settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje nini kuhusu aina ya utawala wa kanisa?

Jibu


Bwana alikuwa wazi sana katika neno lake kuhusu jinsi Yeye anataka kanisa lake duniani kwa lipangwe na kusimamiwa. Kwanza, Kristo ni kichwa cha kanisa na mamlaka yake makuu (Waefeso 1:22; 4:15, Wakolosai 1:18). Pili, kanisa lenyewe linafaa kujitawala, liko huru kutoka mamlaka yoyote ya nje au udhibiti, na haki ya kujitawala na uhuru kutokana na kuingiliwa na uongozi wowote wa watu binafsi au mashirika (Tito 1:5). Tatu, kanisa linastahili kutawaliwa na viongozi wa kiroho likiwa na ofisi mbili kuu - wazee na mashemasi.

"Wazee" walikuwa viongoza wakuu katika Israeli tangu wakati wa Musa. Tunapata wao wakifanya maamuzi ya kisiasa (2 Samweli 5:3; 2 Samweli 17:4, 15), kushauri mfalme katika historia ya baadaye (1 Wafalme 20:7), na kuwakilisha watu kuhusu mambo ya kiroho (Kutoka 7:17, 24: 1, 9; Hesabu 11:16, 24-25). Mapema katika tafsiri ya Kiyunani ya Agano la Kale, ilitumia neno la Kigiriki presbuteros kumaanisha "mzee." Hii ni sawa na neno la Kigiriki lililotumika katika Agano Jipya ambalo limetafsiriwa pia "mzee."

Agano la Jipya mara nyingi sana linarejelea wazee ambao waliwahi tumika katika nafasi ya uongozi wa kanisa (Matendo 14:23, 15:2, 20:17, Tito 1:5; Yakobo 5:14) na inaonekana kila kanisa ilikua na zaidi ya mmoja, kama vile neon kwa kawaida linapatikana kuwa katika hali ya wingi. Isipokuwa tu inaelezea katika kesi ambacho mzee mmoja ametajwa kwa sababu fulani (1 Timotheo 5:1, 19). Katika kanisa la Yerusalemu, wazee walikuwa sehemu ya uongozi pamoja na mitume (Mdo. 15:2-16:4).

Inaonekana kwamba nafasi ya mzee ni sawa na nafasi ya episkopos, limetafsiriwa "mwangalizi" au "Askofu" (Matendo 11:30; 1 Timotheo 5:17). Neno "mzee" linaweza kutaja hadhi ya ofisi, wakati neno "askofu / mwangalizi" linaeleza mamlaka yake na wajibu (1 Petro 2:25, 5:1-4). Katika Wafilipi 1:1, Paulo anawasalimu maaskofu na mashemasi lakini haonekani kutaja wazee, labda kwa sababu wazee ni sawa na maaskofu. Vile vile, 1 Timotheo 3:2, 8 inatoa sifa za maaskofu na mashemasi lakini si ya wazee. Tito 1:5-7 inaonekana pia kufunga maneno haya mawili kwa pamoja.

Nafasi ya "shemasi," kutoka diakonos, maana yake "kwa njia ya uchafu," alikuwa mmojawapo ya uongozi wa utumishi kwa kanisa. Mashemasi ni tofauti na wazee, huku wakiwa na sifa kwa njia nyingi sawa na zile za wazee (1 Timotheo 3:8-13). Masemashi husaidia katika kanisa kwa kila njia wanayohitajika, kama kumbukumbu katika Matendo sura ya 6.

Kuhusu neno “poimen,” kutafsiriwa "mchungaji" likimaanisha kiongozi mwanadamu wa kanisa, linapatikana mara moja tu katika Agano Jipya, katika Waefeso 4:11: "Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na.” Wengi huunganisha majina hayo mawili "wachungaji" na "waalimu" wakimaanisha nafasi moja, wachungaji na walimu. Inawezekana kwamba mchungaji-walimu alikuwa mchungaji wa kiroho wa kanisa maalumu la nyumbani.

Inaonekana kutokana na vifungu hapo juu kwamba kulikuwa na siku zote wingi wa wazee, lakini hii haipunguzi karama fulani ya Mungu kwa mzee fulani mwenye karama ya ualimu huku akiwakirimia wengine karama ya utawala, sala, nk (Warumi 12:3-8; Waefeso 4:11). Wala haipunguzi wito wa Mungu kwao katika huduma ambayo wao hutumia vipawa hivyo (Matendo 13:1). Hivyo, mzee mmoja anaweza kuibuka kama "Mchungaji," mwingine anaweza kuwa ndiye anawatembelea wanachama wa kanisa sana, kwa sababu ana karama ya huruma, huku mwingine anaweza kuwa "mtawala" kwa namna ya utunzaji wa shirika. Makanisa mengi ambayo yanampangilio wa kikao cha wachungaji na Mashemasi hufanya kazi ya wingi wa wazee kiazi kwamba wanasaidiana katika huduma na kufanya kazi kwa pamoja katika kufanya maamuzi. Katika maandiko pia kulikuwa na wingi wa mchango kutoka kwa kanisa juu ya maamuzi. Hivyo, "dikteta" kiongozi ambaye hufanya maamuzi (hata kama anaitwa mzee, au askofu, au mchungaji) sio kibiblia (Matendo 1:23, 26; 6:3, 5; 15:22, 30; 2 Wakorintho 8:19). Sawa na lile kanisa ambalo haliupi uzito uamuzi wa wazee au viongozi wa kanisa' pembejeo lolote.

Kwa muhtasari, Biblia inafundisha uongozi wenye wingi wa wazee (Maaskofu / waangalizi) pamoja na kundi la mashemasi wanaotumikia kanisani. Lakini si kinyume na wingi huu wa wazee kuwa na mzee mmoja akiwahudumia katika jukumu la "uchungaji". Mungu uhita baadhi kama "mchungaji / walimu " (hata kama Alitoa wito baadhi kuwa wamisionari katika Matendo 13) na kuwapa kama zawadi kwa kanisa (Waefeso 4:11). Hivyo, kanisa linaweza kuwa na wazee, lakini si wazee wote wameitwa kutumika katika jukumu la uchungaji. Lakini, kama mmoja wa wale wazee, mchungaji au "mzee mwalimu" hana mamlaka zaidi katika kufanya maamuzi kuliko mzee weingine.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje nini kuhusu aina ya utawala wa kanisa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries