settings icon
share icon
Swali

Je, ni hoja gani kuu dhidi ya upatanisho kiasi?

Jibu


Upatanisho kiwango ni fundisho kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya wateule pekee. Ni Mojawapo ya hoja za Ukalvini. Wengi wanaoamini fundisho la upatanisho kiasi wanapendelea neno “ukombozi mahususi,” lakini ili kuondoa mkanganyiko nakala hii itatumia “upatanisho kiwango.”

Waararati na Wakalvini wenye hoja nne au Waamiraldi, wanaamini kwamba upatanisho kiasi kama ulivyofafanuliwa hauambatani na Biblia. Huduma ya Got Questions Ministries (Huduma ya ninayo Maswali) ina msimamo rasmi wa mambo manne katika kuunga mkono kiwango fulani cha upatanisho kiwango, huku ikipinga dhana kuwa hatimaye watu wote wataokolewa. Hapa, tunawasilisha hoja kadhaa dhidi ya upatanisho kiasi.

Hoja ya 1: Upatanisho kiasi hauungwi mkokono na somo la kuchambu Maandiko (Hermeneutics)

Bishano dhidi ya upatanisho kiwango kunazo aya ambazo zinapinga upatatanisho kiasi na zinaonekana kuunga mkono upatanisho wa ulimwengu wote, in aya ambazo zinaonekana kuweka kiwango kwa upatanisho wa Kristo, aya zinazotangaza umuhimu wa imani katika kupokea wokovu, na aina kadhaa za Agano la Kale ambazo haziambatani na dhana ya upatanisho kiasi.

Vifungu ambavyo vinaunga mkono upatanisho wa ulimwengu wote.

Upatanisho wa jumla (ama usio na kikomo) unaungwa mkono katika Agano Jipya. Yohana 3:16-17 inasema “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee… kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa.” Neno la Kigiriki kosmos, linalotafsiriwa “ulimwengu” linahusisha wakaaji wa dunia nzima. Mistari nyingine inayounga mkono upatanisho usio na mipaka ni pamoja na Yohana 1:29, ambapo Yesu kuwa atachukua “dhambi ya ulimwengu”; Katika Warumi 11:32 Mungu anawarehemu “wote” wasiotii; na 1 Yohana 2:2, amabayo inasema Yesu “ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.”

Kati ya aya hizi hakuna yoyote ambayo ina mipaka inayotajwa au kudokezwa, juu ya dhabihu ya Kristo. Kana kwamba haitoshi kusema kuwa Yesu Kristo ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, mtume Yohana alitumia haswa neno la Kigiriki holou ambalo linamaanisha “zima, yote, kamili.” Isipokuwa upatanisho wenye kikomo unafikiriwa, hakuna msingi dhabiti wa kuzuia kiwango cha upatanisho unaotajwa katika 1 Yohana 2:2.

Vifungu vinavyotaja upatanisho kwa waumini pekee

Katika upande mwingine wa sarafu, kuna mistari nyingine inayosema kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya wale wanaoamini. Mistari inayoonekana kuunga upatanisho wenye mipaka ni pamoja na Yohana 10:15, ambapo Yesu anasema, “nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo”; na Ufunuo 5:9, ambayo inaonyesha kwamba damu ya Yesu “ilumnunulia Mungu watu kutoka kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa.”

Vifungu hivi na vinginevyo vinataja kundi teule la watu kuwa lengo la kazi ya ukombozi wa Yesu. Hata hivyo, hakuna kifungu kinachoweka kikomo kwa utoaji wa Mungu wa wokovu. Inasema tu kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya wale wanaoamini, na sio kuwa alikufa kwa ajili wanaoamini pekee. Yesu alisema kuwa aliutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo; Hakusema kuwa aliutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo pekee. Kumesalia kundi kubwa zaidi ambalo kondoo ni sehemu yake.

Imani inahitajika kwa wokovu

Upatanisho wa kila mtu sio sawa na dhana kuwa kila mtu ataokolewa na kwenda mbinguni. Upatanisho usio na kiwango unakubali ukweli kwamba upatanisho wa Yesu lazima ukubaliwe kwa imani, na kuwa sio kila mtu ataamini. Wafuaasi wa Calvin wenye hoja nne wanaamini kuwa wokovu huja kwa wale walio na imani; ni amani inayoleta athari za kuokoa za upatanisho kwa Mkristo. Ingawa wasioamini wamepewa karama ya wokovu kwa njia ya upatanisho wa Kristo, wao wameikataa karama ya Mungu. Baadhi ya vifungu vinavyotangaza umuhimu wa imani kwa wokovu ni Luka 8:12, Yohana 20:31 Matendo 16:31; Warumi 1:16; 10:9; na Waefeso 2:8

Aina za Kristo wa Agano La Kale

Aina ya Kristo inayorejelewa mara kwa mara inamwakilisha Yeye kama mwana-kondoo. Mfumo wa dhabihu wa Agano La Kale na sherehe ya Pasaka waziwazi unaonyeshwa adhabu ya dhambi na hitaji letu la kuwa na kibadala kisicho na hatia ili kufunika dhambi zetu (tazama 1 Wakorintho 5:7). Wakati wa Pasaka la kwanza, Waisraeli wote walikuwa na fursa ya kutoa dhabihu ya mwana-kondoo na kupaka damu yake kwenye miimo ya milango. Wakati huohuo, kila familia ilipaswa kuonyesha imani katika Mungu. Upatanisho wa Pasaka ulikua wa kila mtu, kwa kuwa ulitolewa kwa ajili ya wote, lakini upatanisho wa kibanafsi lazima ungekuwako kwa imani.

Aina nyingine ya Kristo katika Agano la Kale ni nyoka wa shaba katika mlingoti (Hesabu 21:5-9). Yesu alijifungamanisha na kitu hiki katika Yohana 3:14, akieleza kwamba lazima “ainuliwe” kutoka duniani. Wakati wa tauni ya “nyoka wa moto” siku za Musa, yeyote aliyetazama nyoka wa shaba -akiamini kwamba Mungu angemponya-basi aliponywa. Nguvu ya uponyaji ilikuwa kwa watu wote, kumaanisha ilipatikana kwa kila mmoja wa Waisraeli, ikitegemea tu nia yao ya kutii. Yesu alilinganisha tukio hilo na kifo chake msalabani na uponyaji wa kiroho anaoutoa.

Hoja ya 2: Tamaduni/Mapokeo ya Kikristo yanapinga upatanusho wa kikomo

Upatanisho ulio na kikomo daima umekuwa imani yenye utata. Mkutano wa majimbo ya makanisa wa Dort katika mwaka wa 1619 alitoa hoja za mafundisho ambayo sasa yanajulikana kama hoja tano za Ukalvini; hata hivyo wanatheolojia katika kikao hicho walikataa upatanisho wa kikomo huku wakikubaliana na mambo mengine manne ya Ukalvini.

Athanasiu, baba wa kanisa la kwanza alikuwa akielezea upatanisho muda mrefu kabla ya muungamo wa Kiprotestanti na mkutano wa wakubwa wa kanisa. Katika nakala yake ya "On the Incarnation of the Word" (2.9), Athanasius anaandika kwamba kifo cha Yesu “kilikuwa cha mbadala kwa ajili ya uhai kwa wote” na kwamba kwa sababu ya dhabihu ya Yesu, “uharibifu unaoambatana na kifo umepoteza nguvu zake juu ya wote.” Kumbuka neno wote. Hoja ya Athanasius ni kwamba kifo cha Yesu kilifanya upatanisho wa wanadamu wote.

Kinaya ni kwamba, huenda Calvin mwenyewe hakuweka thamani kubwa juu ya wazo ya upatanisho wa kikomo. Walakini, hoja tano za kile kinachoitwa “Ukalvini” zilitoka katika na kikao majimbo cha kanisa huko Uholanzi takriban miaka 60 baada ya kifo chake. Calvin alikuwa na hili la kusema kuhusu Yohana 3:16: “Ni jambo la busara la imani ambalo hutuweka huru kutokana na uharibifu wa milele…Na ametumia jina la kijumlisha watu wote ambalo ni yeyote, kuwaalika wote kushiriki kwa maisha bila kubagua na kuondoa kisingizio chochote kutoka kwa wasioamini. Tunapata kuona uagizaji wa neno Ulimwengu; anajionyesha kuwa yeye mwenyewe amepatanishwa na ulimwengu wote wakati anapowaalika watu wote kwa imani ya Kristo bila kubagua, ambayo sio kitu kingine ila mlango wa kuingia katika uzima” (tafsiri juu ya Yohana, sehemu ya/ Commentary on John, Vol. 1).

Hoja ya 3: Upatanisho wa kikomo unaifanya isiwezekane kutoa wokovu kwa wote

Upatanisho wa kikomo huathiri imani ya mtu kuhusu uinjilisti na toleo la wokovu. Kimsingi, ikiwa ni wale pekee watookolewa (wateule) ndio ambao wamepatanishwa, basi hakuna upatanisho utakaotolewa kwa mtu mwingine. Ungeweza tu kutoa wokovu kwa wateule. Hata mtazamo wa juu juu katika huduma ya Yesu unaonyesha kwamba alitoa mwaliko wa wokovu kwa watu ambao alijua wangeshiriki katika kumsulubisha (tazama Luka 13:34). Katika kitabu cha Matendo, Paulo alihubiri maeneo mengi ya miji, na Petro alihubiria maelfu ya watu kwa wakati mmoja. Wokovu ulitolewa kwa wote bila masharti ya kuhitimu wala ubaguzi. Toba na imani ndio mambo yaliyohitajika (tazama Mathayo 21:32). Ikiwa kifo cha Kristo hakikutoa upatanisho kwa watu wote, basi mitume na hata Yesu mwenyewe walikua wanatoa kitu ambacho wasikilizaji wao hawangepokea.

Hitimisho:

Upatanisho wa kikomo ndio hoja ya mapokeo ya Ukalvini ambayo yamesababisha mkanganyiko zaidi na fadhaa miongoni mwa wanatheolojia wanaoamini Biblia. Je, ni wateule tu ndio watakaookolewa? Naam. Hata hivyo, dhabihu ya Yesu inatosha kulipia dhambi zote, na toleo la wokovu ni kwa ulimwengu wote. Mwaliko wetu kwa wengine kumpokea Yesu Kristo unapaswa kusisitiza mwito wa Roho katika Ufunuo 22:17: “njoo!’ aliye na kiu aje; anayependa na achukuaye maji ya uhai bila malipo.”

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni hoja gani kuu dhidi ya upatanisho kiasi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries