Swali
Ni nani hawa wapanda farasi wanne wa Ufunuo?
Jibu
Wapanda farasi wanne wa ufunuo wameelezewa katika Ufunuo sura ya 6, aya 1-8. wapanda farasi wanne ni maelezo ya mfano wa matukio tofauti ambayo yatafanyika katika nyakati za mwisho. Farasi wa kwanza wa utabiri ametajwa katika Ufunuo 6:2: "Nikaona, na tazama, farasi mweiupe, nay eye aliympanda an uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akkishinda tena apate kushidna." Huyu farasi wa kwanza kuna uwezekano kuwa aanamrejelea Mpinga Kristo, ambaye atapewa mamlaka na kushinda wote wanaompinga. Adui wa Kristo ni wafananishwaji uongo wa Kristo wa kweli, ambaye pia atarudi juu ya farasi mweupe (Ufunuo 19:11-16).
Mpanda farasi wa pili wa ufunuo anaonekana katika Ufunuo 6:4, "Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, naye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa." Mpanda farasi wa pili inahusu vita vya kutisha vitakavyo tokea katika nyakati za mwisho. Farasi wa tatu ni kama ilivyoelezwa katika Ufunuo 6:5-6 inasema: "... na tazama, farasi mweiusi, nay eye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wane, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia wala usiyadhuru mafuta wala divai" Mpanda farasi wa tatu wa ufunuo inahusu njaa kubwa itakayotokea, kuna uwezekano kama matokeo ya vita vya kutoka mpanda farasi wa pili.
Mpanda farasi wa nne anatajwa katika Ufunuo 6:8, "Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, nay eye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi." Farasi wa nne wa ufunuo ni ishara ya kifo na uharibifu. Inaonekana kuwa mchanganyiko wa farasi aliyepita. Farasi wa nne wa ufunuo huleta vita zaidi na njaa kali pamoja na mapigo ya kutisha na magonjwa. Je, la ajabu zaidi, au labda kutisha, ni kwamba farasi wa nne wa ufunuo ni "mtangulizi" wa hukumu mbaya zaidi ambayo itakuja baadaye katika dhiki (Ufunuo sura ya 8-9 na 16).
English
Ni nani hawa wapanda farasi wanne wa Ufunuo?