settings icon
share icon
Swali

Ni akina nani hawa 144,000?

Jibu


Kitabu cha Ufunuo daima kinamtoa mtafsiri na changamoto. Kitabu ni wamejichimbia katika picha ya wazi na mfano ambao watu wameutafsiri tofauti kulingana na dhana yaho ya kabla ya kitabu kwa ujumla. Kuna mbinu nne kuu za tafsiri kwa kitabu cha Ufunuo: 1) Wale ambao wanaoyaona matukio yote au wingi wa matukio katika Ufunuo kama kuwa tayari yametokea mwisho wa karne ya 1, 2) Wanahistoria (ambao wanaona Ufunuo kama utafiti wa historia ya kanisa kutoka nyakati za mitume hadi sasa); 3) Wale ambao wanaona Ufunuo kama picha ya mapambano kati ya mema na mabaya), 4) Wale ambao wanaona Ufunuo kama utabiri wa matukio yatakoyo kuja. Kati ya hizo nne, ni mbinu ye nne hutafsiri Ufunuo katika njia ya usarufi wa kihistoria kama maandiko mengine katika Biblia. Pia ni bora Ufunuo kudai kuwa unabii (Ufunuo 1:3; 22:07, 10, 18, 19).

Hivyo jibu kwa swali "144,000 ni akina nani?" Itategemea ni mbinu gani ya tafsiri ambayo utachukua kwa kitabu cha Ufunuo. Kando na mtazamo wa mbinu ya matukio yatakayo tokea, mitazamo mingine yote hutafsiri 144,000 kuwa ya mfano, kama mwakilishi wa kanisa na idadi 144,000 kuwa ishara ya ujumla -yaani, idadi-kamili ya kanisa. Hata hivyo, wakati kinachukuliwa katika thamani ya juu juu: " Kisha nikasikia idadi ya wale ambao walikuwa wametiwa mhuri: 144,000 kutoka kabila zote za Israeli" (Ufunuo 7:4 ), hakuna kitu katika kifungu hiki kinachoongoza kutafsiri 144,000 kama kitu chochote lakini ni takwimu ya kawaida ya Wayahudi -12, 000 ilichukuliwa kutoka katika kila kabila la "wana wa Israeli." Agano Jipya halitoi kifungu wazi ambacho huonyesha kuwa nafasi ya Israel imechukuliwa na kanisa.

Wayahudi wametiwa "muhuri," kumaanishaa wana ulinzi maalumu kutoka kwa Mungu kutoka kwa hukumu ya Mungu na kutoka kwa mpinga Kristo kutekeleza azimio lao wakati wa kipindi cha dhiki (angalia Ufunuo 6:17, ambapo watu watastaajabu ni nani ataweza kusimama dhidi ya ghadhabu inayokuja). Kipindi cha dhiki kuu ni baada ya kipindi cha miaka saba mwaka wa wakati ambamo Mungu atahukumu waliomkufuru, basi na kukamilisha mpango wake wa wokovu kwa taifa la Israeli. Yote haya ni kwa mujibu wa ufunuo wa Mungu kwa nabii Danieli (Danieli 9:24-27). Wayahudi 144,000 ni aina ya " uzao wa kwanza" (Ufunuo 14:4) wa Israeli kukombolewa ambao ulikuwa ni wa unabii (Zekaria 12:10, Warumi 11:25-27), na kazi yao ni kuinjilisha baada ya kunyakuliwa kwa dunia na kutangaza habari njema wakati wa kipindi cha dhiki. Kama matokeo ya huduma yao, mamilioni -"umati mkubwa wa watu kwamba hakuna mtu anaweza kuhesabu, kutoka kila taifa, kabila, watu na lugha" (Ufunuo 7:9 ) - watakuja kwa imani katika Kristo.

wingi wa machanganyiko kuhusu 144,000 ni kwa sababu ya mafundisho ya uongo ya Mashahidi wa Yehova. Mashahidi wa Yehova wanadai kuwa 144,000 ni ukomo wa idadi ya watu ambao watatawala pamoja na Kristo mbinguni na kuishi milele na Mungu. 144,000 wana kile Mashahidi wa Yehova huita matumaini ya mbinguni. Wale ambao si miongoni mwa 144,000 watafurahia kile wanachokiita tumaini la peponi ya duniani inayotawalwa na Kristo na 144,000. Ni wazi, tunaweza kuona kwamba mafundo ya Shahidi wa Yehova yantengeza jamii ya tabaka katika maisha ya baadaye na kikundi cha utawala ( 144,000) na wale ambao ni watatawaliwa. Biblia inafundisha hakuna "vitengo viwili". Ni kweli kwamba kulingana na Ufunuo 20:4 kutakuwa na watu tawala katika milenia pamoja na Kristo. Watu hawa watakuwa ni pamoja na kanisa (waumini katika Yesu Kristo), watu wa Mungu katika Agano la Kale (waumini waliokufa kabla ya ujio wa kwanza wa Kristo), na watu wa Mungu dhiki (wale wanaomkubali Kristo wakati wa dhiki ). Hata hivyo Biblia haiweki kikomo idadi ya kundi hiki cha watu. Aidha, milenia ni tofauti na hali ya milele, ambayo itafanyika katika mwisho wa kipindi cha milenia. Wakati huo, Mungu atakaa na sisi katika Yerusalemu Mpya. Yeye atakuwa Mungu wetu na sisi kuwa watu wake (Ufunuo 21:3 ). Urithi aliotuahidi katika Kristo, na kutiwa muhuri na Roho Mtakatifu (Waefeso 1:13-14) utakuwa wetu, na sisi wote kuwa warithi pamoja na Kristo (Warumi 8:17).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni akina nani hawa 144,000?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries