settings icon
share icon
Swali

Kunao kitu kama wageni au UFOs?

Jibu


Kwanza, wacha tulifafanue neno “wageni” kama “kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi ya kimaadili, kuwa na akili, hisia na hiari.” Enye kufuata ni hoja za kisayansi:

1. Binadamu wametuma chombo cha anga karibu kwa kila sayari katika mfumo wetu wa sayari. Baada ya kuzichunguza hizi sayari tumefutilia mbali zote ila tu sayari ya Mars na pengine mwezi wa Jupita kama kuwa na uwezo wa kukimu maisha.

2. Katika mwaka wa 1976, Marekani ilituma viongozi wawili kuelekea Mars. Kila mmoja wao alkuwa na chombo ambacho kingechimba ndani ya Muchanga wa Mars na kuuchunguza kama kuna dalili yo yote ya kukimu maisha. Hawakupata kitu cho chote kabisa. Kwa ulinganisho ikiwa utauchunguza mchanga kutoka kwa changwa tasa au tope liloganda kutoka Antaktiki, utapata kuwa kuna wadudu wamejazana huko. Katika mwaka wa 1997 Marekani ilituma mvumbuzi kwenda anga ya Mars. Hawa wazuluraji walichukua sampuli na kufanya utafiti mwingi. Walipata pia hakuna dalili ya maisha huko. Tangu wakati huo, kuna safari nyingi zimefanywa kwenda Mars. Matokeo kila mara yamekuwa yale yale.

3. Majusi kila mara wanagundua sayari mpya kitika mfumo wa jua la mbali. Wangine wanapendekeza kuwa kuwepo kwa sayari nyingi wathibitisha kuwa lazima kuwe na maisha mahali kwingine mbali na dunia. Ukweli ni huu, kuwa kati ya hizi sayari zote hakuna ile ambayo imewai thibitishwa kuwa inaweza kukimu maisha. Umbali wa ajabu uliopo kati ya ardhi na sayari hizi unaifanya vigumu kufanya uamuzi kuhusu uwezo wao wa kukimu maisha. Tukijua kwamba ardhi peke ndiyo inakimu maisha katika jua letu, wavumbuzi wanataka kwa vyovyote vile kugundua sayari nyingine katika jua lingine la kukimu maisha ili waunge dhana kuwa maisha yalijibuka. Kunazo sayari zingine nyingi kule nche, lakini kwa hakika hatujui ya kutosha kuzihusu kuthibitisha kwamba zinaweza kukimu maisha.

Kwa hivyo, Bibilia inasema nini? Ardhi na wanadamu ni wa ajabu katika uumbaji wa Mungu. Mwanzo 1 yafunza kuwa Mungu aliumba ardhi kabla hata aumbe jua, mwezi au nyota. Matendo Ya Mitume 17:24, 26 yasema, “Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono… Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao.”

Kwanza, mwanadamu hakuwa na dhambi, na kila kitu katika ulimwengu kilikuwa “kizuri sana” (Mwanzo 1:31). Wakati mtu wa kwanza alisini (Mwanzo 3), matokeo yalikuwa ni shida za kila aina yote, ikiwemo ugonjwa na kifo. Hata kama wanyama hawana dhambi ya kibinafsi mbele za Mungu (wao si viumbe vya maadili), bado wanatezeka na kufa (Warumi 8:19-22). Yesu Kristo alikufa kuondoa adhabu ambayo tulihistahili ya dhambi. Wakati atakapo rudi, ataiondoa laana ambayo imekuwa ikidumu tangu Adamu (Ufunuo 21-22). Si kwamba Warumi 8:19-22 yasema kuwa viumbe vyote wanangoja wakati huo. Ni muimu kutambua kwamba Kristo alikuja kufa kwa ajili ya mwanadamu na kwamba afe mara moja peke (Waebrania 7:27; 9:26-28; 10:10).

Kama viumbe wote sasa wanatezeka chini ya laana, maisha mengine mbali na ya dunia yatatezeka pia. Ikiwa ni kwa sababu ya pingamizi, ikiwa viumbe vyenye maadili vinaishi katika sayari nyingine, kwa hivyo pia hoa wanatezeka; na kama si sasa, basi siku nyingine hakika watatezeka wakati kila kitu kimetoweka kwa ile sauti kubwa na kila kitu kitayeyuka kwa ule mto mkali (2 Petero 3:10). Ikiwa hakuwai kutenda dhambi, basi Mungu hatakuwa wa haki kwa kuwaadhibu. Lakini ikiwa walikwisha tenda dhambi, na Kristo angekufa mara moja (ambayo alifanya katika ardhi), basi wameachwa ndani ya dhambi zao, ambazo pia itakuwa kinyume na tabia ya Mungu ( 2 Petero 3:9). Hii inatuacha na sadifa ambayo haijazuluhishwa- ila tu peke kuwe hakuna viumbe wenye maadili katika ardhi.

Je! Itakuwaje kwa vile viumbe havina maadili na vizivyo-ishi katika sayari zingine? Je! Mwani au mbwa na paka watakuwepo katika sayari hazijulikani? Kwa kuchukulia hivyo, na haitawadhuru andiko lolote la kibibilia. Lakini kwa kweli itathibitisha tatizo wakati tunajaribu kujibu maswali kama “kwa vile viumbe wote watezeka, Mungu alikuwa na lengo gani kwa kuwaumba viumbe wasio na madili na viumbe wasio na uai kutezeka katika sayari za mbali?”

Kwa kumalizia, bibilia haitupi sababu yo yote ya kuamini kwamba kuna maisha mahali kwingine katika anga. Kwa kweli, Bibilia inatupa sababu kuu nyingi ni kwa nini hakutakuwa na uai. Naam, kunayo mambo mengi ya ajabu na yasiyoelezeka ambayo yatokea. Hamna sababu, wazo, la kufikiria kwa jambo hili la wageni au UFOs. Kama kunayo mwelekeo ambao ni wa kutambulika kwa tukio hili la kudhaniwa, basi kuna uwezekano kuwa utakuwa ni ule wa kiroho, na hasa wa kishetani kiasili.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kunao kitu kama wageni au UFOs?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries