Swali
Je! Biblia inasema nini kuhusu kuwa msagaji? Je, biblia inataja usagaji?
Jibu
Wengine wanadhani kwamba, ingawa Biblia inashutumu ngono ya mashoga kati ya wanaume, hakuna mahali inalaani kuwa msagaji/usagaji. Walawi 18:22 na 20:13 inataja wanaume kufanya ngono na wanaume wengine, lakini haisemi chochote kuhusu wanawake kufanya ngono na wanawake wengine. Katika simulizi ya Sodoma na Gomora katika Mwanzo 19, wanaume wa miji walitaka kuwabaka wanaume wengine. Wakorintho wa Kwanza 6:9 inawataja wanaume wenye tabia za kike, ambayo kuna uwezekano kuwa inarejelea mashoga, lakini haiwataji wasagaji. Kwa hivyo, je, Biblia kwa hakika inalaani ushoga wa wanaume, lakini sio usagaji?
Warumi 1:26-27 inaliweka swala hili vyema: “Kwa sababu hii, Mungu aliwaacha wavunjiane heshima kwa kufuata tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao wakabadili matumizi ya asili ya miili yao wakaitumia isivyokusudiwa. Vivyo hivyo wanaume pia wakiacha matumizi ya asili ya wanawake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wakafanyiana matendo ya aibu na wanaume wengine nao wakapata katika maisha yao adhabu iliyowastahili kwa ajili ya upotovu wao.” Kwa wazi, kifungu hiki kinaweka ushoga katika kiwango sawia na ushoga wa kiume. Usagaji unaelezewa kuwa wanawake kuacha kujamiana na wanaume vile ilivyo kiasili na kuwa uhusiano usio wa kiasili (na wanawake wenzao). Kulingana na Biblia, kuwa msagaji ni dhambi sawia na ushoga.
Kuna wazo katika Warumi 1:26 kwamba usagaji ni mbaya zaidi kuliko ushoga wa kiume. Kumbuka kifungu “hata wanawake wao.” Maandishi hayo yanaonekana kupendekeza kwamba ni kawaida zaidi kwa wanaume kujihusisha na upotovu wa ngono, na wanawake wanapoanza kufanya hivyo, hiyo ni ishara kwamba mambo yanazidi kuwa mabaya. Wanaume kwa kawaida huwa na misukumo ya ngono yenye nguvu zaidi kuliko wanawake, na kwa hivyo huwa katika hatari kubwa ya kutumbukia katika ngono isiyostahili. Wanawake wanapofanya nongo zisizo za asili, basi kiwango cha uasherati kimekuwa cha aibu kubwa. Usagaji ni ushahidi wa watu kuwachwa kafuata “tamaa mbaya za mioyo yao katika uasherati” (Warumi 1:24).
English
Je! Biblia inasema nini kuhusu kuwa msagaji? Je, biblia inataja usagaji?