Swali
Bibilia inaweza tumika siku hizi?
Jibu
Waebrania 4:12 yasema, “Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigagwanya nafsi na roho na viungo na mafuta yaliiyomo ndani yake; tena li jepesi kuayatambua mawazo na makusudi ya moyo” wakati Bibilia ilikamilika takiribani miaka 1900 iliyopita, ukamilifu wake na umuimu wake siku hizi vilipaki bila kibadilishwa. Bibilia ndiyo chombo pekee cha ufunuo Mungu ametupa kuhusu yeye na mpango wake kwa mwanadamu.
Bibilia yabeba habari/ujumbwe mwingi kuhusu ulimwengu unao onekana na haya yamethibitishwa na wanasayansi na watafiti. Baadhi ya kurasa kama Mambo Ya Walawi 17:11; Mhubiri 1:6-7; Ayubu 36:27-29; Zaburi 102:25-27 na Wakolosai 1:16-17. Kwa vile hadithi ya Bibilia ya mpango wa Mungu wa ukombozi kwa mwanadamu umefunuliwa, wahusika wengi wameelezewa. Katika maelezo hayo, Bibilia yatupa habari nyingi kuhusu tabia ya mwanadamu na maumbilie yake. Uzoefu wetu wa siku baada ya siku watuonyesha habari hii yaweza kuaminika haina kasoro yoyote na inaelezea hali ya mwanadamu na ni kitabu cha kiakili. Nyingi ya hoja za kiistoria ambazo zimeandikwa katika Bibilia zimethibitishwa na sehemu zingine za kibibilia (vitabu na mitandao). Utafiti wa historia waonyesha mkubaliano mkubwa kati ya matukio ya Kibibilia na matukio yaliyo nche ya Bibilia ambayo yanaonekana sawa na hayo ya Bibilia.
Hata hivyo, Bibilia si kitabu cha historia, kitabu cha saikologia (akili) ama nakala ya kisayansi. Bibilia ni mwelekeo ambao Mungu alitupa, kuhusu jinsi alivyo na matamanio yake na mpango wake kwa mwanadamu. Sehemu muimu sana ya ufunuo huu na hadithi kuhusu utengano wetu na Mungu na juudi za Mungu na urejesho wake wa ushirika kupitia kwa Mwanawe Yesu Kristo msalabani. Hitaji letu la ukombozi halibadiliki. Vilevile Mungu hadhihirishi nia yake ya kutuunganisha pamoja naye.
Bibilia iko na habairi kamilifu na ni muimu kwa maisha yetu hii leo. Ujumbe wa maana katika Bibilia wa- ukombozi ni wa ulimwengu wote na wawafaa wanadamu wote. Neno la Mungu kamwe halitawai kupitwa na wakati, lishindwe au lijengwe zaidi. Tamaduni zabadilika, sheria zabadilika, kizazi kinakuja na kizazi kinaenda, lakini neno la Mungu liko siku zote vile lilikuwa wakati liliandikwa mara ya kwanza. Si kila sehemu ya Bibilia yaweza kutufaa hii leo, bali aya zote ziko na ukweli ambao tunaweza na tunastahili kuutumia katika maisha yetu.
English
Bibilia inaweza tumika siku hizi?