settings icon
share icon
Swali

Bibili inasema nini kuhusu ubaguzi wa rangi,kuchochea wengine na kutenga wengine kando?

Jibu


Kitu cha kwanza cha kuelewa katika uchambuzi huu ni kwamba kuna kizazi kimoja tu- kizazi cha mwanadamu. Wayunani, Waafrika, Waarabu, Wahindi, na Wayahudi si vizazi tofauti. Bali ni kabila mbalimbali za kizazi kimoja cha mwanadamu. Wanadamu wote wako na tabia sawa (bila tofauti yoyote hata ndogo ya uumbaji). Cha muimu zaidi ni, wanadamu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1: 26-27). Mungu aliupenda ilimwengu na akamtuma mwanawe Yesu Kristo kwetu ili afe kwa ajili yetu (Yohana 3:16). “Ulimengu” kawaida wajumulisha kabila zote.

Mungu haonyeshi ubaguzi au upendeleo (Kumbukumbu La Torati 10:17; Matendo Ya Mitume 10:34; Warumi 2: 11; Waefeso 6:9), vilevile nasi. Yakobo 2:4 yawaelezea wale wote wanaobagua kama “waamuzi wenye mawazo mabovu.” Badala ya hivyo, tunastahili kupenda majirani wetu vile tunavyojipenda (Yakobo 2:8). Katika Agano La Kale, Mungu aliwaganya wanadamu katika “vizazi” viwili: Wayahudi na watu wa mataifa. Lengo la Mungu kwa Wayahudi lilikuwa wawe ufalme wa makuani, wahudumu kwa mataifa. Badala ya hiyo, katika sehemu nyingi Wayahudi wakawa na kiburi kwa cheo chao na wakawadharau watu wa mataifa. Yesu Kristo anaweka kikomo kwa mambo haya, akauaribu ule ukuta wa uadui (Waefeso 2:14). Aina zote za ubaguzi wa rangi, uchochezi na kutenga wenginge ni chukizo kwa kazi ya Kristo msalabani.

Yesu anatuamuru tuwapende wengine jinsi tunavyojipenda (Yohana 13:34). Kama Mungu si mpaguzi na anatupenda bila upaguzi, basi tunastahili kuwapenda wengine na upendo huo wa hali ya juu. Yesu afundisha katika Mathayo 25 kwamba chochote tufanyacho kwa hao ndugu wetu wadogo, twamfanyia Mungu. Tukimchukulia mtu kwa ubaguzi twamfanyia vipaya mtu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu; twamchukiza mtu ambaye Mungu anampenda na ambaye Yesu alimfia.

Ubaguzi wa rangi, wa njia mbalimbali viwango tofauti, umekua kama pigo kwa wanadamu kwa kipindi cha miaka elfu na elfu. Kaka na dada wa kabila zote hii haistahili kuwa hali. Waadhiriwa wa ubaguzi wa rangi, uchochezi au kutengwa wastahili kusamehe. Waefeso 4:32 yasema, “Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasemehe ninyi.” Wabaguzi wa rangi huenda hawastahili msamaha wako, lakini tulistahili msamaha wa Mungu sana. Wale wanaofanya kubagua, kuchochea, au kutenga wengine wastahili kutubu. “Bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.” Ni ombi langu kuwa Wagalatia 3:28 itambulike kikamilifu, “Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.”

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibili inasema nini kuhusu ubaguzi wa rangi,kuchochea wengine na kutenga wengine kando?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries