settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu baba we Kikristo?

Jibu


Amri kuu kabisa katika maandiko ni hii: “Nawe mpende BWAN, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa nguvu zako zote” (Kumbukumbu La Torati 6:5). Tukirudi nyuma kwa aya ya 2 tunasoma, “Upate kumcha BWANA, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe.” Kufuatilia Kumbukumbu La Torati 6:5 tunasoma, “Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo” (aya ya 6-7).”

Historia ya Waisraeli yafichua kwamba baba alistahili kuwa wa hekima katika kuwapa maagizo watoto wake katika njia za Mungu na neno lake kwa minajili ya ukuaji wao kiroho na maisha yao. Baba ambaye alikuwa mtiivu kwa sheria za maandiko alifanya hivyo. Hii inatuleta katika Methali 22:6, “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokokuwa mzee.” “kumlea” inaonyesha yale maagizo ya kwanza ambayo baba na mama wanampa mtoto, kwa mfano, elimu yake ya mapema. Ulezi umepangwa kuweka wazi kwa mtoto vile maisha yanastahili kuwa. Kwa kuendelea, elimu ya mapema ya mtoto kwa njai hii ni ya muimu sana.

Waefeso 6:4 ni ufupisho wa maagizo kwa baba mzazi, ambayo yametajwa yote yanayofaa na yasiyo faa. “Nanyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwan.” Sehemu ya ukanusho wa aya hii yaonyesha kwamba baba mzazi hastahili kuweka maagizo maovu ndani ya watoto wao kwa, kuwakataa, bila haki, ubaguzi au mamlaka yasiyostahili. Ukali, tabia sisizostahili kwa watoto kwa maana hizi zitatunza maovu kwa moyo wao. Neno “msiwachokoze” lamaanisha “kuchukiza, ghadhibisha, na kufikicha mkono kwa njia isiyosthaili au kuwachochea.” Haya yanafanywa kwa roho mpaya na mitindo mipaya, kwa njia isiyostahili, kwa tetezi, ukali, vizuizi visivyostahili, sisitizo la kiuchoyo juu ya mamlaka yakihimla. Chukizo kama hizo zitazaa tabia isiyofaa, kuua hisia za upendo kwa watoto, na kupunguza hisia za utakatifu, na kuwafanya kuhisi kuwa hawatawafurahisha kamwe wazazi wao. Mzazi mwenye hekima anatafuta kuona kuwa utiivu umetamanika miongoni mwa watoto na upendo umepatikana kwa ukarimu.

Sehemu ya manufaa ya Waefeso 6:4 imefafanuliwa kwa mwelekeo wa ndani sana- waelimishe, welee, kuza tabia yao katika maisha yao kwa kuwaelekeza na kuwafunza neno la Mungu. Huu ni mchakato wote wa kuelimisha na kuonya. Neno “wafunze” labeba dhana ya kukumbusha mtoto makosa yake (kwa njia inayo faa) na majukumu yake.

Baba Mkristo ni chombo katika mikono ya Mungu. Mchakato wote wa maagizo na maonyo lazima yawe yale ambayo Mungu ameyaamuru na ambayo anayasimamia, ili mamlaka yake yaletwe katika hali ya kuendele na kukutana na akili, moyo na hisia za mtoto. Baba wa damu hastahili kujidhhirisha kama mwenye mamlaka yote anayebaini ukweli na jukumu. Ni kufanya Mungu pekee mwalimu na mfalme ambaye kwa mamlaka yake kila kitu kumeumbwa na lengo la kuelimisha litaweza afikiwa vizuri sana.

Martin Luther alisema, “Liweke tunda kando ya kiboko ili umpe akifanya vyema.” Nidhamu lazima itekelezwe kwa umakini sana na mafundisho kila siku kwa maombi mengi. Taadibu, nidhamu na mashauri kwa neno la Mungu, yote yanatoa maonyo na utiaji moyo yako katikati ya “mafunzo.” Maonyo yanaendelea kutoka kwa Mungu, yanafunzwa katika mashule za uzoefu wa Kikristo, na yanasimamiwa na wazazi- has baba mzazi, lakini pia chini ya maelekezo yake mama. Nidhamu ya Kikristo inahitajika kumwezeza motto kukuwa kwa kumcha Mungu, kuwaeshimu wazazi, elimu ya kanunu za Kikristo na mozoea ya kujizuia.

“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katka haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2 Timotheo 3:16-17). Jukumu la baba la kwanza ni kumzoesha mtoto na maandiko. Njia na mitindo ambayo baba anaweza kutumia kumfunza ukweli wa Mungu zitategemea. Kwa vile baba ni mwaminifu kwa kuwa kielelezo, chenye watoto watasoma kuhusu Mungu kitawaweka katika kanuni nzuri na kuishi katika maisha yao yote duniani, haijalishi ni nini watafanya au ni wapi wataenda.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu baba we Kikristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries