Swali
Dhambi ya asili ni gani?
Jibu
Neno "dhambi ya asili" linahusu dhambi ya kutokutii kwa Adamu katika kula kutoka mti wa ujuzi wa mema na mabaya na madhara yake yakawa kwa jamii yote ya binadamu. Dhambi ya asili inaweza fafanuliwa kama "ile dhambi na hatia yake ambayo sisi sote huwa katika macho ya Mungu kama matokeo ya moja kwa moja ya dhambi ya Adamu katika bustani ya Edeni." Mafundisho ya dhambi ya asili yanaangazia hasa juu ya madhara yake juu yetu na nafasi yetu kwa Mungu, hata kabla ya sisi tuwe wa umri wa kutosha kutenda dhambi kwa fahamu. Kuna maoni kuu tatu yanayoangazia athari hiyo.
Pelagianism: Mtazamo huu unasema kwamba dhambi ya Adamu haikuwa na athari juu ya roho za kizazi chake chochote mbali mfano wake wa dhambi hushawishi wale waliomfuata yeye pia walisini. Kulingana na mtazamo huu, mtu ana uwezo wa kuacha dhambi kama ataamua. Fundisho hili linaenda kinyume na idadi ya mistari ambayo inanaonyesha kuwa mwanadamu bila tumaini amekuwa mtumwa wa dhambi zake (mbali na Mungu kuingilia kati) na kwamba kazi zake njema ni "mfu" au hafai wala kustahili neema ya Mungu (Waefeso 2:1-2, Mathayo 15: 18-19; Warumi 7:23, Waebrania 6:01; 9:14).
Arminianism: Waarminia huamini kuwa dhambi ya Adamu imesababisha wanadamu wengine kurithi mwelekeo wa dhambi, inajulikana mara nyingi kama "asili ya dhambi." Asili hii ya dhambi inatufanya kutenda dhambi katika njia sawa asili ya paka inamfanya anapweka - inakuja kawaida. Kulingana na mtazamo huu, mtu hawezi kuacha dhambi kwa uwezo wake mwenyewe; ndio sababu Mungu anatupa neema kwa woteili kutuwezesha sisi kuacha. Katika Arminianism, neema hii inaitwa neema ya kinga. Kulingana na mtazamo huu, sisi si hatuwajibiki kwa dhambi ya Adamu, bali zetu wenyewe. Fundisho hili laenda kinyume na ukweli kwamba wote hubeba adhabu ya dhambi, ingawa wote hawakuweza kufanya dhambi sawia na Adamu (1 Wakorintho 15:22; Warumi 5:12-18). Wala mafundisho ya neema ya kinga kwa wazi kupatikana katika maandiko.
Ukalivinisti: Mafundisho Calvin yanasema kwamba dhambi ya Adamu imesababisha sio tu sis kuwa na asili ya dhambi, lakini pia kuingia katika madeni ya hatia yetu mbele ya Mungu ambayo sisi tunastahili adhabu. Kuwa mimba na dhambi ya asili juu yetu (Zaburi 51:5) matokeo yake sisi tumerithi iliyo ovu sana, ambayo Yeremia 17:9 inaeleza moyo wa binadamu kuwa "ni mdanganyifu kuliko vitu vyote na zaidi ya tiba." Siyo eit Adamu alipatikana na hatia tu pekee kwa sababu yeye alikua amefanya dhambi, bali hatia yake na adhabu yake ni (kifo) tunayostahili pia (Warumi 5:12, 19). Kuna mitazamo miwili ni kwa nini hatia ya Adamu inapaswa kuonekana na Mungu vile pia inafaa kwetu. maoni ya kwanza yanasema kwamba binadamu alikuwa ndani ya Adamu katika hali ya mbegu; hivyo Adamu alipofanya dhambi, sisi tulifanya dhambi katika yeye. Hii ni sawa na mafundisho ya kibiblia kwamba Lawi (kizazi cha Ibrahimu) alitoa sehemu ya kumi Melkizedeki katika Ibrahimu (Mwanzo 14:20; Waebrania 7:4-9), ingawa Lawi hakuwa amezaliwa hadi baada ya mamia ya miaka. Mtazamo mwingine mkuu ni kwamba Adamu aliwahi kuwa mwakilishi wetu na hivyo, wakati alifanya dhambi, sisi tulipatikan na hatia pia.
Maoni ya Kikalvin yamuona mtu kama asiye na uwezo wa kushinda dhambi yake mbali na nguvu ya Roho Mtakatifu, nguvu zinazo milikiwa tu wakati mtu anarudi katika kumtegemea Kristo na sadaka yake ya kuosha dhambi msalabani. Maoni ya Kikalvin ya dhambi ya asili mara nyingi yanaambatana na mafundisho ya kibiblia. Hata hivyo, ni namna gani Mungu anaweza kutuhesabia uwajibikaji kwa ajili ya dhambi hatukufanya sisi wenyewe? Kuna tafsiri inayokubalika kwamba sisi huwa na jukumu la dhambi ya asili wakati sisi huchagua kukubali, na kutenda kulingana na, asili yetu ya dhambi. Wakati hufika katika maisha yetu wakati sisi huwa na ufahamu wa dhambi yetu wenyewe. Katika hatua hiyo tunapaswa kukataa dhambi ya asili na kuitubu. Badala yake, sisi wote "huidhinisha" asili hiyo ya dhambi, katika athari tunasema kwamba ni nzuri. Katika kuidhinisha hali yetu ya dhambi, sisi huonyesha kubalio letu kwa matendo ya Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni. Kwa hiyo sisi tuna hatia ya dhambi bila kuifanya hasa.
English
Dhambi ya asili ni gani?