Swali
Dhambi isiyofutika ni gani / dhambi haiwezi kusamehewa ni gani?
Jibu
Kesi ya "dhambi isiyosameheka / isiyofutika" au "kumkufuru Roho Mtakatifu" imetajwa katika Marko 3:22-30 na Mathayo 12:22-32. Neno "kufuru" linaweza kufafanuliwa kuwa "upeketevu usio maana." Tunataka kutumia neno hili kwa dhambi kama vile kumlaani Mungu au kwa makusudi kuhadhi mambo yanayohusiana na Mungu. Pia ni kumwekea Mungu baadhi ya maovu, au kukanusha baadhi mazuri ambayo ni sifa kwake. Kesi hii ya kashfa, hata hivyo, ni mojapo maalum inayoitwa "Kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu" katika Mathayo 12:31. Katika fungu hili, Mafarisayo walishuhudia dhahiri ushahidi kwamba Yesu alikuwa akifanya miujiza kwa nguvu za Roho Mtakatifu, badala yake walisema ya kuwa Amepagagwa na pepo ya Beelzebuli, (Mathayo 12:24). Katika Marko 3:30, Yesu ni yu maalum sana hasa kuhusu chenye walichofanya "Kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu."
Hali hii ya kukufuru kisha ina husu shutuma kwa Yesu Kristo (katika utu, akiwa duniani) ya kuwa alipagagwa na pepo. Kuna njia nyingine ya kukufuru Roho Mtakatifu (kama vile Kunena uongo kwake, kama katika kesi ya Anania na Safira katika Matendo 5:1-10), lakini mashtaka dhidi ya Yesu yalikuwa kufuru ambayo isiyosameheka. Hii dhambi maalum isiyosameheka dhidi ya Roho Mtakatifu haiwezi kunakilishwa hii leo.
Dhambi isiyosameheka hii leo ni ile ya kuendelea kutokuwa na imani. Hakuna msamaha kwa mtu ambao wamefariki bila imani. Yohana 3:16 inatuambia, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwngu, hata kamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Hali tu ambayo mwanadau angekuwa na msamaha ni kama yeye hayuko miongoni mwa "yeyote" Yule amwaminiye Yeye. Yesu akasema, "Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" (Yohana 14:6). Kukataa njia pekee ya wokovu ni kujihukumu mwenyewe kwndaa jehanamu ya milele kwa sababu ya kukataa msamaha wa pekee, kwa hakika hakuna msamaha.
Watu wengi wanahofia kwamba wamefanya baadhi ya dhambi ambazo Mungu anaweza au hawezi samehe, na wao huhisi hakuna matumaini kwao, hajalishi ata wafanye nini. Shetani angependa kitu bora zaidi kuliko kutuweka kufikiria dhana hili baya. Ukweli ni kwamba kama mtu ana hofu hii, yeye anahitaji tu kuja mbele ya Mungu, kukiri dhambi hiyo, kutubu, na kukubali ahadi ya Mungu ya msamaha. "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki na atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote" (1 Yohana 1:9). Aya hii inatuakikishia kwamba Mungu yu tayari kusamehe dhambi yoyote bila kujali ni jinsi gani inatisha-kama sisi huja kwake kwa toba. Kama wewe unateseka chini ya mzigo wa hatia hii leo, Mungu anasubiri mikono yake ikiwa wazi kwa upendo na huruma kwako ili uje kwake. Yeye kamwe hawezi kuabisha au kushindwa kusamehe wote hutenda dhambi.
English
Dhambi isiyofutika ni gani / dhambi haiwezi kusamehewa ni gani?