Swali
Akiolojia ya Kikristo - kwa nini ni muhimu?
Jibu
Akiolojia linatokana na maneno mawili ya kigiriki -archae maana "ya kale," na logos maana "maarifa"; hivyo, "maarifa au masomo ya kale."Mwaakiolojia ni zaidi ya Indiana Jones aina ya mtu binafsi anayekimbia duniani kote kutafuta vyombo vya kale ili aweke kwa jumba la makumbusho. Akiolojia ni sayansi inayosoma tamaduni za kale kwa kupata tena na kuhifadhi vifaa kutoka siku za nyuma. Akiolojia ya kikristo ni sayansi ya kusoma tamaduni za kale ambazo zimegonganisha Ukristo na Uyahudi na tamaduni za Kiyahudi na Kikristo zenyewe. Si tu wanaakiolojia wa kikristo wanajaribu kufumbua vitu vya kale, wanajaribu kuhalalisha tunachojua tayari kuhusu zamani na kuendeleza kuelewa kwetu kwa tabia na desturi za watu wa Biblia.
Maandiko ya Biblia na kumbukumbu zingine zilizoandikwa ndizo vipande muhimu vya habari tunazo kuhusu historia ya watu wa kale wa Biblia. Lakini kumbukumbu hizi pekee zimeacha maswali mengi yasiyo na majibu. Hapo ndipo wanaakiolojia wakiristo wanakujia ndani. Wanaweza kujaza sehemu ya picha ambazo masimulizi ya kibiblia hutoa. Machimbuzi ya kale ya mahali pa kutupa taka na miji iliyoachwa yametoa hamasa ya kuanza shughuli na vipande vya kutupa dalili kwa siku za nyuma. Lengo la wanaakiolojia wakiristo ni kuthibitisha ukweli halisi wa Agano la Kale na Jipya kupitia kwa vyombo vya kale vya watu wa zamani.
Akiolojia ya kikristo haikuwa somo la kisayansi hadi karne ya 19.Nyezo za kujenga akiolojia ya kikristo ziliwekwa na watu kama vile Johann Jahn, Edward Robinson, na Sir Flinders Petrie. William F. Albright alikuja kuwa mtawala mkuu katika karne ya 20. Albright ndiye aliyefumbua akiolojia ya kikristo katika mijadala ya kisasa juu ya asili na kutegemewa kwa masimulizi ya Biblia. Ilikuwa Albright na wanafunzi wake ambao walitoa sehemu kubwa ya ushahidi halisi kwa matukio ya kihistoria yaliyoelezwa katika Biblia. Hata hivyo, leo inaonekana kana kwamba kuna wanaakiolojia wengi wanaojaribu kukanusha Biblia kama vile kuna wale wanaothibitisha kuwa ni sahihi.
Hatuna haja ya kwenda mbali sana kupata mashambulizi mapya kwa Ukristo kutoka ulimwengu wa kidunia. Mfano ni zaidi ya kuprogramu kwa mlangobahari wa ufumbuzi, kama vile "Da Vinci Code" docudrama.Matoleo mengine yanashughulikia uhistoria wa Kristo. Programu moja, na James Cameron, alidai kuwa kaburi na sanduku la kuzikwa la Yesu lilikuwa limepatikana. Kutokana na "ugunduzi" huu hitimisho ilitolewa kwamba Yesu hakuwa amefufuka kutoka kwa wafu.Chenye program haikusema ni kwamba sanduku liligunduliwa miaka ya awali na kwamba ilikuwa imethibitishwa tayari kuwa si sanduku la kuzikwa la Kristo. Maarifa haya yaliaafikiwa kupitia kwa kazi ngumu ya wanaakiolojia wa Kikristo.
Ni ushahidi wa akiolojia unaotoa habari halisi bora zaidi kwa maisha na nyakati za kale. Wakati njia sahihi za kisayansi zimetumika kwa kuchimbua maeneo ya kale, habari anaibuka ambayo inatupa kuelewa mkubwa wa watu wa kale na utamaduni wao na thibitisho zinazohalalisha maandiko ya Biblia. Rekodi za kiutaratibu za matokeo haya,yaliyogawa na wataalam duniani kote,yanaweza kutupatia habari kamili zaidi juu ya maisha ya wale waliokuwa wakiishi katika nyakati za Biblia. Akiolojia ya kikiristo ni mojapo ya zana wasomi wanaweza kutumia ili kuwasilisha utetezi zaidi kamili wa masimulizi ya kibiblia na injili ya Yesu Kristo. Mara nyingi, wakati kugawana imani yetu, tunauluzwa na wasiowaumini jinsi tunavyojua kuwa Biblia ni ya kweli. Moja ya majibu tunaweza kutoa ni kwamba, kupitia kwa kazi ya wanaakiolojia wakristo, ukweli mwingi halisi wa Biblia umehalalishwa.
English
Akiolojia ya Kikristo - kwa nini ni muhimu?