settings icon
share icon
Swali

Je! Kamwe si dhambi kujichulia?

Jibu


Kwa maelezo ya msingi, tafadhali soma Makala yetu kuhusu “Je, kupiga punyeto ni dhambi?” Ingawa makala hayo yanashughulikia suala hilo kwa namna ya jumla, madhumi ya makala haya ni kuangazia swali la“ni dhambi kupiga punyeto” kutoka kwa mtazamo mwingine. Kila mara tunapokea maswali ambayo kimsingi huorodhesha visingizio vya kupiga punyeto au kuelezea ni kwa nini mara nyingi sio dhambi kupunyeto. Hakuna visingizio au uhalali wowote unaosadikisha, lakini kuna hali moja maalum ambayo inazua maswali kuhusu ni kwa nini kupunyeto ni dhambi.

Hali ni hii: mume na mke wametengana kwa muda mrefu, wana ruhusa ya kila mmoja kujipiga punyeto, na wanapunyeto bila ponografia au kuwa na mawazo ya tamaa au ya usherati na watu wengine. Je! katika hali hiyo ni dhambi kupunyeto? Je! kunalo kosa kwa mwanandoa ambaye ametengana na mwenziwe kwa ajili kazi ya kijeshi kwa mfano, apunyeto akiwa mbali na mwenziwe? Je, ni kweli kwamba mvutano kuhusu ngono huongezeka wakati mtu ambaye amezoea kufanya ngono ananyimwa ngono kwa wakati mrefu. Mkazo huu wa kisaikolojia unaweza kufanya iwe vigumu zaidi kupinga vishawishi vya ngono-uzinzi au ponografia inakuwa hatari zaidi. Naam, ni kweli kupunyeto kunaweza punguza hisia za ngono. Kwa hivyo, je, hali hii ni mfano bora ambapo kupunyeto haitakuwa dhambi?

Jibu bora tunaweza kutoa ni “labda.” Kuwa na ruhusa ya mwenzi wako kunaweza kumaanisha kanuni ya 1 Wakorintho 7:4 haitatumika. Kutokuwepo kabisa na ponografia au mawazo ya tamaa mbaya au mawazo yasiyo ya kiadili kungeondoa mambo ya dhambi yaliyo wazi yanayohusiana na kupunyeto. (Kinachoifanya mara nyingi kupunyeto kuwa dhambi ni tamaa mbaya zinazohusishwa na tendo hilo.” Lakini, katika hali ya wenzi waliotengana, hatuapaswi kupuuza swali muhimu: Je, kuna njia ipi mbadala na kupunyeto? Je nini kitafanyika ikiwa mtu katika hali kama hii hakupunyeto? Kusema kuwa mtu huyo hatakuwa na uwezo wa kuzuia majaribu ni kupuuza nguvu za Roho Mtakatifu anayekaa ndani yake (1 Yohana 4:4). Biblia inatuagiza kuyakimbia majaribu ya ngono (1 Wakorintho 6:18; 10:13; 2 Timotheo 2:22). Biblia haituambii kutafuta njia mbadala za kulifanya jaribio hilo lisiwe na nguvu.

Kwa hivyo, ingawa huenda si dhambi kupiga punyeto katika hali kama iliyopo hapo juu, Biblia inatuambia kufanya maamuzi kwa uhakika zaidi badala ya, “huenda,” “labda” au “pengine.” Warumi 14:23 inasema, “Kwa kuwa chochote kinachofanywa pasipo imani ni dhambi.” Warumi 14:5 inaonyesha kwamba tunapaswa ‘kuwa na hakika ’ kabla ya kufanya au kutofanya jambo fulani. Ukweli kwamba swali “je, bado ni dhambi kufanya punyeto?” huulizwa inaonyesha ukosefu wa uhakika. Muulizaji anatoa ushahidi wa “kutosadikika kikamilifu.” Kuuliza “Je,______ si dhambi IKIWA…..?” ni hatari kwa msingi wake kwa sababu swali kama hilo hutafuta mianya katika viwango ambavyo vinginevyo ni thabiti. Ni afadhali kuliko kujaribu kutafuta hali ambazo dhambi si dhambi tena na kukaa mbali na dhambi iwezekanavyo. Huku ingawa inaweza kuwa si dhambi kupunyeto katika hali maalum iliyoshughulikiwa hapa, tunajua hili kwa hakika: “Kwa hiyo ndugu zangu, sisi tu wadeni, si wa mwili, ili tuishi kwa kuufuata mwili” (Warumi 8:12).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kamwe si dhambi kujichulia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries