settings icon
share icon
Swali

Inamaanisha nini kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Mungu?

Jibu


Kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Mungu huanza wakati tunatambua mahitaji yetu kwake,tunakubali kuwa wenye dhambi, na katika imani tunapokea Yesu Kristo kama Mwokozi. Mungu, Baba yetu wa mbinguni, daima ametaka kuwa karibu na sisi, kuwa na uhusiano na sisi. Kabla ya Adamu kutenda dhambi katika bustani ya Edeni (Mwanzo sura ya 3), yeye na Hawa walimjua Mungu mioyoni katika hali ya kibinafsi. Walitembea pamoja naye katika bustani na kuongea moja kwa moja kwake. Kutokana na dhambi za mwanadamu, tulitenganishwa na uhusiano wetu kukatizwa kutoka kwa Mungu.

Chenye watu wengi hawajui,hawatambui, au kutunza, ni kwamba Yesu alitupa zawadi ya kushangaza zaidi - fursa ya kukaa milele na Mungu ikiwa tutamwamini. "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" (Warumi 6:23). Mungu akawa mwanadamu katika utu wa Yesu Kristo ili kuchukua dhambi zetu,akauwawe, na kisha kufufuliwa kuwa hai tena , akithibitisha kushinda dhambi na mauti. "Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu" (Warumi 8: 1). Kama tutapokea zawadi hii,tumekubaliwa na Mungu na tunaweza kuwa na uhusiano pamoja naye.

Kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Mungu ina maana kuwa tunapaswa kuhusisha Mungu katika maisha yetu ya kila siku. Tunapaswa kumwomba, tusome neno lake, na kutafakari kwa maandiko ili tupate kumjua vizuri. Tunapaswa kuomba kwa ajili ya hekima (Yakobo 1: 5), ambayo ni mali ya thamani zaidi tunaweza kuwa nayo kamwe. Tunapaswa kupeleka mahitaji yetu kwake,tukiuliza kwa jina la Yesu (Yohana 15:16). Yesu ndiye anayetupenda ya kutosha hadi kutoa uhai wake kwa ajili yetu (Warumi 5: 8), na Yeye ndiye aliyejaza pengo kati yetu na Mungu.

Tumepewa Roho Mtakatifu kama Mshauri wetu. "Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. "(Yohana 14: 15-17). Yesu alisema haya kabla ya kufa, na baada ya kufa Roho Mtakatifu akawa anapatikana kwa wale wote ambao kwa bidii walimtafuta kumpokea. Yeye ndiye anayehishi ndani ya mioyo ya waumini na kamwe haami.Anatushauri, anatufundisha ukweli, na anabadilisha nyoyo zetu. Bila hii Roho Mtakatifu , hatuwezi kuwa na uwezo wa kupambana dhidi ya maovu na majaribu. Lakini kwa kuwa tuko naye , tunaanza kuzalisha matunda yatokayo kwa kumruhusu Roho kutudhibiti, upendo, furaha, amani, uvumilivu, unyenyekefu,wema,, uaminifu, upole, na kujizuia kibinafsi (Wagalatia 5: 22-23 ).

Huu uhusiano wa kibinafsi na Mungu si vigumu kupata kama vile tunaweza fikiria, na hakuna namna ya ajabu ya kuipata. Punde tu tunapokuwa watoto wa Mungu,tunampokea Roho Mtakatifu, ambaye ataanza kufanya kazi katika mioyo yetu. Tunapaswa kuomba bila kukoma,tusome Biblia, na kujiunga na kanisa ambalo linaiamini Biblia; haya yote yatatusaidia kukua kiroho. Kumtegemea Mungu ili atuvushe kwa kila siku na kuamini kwamba Yeye ndiye mwenye riziki yetu ndio njia ya kuwa na uhusiano naye. Ingawa hatuwezi kuona mabadiliko mara moja, tutaanza kuyaona baada ya muda, na ukweli wote utakuwa wazi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Inamaanisha nini kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries