Swali
Je! enzi na mamlaka ni nini?
Jibu
Katika sehemu nyingi ambapo tunasoma juu ya enzi na mamlaka katika Biblia, muktadha unaonyesha wazi kuwa inarejelea kundi kubwa la roho waovu na wabaya ambao wanafanya vita dhidi ya watu wa Mungu. Enzi na mamlaka ya Shetani ndio zinaangaziwa hapa, viumbe ambavyo vinatumia nguvu katika ulimwengu usionekana ili kupinga kila kitu na kila aliye wa Mungu.
Kutajwa mara ya kwanza kwa enzi na mamlaka ni katika Warumi 8:37-39: “Lakini katika mambo haya yote tunashinda, naam na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa sio mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote zitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu, Bwana wetu.” Mistari hii inahusu ushindi ambao Kristo ameshinda dhidi ya nguvu zote zinazotukabili. Sisi ni “zaidi ya washindi” kwa sababu hakuna nguvu-wala uhai, wala kifo, malaika, mapepo, hakika hakuna kitu, kinaweza kututenganisha na upendo wa Mungu. “Nguvu” ambazo zinarejelewa hapa ni zile zilizo na nguvu ya miujiza, iwe ni walimu wa uongo na malaika au ushirika wa mapepo inaweza kuzipa nguvu. Kilicho wazi ni kwamba, chochote kile walicho hawawezi kututenganisha na upendo wa Mungu. Tumehakikishwa ushindi. Itakuwa bahati mbaya kushinda ukitaka kugundua nguvu na ukose maana kamili ya aya, ambayo ni uhakikisho wa kile ambacho Mungu amefanya ili kutuokoa.
Kutajwa kwingine kwa enzi na mamlaka ni katika Wakolosai 1:16, “Kwake yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala; vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.” Hapa kuna kauli wazi kuwa Mungu ndiye Muumba na Mtawala juu ya mamlaka zote, ziwe zimenyenyekea Kwake au kuasi dhidi Yake. Nguvu zozote jeshi la uovu linaweza kuwa nayo, haziko nje ya udhibiti wa Mungu wetu Mkuu, ambaye huwatumia hata wanyonge ili kutimiza malengo na makusudi Yake kamili (Danieli 4:35; Isaya 46:10-11).
Katika sura inayofuata ya Wakolosai, tunasoma kuhusu uwezo mkuu wa Yesu juu ya mamlaka nyingine zote: “Mungu akiisha kuzivua enzi na mamlaka, alizifanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuziburura kwa ujasiri, akizishinda katika msalaba wa Kristo” (Wakolosai 2:15). Kwa kuzingatia mambo yote, mamlaka yanaanzishwa na Kristo na kwa hivyo yako chini ya udhibiti wake. Hayapaswi kuogopwa, kwa kuwa yameshakishwa nyang’anywa silaha na msalaba. Mwokozi kwa kifo chake, alitwaa mamlaka kutoka kwao, na kuchukua tena kile walichokwisha kichukua. Shetani na jeshi lake walivamia dunia na kuwavuta wanadamu hadi matekani, wakiwafanya kuwa chini ya utawala wao mwovu. Lakini Kristo, kupitia kwa kifo chake, alimkimbiza mvamizi na kuwatwaa wale wote ambao walikuwa wamepotoshwa. Wakolosai 2:14 inazungumza juu ya Yesu kusulubishwa huku mashtaka dhidi yake yakiwa yameandikwa juu yake. Rekodi ya makosa yetu ambayo kwayo Shetani anatushtaki nayo kwa Mungu, imetundikwa msalabani. Na kwa njia hii imeharibiwa, na nguvu hizo haziwezi tena kutushtaki; sisi hatuna hatia machoni pa Mungu. Na hivyo zimenyanganywa makali.
Waefeso 3:10-11 inatuonyesha enzi na mamlaka tofauti-zile za ulimwengu wa mbingu: “Ili sasa kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na wenye mamlaka katika ulimwengu wa roho, sawasawa na kusudi lake la milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Hapa tunaona majeshi ya malaika yakionyeshwa hekima na kusudi la Mungu katika mpango wa wokovu kupitia Kristo. Malaika wale watakatifu na wasio watakatifu, wanashuhudia utukufu wa Mungu na ukuu wa Kristo juu ya viumbe vyote katika kanisa, wale ambao wameokolewa na kuhifadhiwa kwa nguvu Zake (Waefeso 1:20-21).
Waefeso 6:12 inatangaza vita ambavyo tunapigana navyo katika maisha yetu yote “bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Kwa hiyo, baada ya kuokolewa, ni lazima tupambane katika kutenda mambo mema kwa kuzingatia ushindi wa hakika ulioahidiwa katika Warumi 8. Ni kana kwamba tunakabiliana na jeshi la wenye nguvu za giza ambao wamenyang’anywa silaha kutoka kwa nguvu halisi na ambao kwao tumeahidiwa ushindi. Ni jukumu letu kuonyesha na kutegemea hekima na nguvu za Mungu katika kuzishinda maishani mwetu. Tunaweza kufanya hivyo kwa kutumainia ushindi wa Mungu.
Rejeleo la mwisho kwa enzi na mamlaka ni Tito 3:1. Hapa zinarejelea ule utawala wa kiserikali ambao Mungu ameweka juu yetu kwa ajili ya ulinzi na hali njema yetu. Wao ni wawakilishi wa Mungu duniani, na kumtii Yeye kunahusisha kujiitisha kwa mamlaka yake yaliyowekwa kikatiba. Wale ambao wataasi mamlaka ya dunia hii kwa “hiyo yeye anayeasi dhidi ya mamlaka inayotawala anaasi dhidi ya kile kilichowekwa na Mungu, nao wale wafanyao hivyo watajiletea hukumu juu yao wenyewe” (Warumi 13:2).
English
Je! enzi na mamlaka ni nini?