Swali
Agano la Adamu ni nini?
Jibu
Agano la Adamu linaweza kufikiriwa katika sehemu mbili: Agano la Edeni (lisilo na hatia) na Agano la Adamu (neema). Agano la Edeni linapatikana katika Mwanzo 1:26-30; 2:16-17. Maelezo ya kina ya agano hili hujumuisha yafutayo:
Mwanadamu (mwanamume na mwanamke) walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
Mwanadamu kutawala ufalme wa wanyama.
Maagizo ya kiungu kwa mwanadamu wapate kuzaa, kuijaza dunia na kuitiisha.
Mwanadamu kuwa mla mboga/majani (huku wakila nyama kama inavyonakiliwa katika Agano ya Nuhu: Mwanzo 9:3).
Kukanywa kula tunda la mti wa kujua mema na mabaya (kifo ndiyo adhabu inayotajwa).
Agano la Adamu lapatikana katika Mwanzo 3:16-19. Laana zifuatazo zilitamkwa, ikiwa ni matokeo ya dhambi ya Adamu:
Uadui kati ya Shetani na Hawa na uzao wake.
Wanawake kuzaa kwa uchungu.
Ugomvi katika ndoa.
Udongo ulilaaniwa.
Miiba na mibaruti kuwepo.
Kuishi kwa mapambano.
Kifo kuwepo.
Kifo kitakuwa hatima isiyoepukika kwa viumbe vyote vilivyo hai.
Ingawa laana hizi ni kali na haziepukiki, ahadi ya neema pia ilijumuishwa katika Agano la Adamu. Mwanzo 3:15 mara nyingi huitwa “mfano wa injili” au “Injili ya Kwanza”. Akizungumza na Shetani, Mungu anasema, “Nami nitaweka uadui kati kayo na huyo mwanamke, na kati ya uzao wake na wako, yeye atakuponda kichwa, nawe utamuuma kisigino.”
Hapa Mungu anaahidi kwamba mtu aliyezaliwa na mwanamke angejeruhiwa katika hali ya kumuangamiza Shetani. “Uzao” wa mwanamke ambaye angeponda kichwa cha Nyoka sio mwingine bali ni Yesu (Tazama Wagalatia 4:4 na 1 Yohana 3:8). Hata katikati ya laana, wokovu wa Mungu anayotoa kwa neema unang’aa.
English
Agano la Adamu ni nini?