Swali
Je, Agizo Kuu ni gani?
Jibu
Mathayo 28: 19-20 ina kile ambacho kimekuja kuitwa Agizo Kuu: "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari." Yesu alitoa amri hii kwa mitume muda mfupi kabla ya kupaa kuelekea mbinguni, na kimsingi inaonyesha kile Yesu alitatarajia mitume, na wale walio wafuata, wafanye wakati hayupo.
Inavutia kwamba katika Kigiriki asili, amri pekee maalumu katika Mathayo 28: 19-20 ni “wafanye wanafunzi.“ Agizo linatuelekeza sisi tuwafanye wanafunzi tunapoenda duniani kote na tunapofanya shughuli zetu za kila siku. Ni vipi itupasavyo kuwafanya wanafunzi? Kwa kuwabatiza na kuwafunza yote ambayo Yesu aliamuru. "Wafanye wanafunzi" ni amri ya Agizo Kuu. "mtakapokuwa mkienda," "mkibatiza," na "kufundisha"ndizo njia ambazo kwazo tunatimiza amri ya "wafanye wanafunzi."
Wengi wanaelewa Matendo 1: 8 kama sehemu ya Agizo Kuu pia, "Lakini mtapokea nguvu wakati Roho Mtakatifu atakapowakujia kwenu; na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi yote, na Samaria, na hata kwa mwisho wa dunia. "Agizo kuu linawezeshwa na nguvu za Roho Mtakatifu.Tunapaswa kuwa mashahidi wa Kristo, tukitimiza Agizo kuu katika miji yetu (Yerusalemu), katika majimbo yetu na nchi (Yudea na Samaria), na mahali popote Mungu anatutuma (kwa mwisho wa dunia).
English
Je, Agizo Kuu ni gani?