settings icon
share icon
Swali

Agano la Nuhu ni gani?

Jibu


Agano la Nuhu linapatikana katika Mwanzo 9:8-17, ni ahadi ambayo Mungu alimpa Nuhu na uzao wake baada ya gharika iliyoangamiza ulimwengu. Agano la Nuhu lina sifa nyingi bainifu. Kwanza, ni agano lisilo la masharti. Pili, lilifanyiwa Nuhu pamoja na uzao wake wote “kila kiumbe hai” na dunia kwa ujumla (Mwanzo 9:8-10). Tatu, lilitiwa muhuri kwa ishara ya upinde wa mvua.

Agano la Nuhu ni agano lisilo la masharti kwa sababu halitegemei chochote ambacho Nuhu au uzao wake wangefanya ndio agano limitimie. Ahadi hii ina msingi wake katika uaminifu wa Mungu pekee. Kwa sababu ya uaminifu wa Mungu siku zote kufanya kile Anachosema atafanya, hii leo tunaweza kujua kwa uhakika kwamba hakutakuwa na gharika nyingine tena kwa ulimwengu kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, haijalishi kuwa ikiwa wanadamu watakuwa wouvu namna gani. Agano hili lisilo la masharti haliwezi athiriwa na uovu au uadilifu wa mwanadamu. Hakuna “masharti” ambayo kwayo yatamfanya Mungu aghairi ahadi yake. Hata hivyo, hiyo haimaanishi kwamba Mungu hataiangamiza dunia tena. Ameahidi siku moja kuiharibu duia kwa moto (2 Petro 3:10, 11; Ufunuo 20:9; 21:1) katika matukio ya kustaajabisha yanayojulikana kuwa “siku ya Bwana.”

Baada ya gharika Mungu aliahidi kwamba hatatuma tena gharika kwa dunia nzima ili kuiharibu dunia kama kitendo cha hukumu yake ya kiungu kwa ajili ya dhambi. Kama ishara ya kumkumbusha Nuhu na uzao wake juu ya ahadi yake ya agano, Mungu “Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni” (Mwanzo 9:12-13). Kama vile tohara ilivyokuwa ishara ya Agano la Abrahamu, upend wa mvua ni ishara ya Agano la Nuhu. Funzo kwetu ni kwamba tunapooana upinde wa mvua tunapaswa kukumbushwa daima juu ya uaminifu wa Mungu na neema yake ya ajabu. Tunapaswa pia kukumbushwa kwamba Mungu wetu ni Mungu mtakatifu na mwadilifu ambaye ana chuki takatifu kwa dhambi na ambaye hataruhusu dhambi iendelee bila kuadhibiwa milele. Pia, kama vile Mungu alivyotayarisha njia ili Nuhu na familia yake waokolewe ndani ya Safina, vile vile Ameandaa njia yetu kuokolwa kupitia Yesu Kristo. Nuhu na familia yake waliokolewa kutoka kwa ghadhabu ya Mungu iliyokuja katika gharika, na kama vile wale walio ndani ya Kristo wameokolewa kutokana na “ghadhabu inayokuja” (1 Wathesalonike 1:10).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Agano la Nuhu ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries