settings icon
share icon
Swali

Je, ni mtazamo gani wa kibiblia kuhusu ujinsia?

Jibu


Ujinsia wa binadamu, pamoja na maumbile yake, kihisia na kiroho, ulikuwa uvumbuzi wa Mungu. Aliwapa viumbe vyake vya kibinadamu ujinsia kama zawadi yenye kazi mbili: kuendeleza jamii ya binadamu na kuunda uhusiano wa karibu kati ya mume na mke. Matumizi sahihi ya ujinsia hutuongoza kuelewa ukaribu na Mungu kwa njia kubwa zaidi; matumizi mabaya yake huharibu uhusiano wa karibu na Mungu na ujinsia kuchukua nafasi ya Mungu. Ili kuelewa mtazamo wa kibiblia wa ujinsia, tutachunguza asili yake yenye pande nyingi kipengele kimoja baada ya kingine.

Kutajwa kwa kwanza kwa ujinsia katika Biblia ni katika bustani ya Edeni. Mungu aliwaambia Adamu na Hawa “zaeni, mkaongezeke, mkaijaze dunia” (Mwanzo 1:27-28), amri ambayo inalazimu ngono. Muda mfupi baada ya hapo, tunasoma kwamba Adamu “akakutana kimwili na mkewe Hawa, naye akapata mimba” (Mwanzo 4:1). Matumizi hayo ya neno kukutana ni tafsiri kamili zaidi ya dhana hii kuliko misemo ya kisasa kama vile “kuwa na mahusiano ya ngono.” Inaashiria mengi zaidi kuliko tendo la kimwili. Wakati Adamu “alikutana” na mkewe, wanandoa wa kwanza walikuwa na ujinsia namna ambayo Mungu alikuwa amewazawadi. Ngono ilipaswa kuwa tendo la kuunganisha walilofannya kwa pamoja ambalo lilikuwa tofauti na muungano mwingine wowote. Iliundwa mahususi na Muumba wao ili liwe tendo moja la karibu zaidi ambalo wanadamu wawili wangeweza kupata. Ndani ya ndoa ya agano, muungano wa kingono ni mvuto unaofunga na unaoleta wanandoa pamoja kama “mwili mmoja” (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:6). Wanagundua na kushiriki wao kwa wao kwa njia ambazo ni za kipekee kwa wanandoa na kuunda umoja mtakatifu.

Chochote anachoumba Mungu, Shetani hukipotosha. Haikuchukua muda mrefu kwa wanadamu walioanguka kupotosha na kuharibu zawadi takatifu ya Mungu ya ujinsia. Kufikia wakati ambapo Mungu aliwapa Waisraeli Sheria, Aliwakataza aina zote potovu za kingono ambazo zilikubaliwa na tamaduni za wakati huo. Mungu alikuwa tayari amemteua mwanamume mmoja kwa mwanamke mmoja tangu uumbaji lakini sasa ilimbidi kufafanua na kukataza kila aina ya upotovu ambao watu walikuwa wamebuni. Ni idadi ya watu duniani ilipoongezeka, Mungu aliimarisha mipaka ya kiadili kuhusu kuoa watu wa ukoo wa karibu. Walawi 18 na 19 hufafanua desturi nyingi zilizokatazwa, kama vile kufanya ngono na mtu wa karibu wa familia, uzinzi, na ushoga.

Ingawa mitala ilistahimiliwa wakati wa Agano la Kale, kwa kiasi fulani kutokana na ukosefu wa chaguzi kwa wanawake wasio na waume na hitaji la wanaume kuwa na watoto wengi wa kiume kwa ajili ya kuendeleza ukoo wa familia, desturi hiyo ilikuwa haipo katika nyakati za Agano Jipya. Kwa kweli, Yesu alirudia kusudi la kwanza la Mungu la ndoa alipoulizwa kuhusu talaka. Katika Mathayo 19:3-6 Yesu alisema, “Hapo mwanzo Muumba aliwaumba mwanaume na mwanamke, naye akasema, ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.” Kuwa mume wa mke mmoja tu lilikuwa hitaji la uongozi wa kanisa (1 Timotheo 3:2, 12; Tito 1:6).

Asilimia kubwa ya matatizo ya ulimwengu yanatokana moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na matumizi mabaya ya zawadi ya Mungu ya ujinsia. Hebu wazia ulimwengu ambao tungekuwa nao ikiwa kila mwanadamu angefuata viwango vya Mungu kuhusu ujinsia. Uavyaji mimba, talaka, magonjwa ya zinaa, UKIMWI, ponografia, biashara haramu ya ngono, ubakaji, watoto waliotelekezwa, na ulawiti wa watoto vyote vingekoma au kupungua sana. Athari za mabadiliko hayo pekee zingebadilisha kabisa kila bara, kila taifa, na kila utamaduni. Uchumi ungeongezeka, magonjwa yangepungua, na hospitali za wagonjwa wa akili zingekuwa na vitanda tupu.

Mungu anajua anachozungumza anapojumuisha mipaka katika karama zake. Umeme ni uvumbuzi wa ajabu na ukitumiwa ipasavyo huwanufaisha wanadamu wote. Hata hivyo, ikitumiwa vibaya, umeme unaweza kulemaza au kuua. Ndivyo ilivyo kwa nguvu ya ujinsia wa mwanadamu. Ujinsia huwa ni zawadi nzuri sana tunapotafuta kuishi ndani ya mipaka yenye nzuri ambayo Mungu aliiweka kwa ajili ya ustawi wetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni mtazamo gani wa kibiblia kuhusu ujinsia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries