Swali
Je! Mwana anawajibika kwa dhambi za baba yake?
Jibu
Ezekieli 18 inaweka wazi kwamba Mungu anamwajibisha kila mtu kwa dhambi yake mwenyewe. Mstari wa 1 hadi 4 wasema, “Neno la Bwana likanijia kusema: “Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli: “‘Baba wamekula zabibu zenye chachu, nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’? “Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli. Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.” Wakati huohuo, Kutoka 20:5-6 inasema, ” Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.” Je! Kwa hivyo, watoto wanawajibika kwa dhambi ya wazazi wao? Naam na la.
Mungu anahukumu moyo wa kila mtu. Katika Agano la Kale na Agano Jipya, tunaona Mungu akishirikiana na watu kulingana na imani yao wenyewe. Katika Mwanzo tunaona Mungu akimtendea Kaini tofauti na alivyomtendea Abeli, kulingana na Matendo yao tofauti. Ezekieli 18:30, “Kwa hiyo, ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake.” Yohana 3:16 inasema kwamba “ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Mstari wa 18 unasema, “Yeyote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.” Kwa wazi, wokovu hutolewa kwa wote, bila kujali matendo ya wazazi wa mtu.
Kwa upande mwingine, ni wazi kwamba dhambi za wazazi huathir watoto wao. Mwana wa kwanza wa Daudi na Bathsheba alikufa mara tu baada ya kuzaliwa kwa sababu ya dhambi ya Daudi. Waisraeli, wakiwa taifa, waliadhibiwa na Mungu kwa ajili ya dhambi yao, na nyakati nyingine adhabu hiyo iliathiri watoto pia. Leo hii, tunaona jinsi dhambi ya wazazi inavyoathiri watoto. Wale wanaokua wakitazama tabia ya dhambi mara nyingi wana uwezekano mkubwa wa kujihusisha wenyewe. Dhambi fulani huwaondoa wazazi nyumbani au huzuia uwezo wao wa kuwa walezi wenye upendo, na kuwaweka watoto kwa matatizo yanayoweza kutokea siku zijazo. Uraibu mara nyingi una chembechembe za maumbile. Sehemu mpya ya ufumbuzi wa chembechembe inapendekeza kwamba kiwewe kinaweza kuacha “makovu ya molekuli” kwenye chembechembe yetu- na kwamba makovu hayo hupitishwa kwa kinasaba kwa kizazi cha tatu na cha nne. Hata wazi zaidi, dhambi ya Adamu na Hawa imetuathir sisi sote. Sisi sote tumezaliwa na asili ya dhambi kwa sababu Adamu alichagua kutomtii Mungu. Dhambi yake “ilipitishwa” kwetu.
Dhambi kamwe sio jambo la siri. Daima huathiri wale walio karibu nasi. Hii ni kweli hasa katika familia. Dhambi za wazazi zitaathiri watoto wao. Hata hivyo, Mungu ni mwenye neema na rehema. Sisi sote tumeharibiwa na dhambi (Warumi 3:23). Sote tumepewa fursa ya kukubali utakaso wa Yesu (Warumi 6:23). Tunaweza kufanwa watoto katika familia ya Mungu na kurithi asili mpya. Biblia hata inazungumza kuhusu kuzaliwa mara ya pili kwa maneno ya urithi: “Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu” (1 Yohana 3:9). Mungu husamehe dhambi tunapokubali dhabihu ya Yesu. “Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye” (2 Wakorintho 5:21).
English
Je! Mwana anawajibika kwa dhambi za baba yake?