settings icon
share icon
Swali

Je! Bibilia inakubalia utumwa?

Jibu


Kuna tabia ya kuangalia utumwa kama kitu cha kale. Lakini imekadiriwa kuwa kuna hii leo watu milioni 12 katika dunia ambao ni watumwa: kazi ya kulazimishwa, biashara ya usherati, mali ya kuridhiwa, na kadhalika. Kwa wale ambao wamekombolewa kutoka kwa utumwa wa dhambi, wafuasi wa Yesu Kristo lazima wawe mustali wa mbele wa kumaliza utumwa duniani hii leo. Swali linajipusa, hata hivyo ni kwa nini Bibilia haizungumzii kwa nguvu ikipinga utumwa? Ni kwa nini Bibilia kwa kweli, yaonekana kuunga mkono tendo la utumwa wa mwanadamu?

Bibilia moja kwa moja haipingi tendo la utumwa. Inapatiana maagizo jinsi ya vile watumwa wanastahili kuchukuliwa (Kumbukumbu La Torati 15:12-15; Waefeso 6:9; Wakolosai 4:1), lakini haifutilii mbali utumwa kabisa. Wengi wanaiona hii kuwa Bibilia inaikubalia aina zote za utumwa. Chenye wengi wanakosa kuelewa ni kuwa utumwa katika nyakati za Bibilia ulikuwa tofauti kutoka ule utumwa ulikuwa ukifanyika katika karne chache zilizopita katika sehemu nyingi za dunia. Utumwa katika Bibilia haukuwa kwa misingi ya rangi. Watu hawakupelekwa mateka kwa sababu ya utaifa wao au rangi ya ngozi yao. Katika nyakati za Bibilia, utumwa ulikuwa hasa hali ya cheo katika jamii. Watu walijiuza wenyewe kama watumwa wakati hawangeweza kulipa deni zao au kuweza kulisha familia zao. Katika nyakati za Agano Jipya, wakati mwingine madaktari, mawakili, na hata wanasiasa walikuwa watumwa wa mtu mwingine. Watu wengine walichagua kuwa watumwa ili wapate mahitaji yao yatimizwe na wakubwa wao.

Utumwa wa karne chache zilizopita hasa ulikuwa kwa misingi ya rangi ya ngozi. Marekani, wengi wa watu weusi walichukuliwa kuwa watumwa kwa sababu ya utaifa wao; wamiliki wa wengi wa watumwa kwa kweli waliamini kuwa watu weusi si wanadamu kamili. Bibilia basi inakataa utumwa kwa misingi ya rangi. Uchukulie utumwa Wayahudi walikuwa nao wakati walikuwa Misri. Wayahudi walikuwa watumwa, si kwa kupenda kwao, lakini kwa sababu walikuwa Wayahudi (Kutoka 13:14). Mapigo ambayo Mungu aliyaachilia kwa Wamisri yaonyesha vile Mungu anahisi kuhusu utumwa wa ubaguzi wa rangi (Kutoka 7-11), kwa hivyo, naam, Bibilia haikatai baadhi ya utumwa. Kwa wakati huo huo, Bibilia haionekani kukubalia aina zingine za utumwa. Hoja kuu ni kuwa utumwa Bibilia iliruhusu kwa njia yo yote ile haufanani na ule utumwa wa rangi ambao ulipiga nchi yetu katika karne chache zilizopita.

Kwa kuongezea, zote Agano La Kale na Jipya zakemea tendo la “kuiba-mtu” ambayo ndiyo ilifanyika Afrika katika karne ya 19. Waafrika walifungwa na wawinda watumwa, ambao waliwauza kwa wanunuzi wa watu, ambao waliwaleta katika ulimwengu mpya wa kazi katika mashamba yao. Tendo hili ni chukizo kwa Mungu. Kwa kweli adhabu ya kosa kama hilo katika sheria ya Musa ilikuwa kifo: “Yeye amwibaye mtu, na kumwuuza, au akipatikana mkononi mwake sharti atauawa huyo” (Kutoka 21:16). Vilevile, katika Agano Jipya, uuzaji na ununuzi wa watu umetajwa kati ya wale ambao si “wacha Mungu” na wako katika kiwango kimoja na wale wanawaua baba zao au mama zao, wauaji, wazinzi na wageuza kweli, na waongo (1 Timotheo 1:8-10).

Pointi nyingine ya muimu sana, ni kuwa lengo la Bibilia ni kuonyesha njia ya wokovu, si kubadilsha kijiji. Bibilia kila mara yakabiliana na hali kutoka ndani nche. Ikiwa mtu anahisi upendo, huruma na neema ya Mungu kwa kupokea wokovu wake, Mungu ataipadilisha nafsi yake, na kumpadilisha njia anayofikiri na kutenda. Mtu ambaye amehisi kipaji cha Mungu cha wokovu na uhuru kutoka kwa utumwa wa dhambi, Mungu anapobadilisha nafsi yake, mtu huyo atagundua kwamba kumweka utumwa mwanadamu mwingine ni makosa. Mtu ambaye kwa kweli amehisi neema ya Mungu vilevile naye pia atakuwa wa neema kwa wengine. Hiyo litakuwa elezo la Kibibilia la kumaliza utumwa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Bibilia inakubalia utumwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries