settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kumfanya Yesu Bwana wa maisha yangu?

Jibu


La muhimu kuelewa kwamba Yesu tayari ni Bwana wa maisha yako. Hatumfanyi Yesu Bwana. Yesu ni Bwana. Tunachotakiwa kufanya ni kujiwasilisha kwa utawala Wake. Neno jingine la itikio letu kwa utawala wa Bwana ni "kujiwasilisha." Kujiwasilisha ni kukubaliana na mapenzi na udhibiti wa mwingine, na kwa kuzingatia Wakristo, ni kukubaliana na mapenzi na udhibiti wa Yesu Kristo. Hii inamaanisha kwamba wakati Maandiko yanapoamuru waumini kupendana (Yohana 5:17), hilo ndilo linafaa kufanyika. Ina maana kwamba wakati Maandiko inasema tusifanye uzinzi au kuiba (Kutoka 20: 14-15), mambo haya hayatakiwi. Inapaswa kueleweka kuwa kunyenyekea, au utifu kwa amri za Mungu, inahusiana na ukuaji wa kikristo na ukomavu, na hauhusiani na kuwa Mkristo. Mtu anakuwa Mkristo kwa imani pekee katika Kristo mbali na kazi (Waefeso 2: 8-9).

Tunapaswa kutambua kwamba utiifu kamili hauwezi kukamilika kwa kuhirusu kwa urahisi tu au kwa nguvu ya mtu wa ndani. Haitatokea tu kwa sababu tuna "amua" kufanya hivyo. Hii ni kwa sababu hata waumini wanakabiliwa na tabia na mawazo ya dhambi silizo mbali na kazi na nguvu za Roho Mtakatifu. Ili tuwe watiifu, tunapaswa kutegemea nguvu zinazotokana na ujazo wa Roho Mtakatifu (Yohana 14: 16-17). Hili kwa lenyewe ni tendo la utii, kwa sababu tunaamriwa katika Waefeso 5:18 kujazwa na Roho. Hii haina maana kwamba muumini hupata Roho zaidi, lakini Roho anampata muumini zaidi-ambayo ndiyo wazo lote la kujiwasilisha. Kujazwa na Roho ni kukubaliana na udhibiti wa Roho. Kwa kawaida, hii hutokea ikiwa muumini anajitikia uongozi wa Roho Mtakatifu. Hii haimaanishi kuwa ikiwa mtu anaongoza katika huduma ya Kikristo ya wakati wote na kutii hisia hiyo, ingawa hii inaweza kuwa mojawapo. Badala yake, ina maana ya maamuzi ya kila siku tunayofanya, kama vile kuitikia kwa huruma mtu ambaye ametufanyia maovu (Warumi 12:17); kuwa wa kweli katika mawasiliano yetu na wengine (Waefeso 4:25); kuwa waaminifu katika shughuli zetu za biashara (Waefeso 4:28); au kutumia muda katika sala na kujifunza Neno la Mungu kama tunavyoamriwa (2 Timotheo 2:15). Hii ni mifano michache tu ya maamuzi ya kila siku ambayo inaonyesha utii kwa Kristo.

Ni muhimu pia kutambua kwamba hata wakati tunashindwa kumtii, Mungu ametoa nafasi tena ili tuweze kubaki katika ushirika na Yeye. Waraka wa Kwanza Yohana 1: 9 inasema, "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote." Hata hii ni sehemu ya kujiwasilisha kwa utiifu-kuungama dhambi zetu kwa Mungu ili tuweze kubaki katika ushirika na Yeye. Ni muhimu kutambua kwamba wakati maamuzi magumu yanatokea, jambo la kwanza tunapaswa kufanya ni kuomba, kumwomba Bwana kutusaidia kufanya uamuzi sahihi na / au kutii kile tunachojua tayari ni sahihi kutoka kwa Neno.

Ili kuzingatia wazo la Ufalme wa Kristo, haijumuishi kitendo kimoja cha utii bali inavyohesabiwa kwa jumla ya utii wetu, na hauwezi kukamilika kwa nguvu zetu au uwezo wetu, bali kwa nguvu zilizopo kwetu kupitia ujazo wa Roho Mtakatifu. Tuna nguvu zaidi tunapomtegemea Yeye (2 Wakorintho 12:10).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kumfanya Yesu Bwana wa maisha yangu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries