settings icon
share icon
Swali

Chukizo ni nini?

Jibu


Chukizo ni jambo linalosababisha chuki au karaha. Katika matumizi ya Kibiblia, chukizo ni kitu ambacho Mungu hataki au anachukia kwa sababu ni machukizo kwake na tabia yake.

Maneno ya Kiebrania yanayotafsiriwa “chukizo” mara nyingi hautumika katika uhusiano na mambo kama vile ibada ya sanamu na miungu ya uongo (Kumbukumbu 17:2-5; 27:15; 29:17; Isaya 66:3; Yeremia 32:34; Ezekieli 5:9; 11:18; Hosea 9:10). Katika 1 Wafalme 11:5, mungu Moleki anaitwa “chukizo la Waamoni.” Jambo ni kwamba Mungu anachukia uongo, uchafu, na uovu wa miungu hii ya kikafiri/kipagani.

Matendo ya uchawi pia yanaitwa chukizo katika Maandiko, kama vile dhabihu ya watoto (Kumbukumbu 18:9-12; 20:18; 2 Mambo ya Nyakati 28:3). Chukizo zingine machoni pa Mungu ni mahusiano ya kingono yasyiyo ya kimungu kama vile ushoga na uzinzi (Walawi 18:22-29; 20:13; Kumbukumbu 24:4), mavazi mtambuka (mwanaume kuvaa nguo za kike au wa kike kuvaa za kiume Kumbukumbu 22:5), dhabihu zisizo kamilifu (Kumbukumbu 17:1), shughuli za biashara bila uaminifu (Kumbukumbu 25:13-16; Mithali 11:1; 20:10,23), uovu (Mithali 15:9,26), ukosefu wa haki (Mithali 17:15), kukataa kusikiliza maagizo ya Mungu (Mithali 28:9), na matoleo ya kinafiki kutoka kwa wasiotubu (Mithali 15:8; Isaya 1:13). Marejeleo mengi ya kile ambacho kimekataliwa au chukizo huonekana katika Sheria ya Mungu katika Walawi na Kumbukumbu, na katika unabii unaotangaza hukumu ya Mungu dhidi ya Israeli, na katika Mithali.

Mithali 6 ina orodha ya vitu saba ambavyo Mungu anaviita chukizo: “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, moyo uwazao mipango miovu, miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu, shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo, na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu” (Mithali 6:16-19)

Luka 16:15 Yesu anawaambia Mafarisayo, “Kwa maana vile vitu ambavyo wanadamu wanavithamini sana, kwa Mungu ni machukizo.” Muktadha wa kauli ya Yesu ni kemeo la Mafarisayo kupenda pesa. Alikuwa ametoka kuwafundisha kwamba mtu hawezi kutumikia mabwana wawili na kwamba kumtumikia Mungu na kutumikia pesa ni jambo la pekee (aya za 13-14). Mafarisayo waliitikia kwa kejeli, wakionyesha opofu wa moyo unaofurahia kile ambacho Mungu anakiita chukizo.

Tito 1:16 inasema kwamba walimu wa uongo “Wanadai kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Hao watu ni chukizo, wasiotii, wasiofaa kwa jambo lolote jema.” Yesu na Danieli wote walitabiri chukizo la uharibifu ambalo lingeharibu mahali patakatifu pa hekalu (Mathayo 24:15; Danieli 9:27). Pia kuhusiana na nyakati za mwisho, kahaba wa Babeli anaonyeshwa akiwa “Mkononi mwake ameshika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya machukizo na uchafu wa uzinzi wake” (Ufunuo 17:4). Anasemekana kuwa mama wa machukizo yote duniani (Ufunuo 17:5) na kutambuliwa kuwa “ule mji mkubwa unaotawala juu ya wafalme wa dunia” (aya ya 18). Mji huu pamoja na matendo yake yote ya kuchukiza utaangamizwa (mistari 16:17).

Ibada ya sanamu, mizani isiyo ya haki hadi mahusiano ya kingono yasiyo ya kimungu hadi uovu wa aina mbalimbali, machukizo haya hutenganisha watu na Mungu. Kweli, dhambi zote (zinazokosa kifikikia ukamilifu wa Mungu) zinaweza kuchukuliwa kuwa chukizo. Dhambi zote hututenganisha na Mungu na ni chukizo kwake (Warumi 3:23; 6:23; Mithali 15:9). Chuki la Mungu kwa dhambi hufanya dhabihu ya Kristo msalabani kuwa ya ajabu zaidi. Ilikuwa pale msalabani ambapo “Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye” (2 Wakorintho 5:21). Alipoteseka na kukufa kwa ajili ya dhambi zetu, Yesu anajitambulisha na mtunga zaburi: “Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau” (Zaburi 22:6). Yesu alichukua machukizo yetu na kuyabeba Yeye mwenyewe na badala yake akatupa karama ya haki yake. Wote ambao wanaiweka imani yao Kwake wataokolewa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Chukizo ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries