settings icon
share icon
Swali

Je! Elimu ya uhusiano wa nyama na nafsi katika mwili wa mwanadamu ni nini?

Jibu


Fundisho ambalo linahusishwa kwa karibu sana na lile la Aristotle na Thomas Aquinas, ni mtazamo wa elimu ya uhusiano wa mwili na nafsi na uhusiano kati ya mwili na roho.

Somo la uhusiano wa mwili na nafsi ni nadharia kwamba “maada” (asili kamili, asili dhahanio) inaunganika na “umbo” (ambayo mara nyingi tunaichukulia kuwa maada). Kwa mfano, udongo ambao haujatengezwa umbo unaweza tengezwa umbo na kufanywa mgumu ili utengeze tofali-udongo ndio “maada,” na umbo na kufanywa gumu ndio “umbo”; na tofali ndio “kitu” kinachotokea.

Elimu ya uhusiano wa mwili na nafsi inatumia nadharia ile ya hali asili ya mwanadamu. Ni jinsi gani mwili, nafsi na roho zinahusiana? Majadiliano mengi ya Wakristo ya suala hili huzingatia dhana ya mgao mtatu kuliko mgao uwili. Maoni yote yanaonyesha tafauti kati ya nafsi na mwili. Aristotle, Aquinas na wengine walishikilia kwamba mwili ni “maada” na nafsi ni “umbo” ambavyo vinampa mtu asili yake. Pia waliamini kwamba umbo na maada vimeunganishwa bila kutenganishwa na vinategemeana. Tofali haliwezi kuwa tofali bila kuchanganya udongo na ugumu na umbo fulani. Vile vile, mwanadamu hawezi kuwa mwanadamu bila kuunganisha mwili na nafsi.

Neno elimu ya hilomofia (uhusiano wa mwili na roho ya mwanadamu) humaanisha “maada”(hylos) na “umbo”(morphos) la mwanadamu. Aristotle aliazima maneno haya kutoka kwa Plato, ambaye maoni yake kuhusu somo hili zilielezewa katika fumbo lake la pango katika Jamhuri (The Republic). Aristotle alifundisha kwamba hakuna maada inayoweza kuwepo bila kufuata umbo fulani, na hakuna umbo linaloweza kuwepo bila kuwa na uwepo wake katika maada. Kwa hivyo, Aristotle alifundisha kwamba mwili hauwezi ishi bila nafsi, na nafsi haiwezi ishi bila mwili (hakuwezi kuwa na maisha baada ya kifo).

Aquinas hakutilia mkazo kuhusu kutotenganishwa kwa umbo na maada. Kama kasisi wa Dominika, Aquinas aliheshimu sana Maandiko, jambo ambalo linaonyesha kwamba kuna uwezekano wa mtengano kati ya nafsi na maada. Mistari kama vile Mathayo 10:28 inafundisha kwamba kati ya mwili na nafsi hakuna kile kinategemea kingine: “Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho.” Pengine hoja nyenye nguvu dhidi ya Imani kauli ya Aristotle imo katika 1 Wakorintho 15:40, ambapo Paulo anaandika kuhusu ufufuo: “kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani.”

Hata hivyo, Aquinas aliweza kuunganisha mwili na nafsi wa binadamu na mafundisho muhimu ya Kristo. Alikanuni kwamba, hata ingawa nafsi na mwili vina uhusiano, nafsi inaweza kuishi bila mwili. Nafsi haijakamilika hadi iunganike tena na mwili. Nafsi au “umbo” wa mwanadamu ipo katika hali isiyo ya asili hadi Mungu atakapoufufua mwili. Kwa njia hii Aquinas alifafanua mpito kati ya kifo cha mwili wa dunia hii na ufufuo wa mwili wa mbinguni. Kulingana na Aquinas, Kuwa na mwili ni muhimu sana katika kufanyika binadamu, na hivyo ubinadamu hauwezi kukamilishwa bila mwili.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Elimu ya uhusiano wa nyama na nafsi katika mwili wa mwanadamu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries