settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu gadhabu?

Jibu


Kudhibiti hasira ni mada muhimu. Washauri wakristo wanaarifu kwamba asilimia 50 ya watu wanaingia kutafuta ushauri wana matatizo yanayohusiana na hasira. Hasira inaweza haribu kabisa mawasiliano nakusambaratisha uhusiano, na inaathiri furaha na afya ya watu wengi. Cha kusikitisha, watu huwa wanahalalisha hasira zao badala ya kukubali jukumu kwa ajili yake. Kila mtu anajitahidi, kwa viwango tofauti, na hasira.Shukurani , Neno la Mungu lina kanuni kuhusu jinsi ya kushughulikia hasira kwa namna Mungu apendavyo, na jinsi ya kuzishinda hasira za dhambi.

Hasira sio dhambi kamwe. Kuna aina ya hasira ambayo Biblia inaidhinisha, mara nyingi huitwa “ufidhuli adilifu.” Mungu amegadhabika (Zaburi 7:11, Marko 3: 5). Na waumini wameamriwa kuwa na hasira (Waefeso 4:26). Maneno mawili ya Kiyunani yametumika katika Agano Jipya kwa neno letu la Kiingereza "hasira."Moja linamaanisha "Hisia kali , nishati" na lingine linamaanisha "Enye wasiwasi, kuchemka." Kibiblia, hasira ni nguvu ambazo Mungu ametupa zitusaidie kutatua matatizo. Mifano ya hasira katika Biblia ni pamoja na Paulo kukabiliana na Petro kwa sababu ya mfano wake mbaya katika Wagalatia 2: 11-14, Daudi kutamauka kwa kusikia kuwa Nathanieli nabii kushiriki katika ufisadi (2 Samweli 12), na hasira ya Yesu juu ya jinsi baadhi ya jews walienda katika mlolongo kwa ibada katika hekalu la Mungu Yerusalemu (Yohana 2: 13-18). Jua kwamba kwa hii mifano ya hasira hakuna hata moja ambayo kulikuwa na utetezi wa binafsi, bali utetezi wa wengine au wa kanuni.

Hasira huwa dhambi wakati imetiwa motisha kibinafsi (Yakobo 1:20), wakati lengo la Mungu limetiwa dosari (1 Wakorintho 10:31), au wakati hasira imeruhusiwa kudumu (Waefeso 4: 26-27). Badala ya kutumia nguvu zinazotokana na hasira kutatua shida tuliyonayo, ni mtu anayeshambuliwa. Waefeso 4: 15-19 inasema kuwa tunafaa kusema ukweli kwa upendo na tutumie maneno yetu kuwajenga wengine, tusiruhusu maneno mabovu au yenye uharibifu kutoka kwa midomo yetu. Kwa bahati mbaya, usemi huu wenye sumu ni tabia ya kawaida kwa mwanadamu asiyeokoka (Warumi 3: 13-14). Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; bali mwenye hekima huizuia na kuhituliza. (Mithali 29:11),. Kuachana na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe ibilisi nafasi. (Waefeso 4: 26-27). Hii inaweza kusababisha huzuni na kuudhika juu ya vitu vidogo, hata ambavyo havihusiki na shida ilioko.

Tunaweza kushughulikia hasira kibiblia na kutambua na kukiri hasira zetu za kibinafsi na / au utunzaji wetu wa makosa ya hasira kama dhambi (Mithali 28:13; 1 Yohana 1: 9). Kukiri huku kunapaswa kuwa kwa Mungu na wale ambao wamejeruhiwa na hasira yetu. Tunapaswa si kupunguza dhambi kwa kuwatetea au kulaumiana.

Tunaweza kushughulikia hasira kibiblia kwa kumwona Mungu katika majaribu. Hii hasa ni muhimu wakati watu wamefanya jambo la kutuchukisha. Yakobo 1: 2-4, Warumi 8: 28-29, na Mwanzo 50:20 zote hulenga ukweli kwamba Mungu ni mwenye nguvu na anadhibiti kamili kila hali na mtu ambayo inaingia njiani mwetu. Hakuna kinachotokea kwa maana ya kuwa yeye hana sababu au kukiruhusu. Na kama aya hizi hushiriki, Mungu ni Mungu mwema (Zaburi 145: 8, 9, 17) ambaye Anaruhusu mambo yote katika maisha yetu kwa manufaa yetu na mema ya wengine. Kutafakari juu ya ukweli huu mpaka utoke kwa vichwa vyetu hadi mioyo yetu lazima tubadilishe jinsi sisi huguswa na wale ambao hutukosea.

Tunaweza kushughulikia hasira kibiblia kwa kufanya chumba kwa ghadhabu ya Mungu. Hii ni muhimu hasa katika kesi ya ukosefu wa haki, wakati watu "waovu" huwakandamiza wati "wasiojua" . Mwanzo 50:19 na Warumi 12:19 zote mbili hutuambia kuwa tusimchezee Mungu. Mungu ni mwenye mwema na wa haki, na tunaweza kumwamini Yeye ambaye anajua yote na kuona kila kitu na kutenda haki (Mwanzo 18:25).

Tunaweza kushughulikia hasira kibiblia kwa kutolipza uovu kwa mema (Mwanzo 50:21, Warumi 12:21). Hii ni muhimu kwa kubadili hasira yetu na kuwa upendo. Kama vile matendo yetu hububuchika kutoka katika mioyo yetu, hivyo pia mioyo yetu inaweza kubadilishwa kwa matendo yetu (Mathayo 5: 43-48). Hiyo ni, tunaweza kubadili hisia zetu kuhusu watu wengine kwa kubadilisha jinsi kutenda kwa watu hao.

Tunaweza kudhibiti hasira kibiblia kwa kuwasiliana na kutatua tatizo. Kuna kanuni nne za msingi za mawasiliano zimeelezwa katika Waefeso 4:15, 25-32:

1) Kuwa waaminifu na ongea (Waefeso 4:15, 25). Watu hawawezi kusoma akili zetu. Ni lazima tuseme ukweli katika upendo.

2) Kukaa sasa (Waefeso 4: 26-27). Tusiruhusu kinacho tusumbua kijijenge hadi tupoteze udhibiti. Kushughulika na kushiriki kile kinachotusumbua kabla ifike kiwango ni muhimu.

3) Shambulia tatizo, si mtu (Waefeso 4:29, 31). Kando ya mstari huu, lazima tukumbuke umuhimu wa kutunza kiasi cha sauti zetu chini (Mithali 15: 1).

4) Tenda, na usikerwe (Waefeso 4: 31-32). Kwa sababu ya asili yetu ya kuanguka, msukumo wetu wa kwanza mara nyingi mpigo wetu ni wa dhambi (v. 31). Wakati aliotumia katika "kuhesabu hadi kumi" inapaswa kutumika kwa kutafakari juu ya njia inayompendeza Mungu kwa kujibu (v. 32) na kujikumbusha jinsi hasira hutumika kutatua matatizo na sio kuleta shida kubwa.

Hatimaye, ni lazima tuchukue hatua ya kutatua sehemu yetu ya tatizo (Matendo 12:18). Hatuwezi kudhibiti jinsi wengine hututendea au kujibu, lakini tunaweza kufanya mabadiliko sinji ambavyo wengine wanaweza kutujibu, lakini tunaweza fanya mabadiliko yanayohitajika kwa upande wetu. Kushinda hasira sio ya usiku mmoja. Lakini kwa njia ya maombi, kujifunza Biblia, na kumtegemea Roho Mtakatifu wa Mungu, hasira mwovu inaweza kushindwa. Tu kama vile tunaweza ruhusu hasira kuingia ndani mwetu kwa matendo y akila siku, ni lazima pia tujue kukabiliana usahihi mpaka inakuwa tabia yenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu gadhabu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries