settings icon
share icon
Swali

Biblia ni nini?

Jibu


Neno "Biblia" linatokana na na neon la Kilatini na la Kigiriki lenye maana ya "kitabu," jina linalofaa, tangu Biblia ni kitabu kwa watu wote, kwa wakati wote. Ni kitabu si kama vingine, ni ya hali yake yenyewe.

Vitabu sitini na sita tofauti vyaunda Biblia. Navyo ni pamoja na vitabu vya sheria, kama vile Mambo ya Walawi na Kumbukumbu; vitabu vya kihistoria, kama vile Ezra na Matendo; vitabu vya mashairi, kama vile Zaburi na Mhubiri; vitabu vya unabii, kama vile Isaya na Ufunuo; wasifu, kama vile Mathayo na Yohana; na nyaraka (barua rasmi kama vile Tito na Waebrania.

Waandishi

takribani waandishi 40 mbalimbali wa binadamu walichangia kuandika Biblia, ambayo iliandikwa katika kipindi cha miaka 1500. Waandishi walikuwa wafalme, wavuvi, makuhani, viongozi wa serikali, wakulima, wachungaji, na madaktari. Kutoka tofauti hii yote inakuwa umoja wa ajabu, na ndhamira moja kuunganishwa pamoja.

Umoja wa Biblia ni kutokana na ukweli kwamba, hatimaye, ina Mwandishi mmoja - Mungu mwenyewe. Biblia ni "pumzi ya Mungu" (2 Timotheo 3:16). Waandishi wanadamu waliandika kile hasa Mungu alitaka waandike, na matokeo yake ilikuwa kamilifu na takatifu ya neno la Mungu (Zaburi 12:6, 2 Petro 1:21).

Mgawanyiko

Biblia imegawanywa katika sehemu mbili kuu: Agano la Kale na Agano Jipya. Kwa ufupi, Agano la Kale ni hadithi ya taifa, na Agano Jipya ni hadithi ya mwanadamu. Taifa ilikuwa njia ya Mungu ya kuleta Mwana-Adamu- Yesu Kristo ulimwenguni.

Agano la Kale inaeleza mwanzilishi na utunzaji wa taifa la Israeli. Mungu aliahidi kutumia Israeli kubariki dunia nzima (Mwanzo 12:2-3). Pindi tu baada ya Israeli ilianzishwa kama taifa, Mungu alianzisha familia ndani ya taifa hilo ambaye kupitia kwayo baraka zitapitia: jamaa ya Daudi (Zaburi 89:3-4). Kisha, kutoka ukoo wa Daudi ameahidi Mtu moja ambaye ataleta baraka ya ahadi (Isaya 11:1-10).

Agano la Jipya laeza kwa undani juu ya ujio wa mtu wa ahadi. Jina lake Yesu, na alitimiza unabii wa Agano la Kale kama Yeye aliishi maisha kamilifu, alikufa ili awe Mwokozi, na kufufuka kutoka wafu.

Tabia ya Kati

Yesu ni mhusika mkuu katika Biblia, kitabu chote chazungumza juu yake. Agano la Kale linatabiri kuja kwake na laweka mikakati ya kuingia kwake ulimwenguni. Agano la Jipya inaeleza kuja kwake na kazi yake huleta wokovu kwa ulimwengu wetu wa dhambi.

Yesu ni zaidi ya shujaa wa kihistoria, kwa kweli, Yeye ni zaidi ya mwanadamu. Yeye ni Mungu katika mwili, na kuja kwake kulikuwa tukio muhimu katika historia ya dunia. Mungu mwenyewe akawa mwanadamu ili atupe mwelekeo wa picha inayoeleweka kuwa yeye ni nani. Mungu anafanana na nini? Yeye ni kama Yesu; Yesu ni Mungu katika umbo la binadamu (Yohana 1:14, 14:9).

Muhtasari

Mungu alimuumba mwanadamu na kumweka katika mazingira kamili, hata hivyo, mwanadamu alimwasi a Mungu na akaanguka kutoka kwa kile Mungu alikusudia awe. Mungu aliiweka dunia chini ya laana kwa sababu ya dhambi lakini papo hapo Akaweka mpango wa kurejesha mwanadamu na viumbe vyote kwa utukufu wake wa awali.

Kama sehemu ya mpango wake wa ukombozi, Mungu alimwita Ibrahimu toka Babeli na kuenda katika nchi ya Kanaani (kuhusu 2000 BC). Mungu alimwahidi Abrahamu, Isaka mwanawe, na mjukuu wake Yakobo (pia iitwayo Israeli) kuwa atabariki dunia kwa njia ya ukoo wao. Familia ya Israeli ilihamia Misri toka Kanaani, ambapo waliongezeka na kuwa taifa.

Kadri 1400 BC, Mungu aliwaongoza wana wa Israeli nje ya Misri chini ya uongozi wa Musa akawapa Nchi ya Ahadi, Kanaani, kama nchi yao wenyewe. Kupitia Musa, Mungu aliwapa watu wa Israeli Sheria na alifanya patano (agano) pamoja nao. Kama wangeweza kukaa waaminifu kwa Mungu bila kufuata ibada ya sanamu ya mataifa jirani, basi wao watafanikiwa. Ikiwa watamwaacha Mungu na kufuata sanamu, basi Mungu atariaharibu taifa lao.

takribani miaka 400 baadaye, wakati wa utawala wa Daudi na Sulemani mwanawe, Israeli uliunganishwa pamoja na kuwa ufalme mkubwa na wa nguvu. Mungu aliahidi Daudi na Sulemani kwamba mtoto wao angetawala kama mfalme wa milele.

Baada ya utawala wa Sulemani, taifa la Israeli likagawanyika sehemu mbili. Makabila kumi ya kaskazini waliitwa "Israel," na wao walidumu miaka 200 kabla ya hukumu ya Mungu kwa ajili ya ibada yao. Asiria ikatwaa Israeli kama watumwa karibu 721 BC. Makabila mawili katika kusini yaliitwa "Yuda," na wao walidumu muda mrefu kidogo, lakini hatimaye, pia, wakageuka kutoka kwa Mungu. Babeli aliwachukua mateka 600 BC

Miaka 70 baadaye, Mungu kwa neema aliwaleta mabaki ya wafungwa nyumbani kwa nchi yao wenyewe. Yerusalemu, mji mkuu, ulijengwa upya karibu 444 BC, na Israeli kwa mara nyingine tena ikawa na urahia wa taifa. Hivyo, Agano la Kale lafungw.

Agano la Jipya linaanza karibu miaka 400 baadaye na kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika Bethlehem. Yesu ni mtoto aliyeahidiwa Ibrahimu na Daudi, yole atakayetimiza mpango wa Mungu kwa kumkomboa mwanadamu na kurejesha viumbe. Yesu kwa uaminifu alikamilisha kazi yake alikufa kwa ajili ya dhambi na kufufuka kutoka wafu. Kifo cha Kristo ni msingi kwa ajili ya Agano Jipya (agano) pamoja na ulimwengu. Wote ambao wana imani katika Yesu wataokolewa kutoka katika dhambi na kuishi milele.

Baada ya kufufuka kwake, Yesu aliwatuma wanafunzi wake kueneza habari kila mahali ya maisha yake na uwezo wake wa kuokoa. Wanafunzi wa Yesu wakaenda katika kila sehemu kueneza habari njema ya Yesu na wokovu. Wao walisafiri kwa njia ya Asia ndogo, Ugiriki, na kila Dola ya Kirumi. Agano Jipya linafungwa na utabiri wa kurudi kwa Yesu kuhukumu ulimwengu usio amini na kukomboa viumbe kutoka kwa laana.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries