settings icon
share icon
Swali

Ni jinsi gani mimi naweza kuwa na furaha katika maisha yangu ya kikristo?

Jibu


Misimu ya huzuni na unyogovu inaweza kuingia katika maisha Mkristo hata ule mcha Mungu zaidi. Tunaona mifano mingi ya hili katika Biblia. Ayubu alitamani kama yeye hangalizaliwa (Ayubu 3:11). Daudi aliomba achukuliwa mbali mahali ambapo yeye hawezi kukabiliana na ukweli (Zaburi 55:6-8). Elia, hata baada ya kuwashinda manabii 450 wa Baali kwa moto aliouita kutoka mbinguni (1 Wafalme 18:16-46), alitorokea nyikani na kumwomba Mungu kuyachukua maisha yake (1 Wafalme 19:3-5).

Hivyo ni jinsi gani sisi tutavishinda vipindi hivi vya huzuni? Tunaweza kuona jinsi watu hawa walishinda uchungu wa matatizo yao. Ayubu alisema kwamba, kama sisi huomba na kukumbuka baraka zetu, Mungu huturudishia furaha na haki (Ayubu 33:26). Daudi aliandika kwamba kusoma neno la Mungu kunaweza tuletea furaha (Zaburi 19:8 ). Daudi pia alitambua kwamba alihitaji kumtukuza Mungu hata katikati ya kukata tamaa (Zaburi 42:5). Katika kesi cha Eliya, Mungu basi alimruhusu apumzike kwa muda na kisha akatuma mtu, Elisha, kumsaidia (1 Wafalme 19:19-21). Sisi pia tunahitaji marafiki tuweze kushiriki nao machungu na maumivu yetu (Mhubiri 4:9-12). Inaweza kuwa na manufaa kwa kushiriki hisia zetu na Mkristo mwenzetu. Sisi tunaweza kuwa na mshangaa kuona kwamba mtu mwingine anajitahidi na baadhi ya mambo sawia na yele tunayapitia.

Muhimu zaidi, kuna uhakika kwamba kuishi maisha yetu wenyewe, matatizo yetu, machungu yetu, na hasa machangu yetu ya kale kamwe hayatazalisha furaha ya kweli ya kiroho. Furaha haipatikani katika mali, ni si haipatikani katika matibabu ya kisaikolojia, na kwa hakika haipatikana katika kujidhania kwa nafsi yetu wenyewe. Inapatikana katika Kristo. Sisi ambao ni mali ya Bwana "tunaona fahari katika Kristo Yesu, wala hatuutumaini mwili" (Wafilipi 3:3). Kumjua Kristo ni kuwa na fahamu ya nafsi zetu wenyewe, na ufahamu wa kweli wa kiroho, na kuifanya vigumu sisi kuwa na kiburi kwa utukufu wetu wenyewe, kwa hekima, nguvu , utajiri, au wema, bali katika Kristo kwa hekima yake na nguvu, katika utajiri wake na wema, na katika nafsi yake. Kama tutabaki ndani yake, kujuzamisha katika neno lake, na kutafuta kumjua kwa undani zaidi, "furaha itakuwa tele" (Yohana 15:1-11).

Mwisho, kumbuka kwamba ni kwa njia ya Roho Mtakatifu wa Mungu kwamba tunaweza kupata furaha ya kweli (Zaburi 51:11-12; Wagalatia 5:22, 1 Wathesalonike 1:6). Hatuwezi kufanya chochote mbali na nguvu ya Mungu (2 Wakorintho 12:10, 13:4). Hakika, ni vigumu sisi kujaribu kuwa na furaha kwa njia ya juhudi zetu wenyewe, tutakuwa katika hali mbaya zaidi. Kupumzika katika mikono ya Bwana (Mathayo 11:28-30) na kutafuta uso wake kwa njia ya maombi na maandiko. "Basi Mungu wa matumaini na awajaze niny furaha yote na amani katika kuamini mpate kuzidi san kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu" (Warumi 15:13).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni jinsi gani mimi naweza kuwa na furaha katika maisha yangu ya kikristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries