) na kwa kuwashangaza maadui zao (Waamuzi 7: 16-22). Katika Agano Jipya, mtume Paulo anawaelekeza Wakristo kutiana moyo kwa muziki: "mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu" (Waefeso 5:19). Hivyo, wakati madhumuni ya msingi ya muziki yanaonekana kuwa kuabudu , Biblia dhahiri inaruhusu matumizi mengine ya muziki.

2) mtindo wa muziki. Cha kusikitisha, suala la mitindo ya muziki inaweza kuwa ya kugawanya sana miongoni mwa Wakristo. Kuna Wakristo ambao wanakataa katakata matumizi ya vyombo vya muziki . Kuna Wakristo ambao tu wanataka kuimba "nyimbo za imani za kale " . Kuna Wakristo ambao wanataka muziki wa kisasa wa pigo lisilo na mkazo. Kuna Wakristo ambao wanadai kuabudu bora katika "mazingira ya tamasha aina ya mwamba " . Badala ya kutambua tofauti hizi kama mapendeleo ya kibinafsi na tofauti za kitamaduni, baadhi ya Wakristo hutangaza mitindo ya mapendeleo yao ya muziki kuwa tu ya pekee " ambayo ni ya kibiblia" na kutangaza aina nyingine zote za muziki kuwa hazipendezi ,mbaya, au hata za kishetani.

Hakuna mahali ambapo Biblia inalaani aina yoyote ile ya muziki.Hakuna mahali ambapo Biblia inatangaza chombo chochote cha muziki kuwa mbaya. Biblia inataja aina mbalimbali ya vyombo vya kamba na vyombo vichezwao hewani. Wakati Biblia haitaji hasa ngoma, inataja vyombo vingine vya kugonganishwa. (Zaburi 68:25; Ezra 3:10). Karibu aina zote za muziki wa kisasa ni tofauti na / au mchanganyiko wa aina moja ya vyombo vya muziki,vinavyochezwa kwa kasi tofauti au kwa msisitizo wa juu. Hakuna msingi wa kibiblia kutangaza aina yoyote ile ya muziki kuwa mbaya au nje ya mapenzi ya Mungu.

3) maudhui ya maneno ya wimbo.Kwa vile sio madhumuni ya muziki wala mtindo wa muziki huamua kama Mkristo anapaswa kusikiliza muziki wa kidunia, maudhui ya maneno ya wimbo lazima yazingatiwe. Wakati hasa haizungumuzii kuhusu muziki, Wafilipi 4: 8 ni mwongozo bora kwa maneno ya kimuziki ya wimbo: "Hatimaye, ndugu zangu,kilicho kweli, kilicho chema, kilicho cha haki, kilicho halisi, kinachopendeza, kinachovutia – ikiwa chochote ni bora au tukufu – fikiria kuhusu vitu hivyo. "Kama tutakuwa tukifikiria kuhusu vitu hivyo, hakika hayo ni mambo tunapaswa kukaribisha katika akili zetu kwa njia ya muziki na maneno ya wimbo. Je,maneno ya wimbo katika wimbo wa kidunia yanaweza kuwa kweli,mema, ya haki, yanayopendeza, yanayovutia, bora, na tukufu? Kama ni hivyo, basi hakuna kitu kibaya kwa mkristo kusikiliza wimbo wa kidunia wenye asili kama hiyo.

Hata hivyo, miziki mingi ya kidunia haifikii kiwango cha Wafilipi 4: 8. muziki wa kidunia mara nyingi hukuza usherati na vurugu na kwa wakati huo kudunisha uhalisi na uadilifu. Kama wimbo unatukuza chenye kinampinga Mungu, Mkristo hapaswi kuisikiliza. Hata hivyo, kuna nyimbo nyingi za kidunia zenye hazimtaji Mungu ambazo bado huzingatia maadili ya kimungu kama vile uaminifu, usafi, na uadilifu. Kama wimbo wa mapenzi utakuza heshima ya ndoa na / au usafi wa upendo wa kweli-hata kama haumtaji Mungu au Biblia-bado unaweza kusikilizwa na kufurahiwa.

Chochote mtu anaruhusu kuchukua mawazo yake kwa muda mfupi au baadaye kitaamua hotuba yake na matendo yake. Hii ni Nguzo ya iliyo katika Wafilipi 4: 8 na Wakolosai 3: 2, 5:ikijenga sambuli ya mawazo mema. 2 Wakorintho 10: 5 inasema tunapaswa "tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka,kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo." Maandiko haya hutoa picha ya wazi ya aina ya muziki hatupaswi kusikiliza.

Ni wazi, aina bora ya muziki ni ile ambayo inamsifu na kumtukuza Mungu. Wanamuziki wakristo wenye vipaji hufanya kazi karibu katika kila aina ya muziki, kuanzia muziki dhati hadi kwa dansi ya kurukaruka,nyimbo zinazoimbwa kwa haraka, na muziki maarufu wa visiwa vya West Indies. Hakuna kitu kibaya asili na aina yoyote ile ya muziki.Maneno ya wimbo ndiyo huamua ikiwa wimbo " umekubaliwa" kwa Mkristo kusikiliza. Iwapo chochote kitakuongoza kufikiri kuhusu au kujihusisha katika kitu ambacho hakimtukuzi Mungu, kinapaswa kuepukwa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mkristo anafaa kusikiliza muziki wa kidunia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries