Swali
Je! Biblia inasema kwamba kutekelezwa ni sababu halali ya talaka na kuoa tena?
Jibu
Ni ukweli wa kusikitisha kwamba Wakristo wakati mwingine wanakabiliwa na kutekelezwa na wenzi wao. Ingawa Mungu alipanga wanandoa kuoana hadi kifo (Mwanzo 2:24) na kumpa talaka mwenziwe wa ndoa ni dhuluma sawa na unyanyasaji (Malaki 2:16), pia Anatambua Wakristo huenda hawatakuwa na udhibiti juu ya kile wenzi wao wanachofanya. Katika hali ambapo mwenzi asiyeamini anamtekeleza muumini, Mungu hutoa neema kwa yule aliyetelekezwa.
Je! mwenzi aliyetelekezwa ana uhuru gani?
Paulo anaeleza, “Lakini kama yule asiyeamini akijitenga, basi afanye hivyo. Katika hali kama hiyo mwanamke au mwanaume aaminiye hafungwi, kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani” (1 Wakorintho 7:15), Andiko liko wazi kwamba, mwezi asiyeamini akijitenga, aaminiye yuko huru kukubali kutengana na kuendelea na maisha. Yeye, “hajafungwa” kuonyesha uhuru kamili. Mwenzi anayeamini anaweza na anapaswa kutafuta upatanisho (I Wakorintho 7:11), lakini hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mwingine kutenda kinyume na hiari yake.
Na je, ikiwa mwenzi anayejitenga ni muumini?
Maagizo ya Paulo katika 1 Wakorintho 7 yanahusu hasa ndoa mchanganyiko—muungano kati ya muumini na asiyemuumini. Katika hali ya Wakristo wawili waliooana, 1 Wakorintho 7 haiwezi tumika. Katika hali hiyo, tunageukia maeneno ya Yesu katika Mathayo 18: 15-17: “Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonyeshe kosa lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Kama akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. Lakini kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno lithibitishwe kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu. Kama akikataa kuwasikiliza hao, liambie kanisa. Naye kama akikataa hata kulisikiliza kanisa, basi awe kwenu kama mtu asiyeamini au mtoza ushuru.”
Ikiwa muumini anaishi katika dhambi isiyotubu— katika hali hii, kumwacha mwenzi—hata baada ya kukabiliwa na uongozi wa kanisa, atachukuliwa kuwa asiyeamini. Kwa njia hiyo, 1 Wakorintho 7:15 inaweza kutumika kwa waumini ambao huwatelekeza wenzi wao na kukataa kuitikia nidhamu ya kanisa.
Ni kipi kinachohitimiza telekezo?
Katika muktadha huu, kutelekezwa kunamaanisha kutengana kimwili au talaka. Ikiwa mmoja wa wanandoa atamwacha mwingine, awe ameondoka nyumbani hasa, ndoa hiyo hiyo inavunjika, kwa madhumini yote ya vitendo. Mwenzi aliyetelekezwa yuko huru kumwachilia mwenziwe. Mwenzi aliyeachwa nyuma “hajafungwa,” na kile tunacho chukua kuwa adili na kiroho. Hakuna kitu kinachomfunga mwenzi kwa yule aliyemtelekeza. Mwenzi aliyeachwa ana uhuru wa talaka na uhuru wa kuolewa tena, ingawa hatakiwi kufanya hivyo.
Ikiwa kuachana kunatokea kwa mwenzi mmoja kuwasilisha talaka, basi mwenzi anayeachwa yuko huru kutia sahihi makaratasi, mara tu majaribio yote ya upatanisho yameshindwa. Hakuna dhambi au aibu kwa mwenzi aliyeachwa. Kukubali kuvunjika kwa ndoa ni sehemu ya kufuata mwito wa Mungu wa kuishi kwa amani.
Baadhi ya washauri na makasisi, wakiazimia kuwa wenye neema, wamefafanua kutelekezwa kwa mapana kupita kiasi. Wengine husema kwamba inaweza kuwa ni kwa sababu ya magumu kutokana na uraibu, ugonjwa wa akili, vifungo vya jela, au ukosefu wa fadhili. Hiyo sio ufafanuzi wa kibiblia wa kutelekeza, hata hivyo—isipokuwa ugumu kama huo unazidi kiwango na kuwa vita, lakini hoyo ni mada tofauti.
Ikiwa mtu ameachwa, je, anaweza kuolewa tena?
Biblia haisemi. Uzinzi na talaka bila hiari ndizo pekee zimesungumziwa katika Biblia kama sababu ya talaka—hali mbili pekee ambazo mtu aliyetalakiana anaweza kusemekana kuwa hakutenda dhambi. Katika Mathayo 19:9, Yesu anaruhusu kwamba mtu anayemwacha mwingine kwa misingi ya uzinzi wa mwenzi wake anaweza kuoa tena. Tafsiri inaweza kuwa kati ya hizi mbili 1) kwa kuwa Biblia haitaji kuoa tena baada ya talaka bila hiari, hairuhusiwi; au 2) kwa kuwa kesi moja inaruhusu kuolewa tena kwa mhusika asiye na hatia, yule mwingine pia anaweza kufanya hivyo.
Ni mtazamo wetu kwamba mtu ambaye amepewa talaka bila hiari yake—yaani, mwathiriwa wa telekezo—anaweza kuolewa. Maneno hayo hayajakatazwa na 1 Wakorintho 7:15 inaonekana kutoa aina hiyo ya uhuru. Hata hivyo, mtu anayetaka kuolewa tena anapaswa kufanya hivyo kwa tahadhari kubwa. Kunapaswa kuwa na wakati wa kupona kutokana na mshutuko wa uhusiano uliovunjika, ili kuchambua yale yote yaliyochangia kuvunjika kwa uhusiano, na kutafuta mapenzi ya Mungu kwa wakati ujao.
Je! mtu aliyetelekezwa daima hana hatia?
La sivyo. Watu wengine, wasio furahia ndoa yao, watafanya chochote wawezacho kumfukuza mwenzi wa ndoa aondoke kisha waanzishe mchakato wa talaka, huku wakibaki kuwa “wasio na hatia.” Lakini hio sio kubaki bila hatia, ni dhambi ya unyanyasaji na ghaliba. Unyanyasaji katika ndoa—na hata kwa kujibu unyanyasaji—ni dhambi, na hiyo inahitaji toba mbele za Mungu na kuungama kwa uliyemkosea.
English
Je! Biblia inasema kwamba kutekelezwa ni sababu halali ya talaka na kuoa tena?