settings icon
share icon
Swali

Je, ina maana gani kuwa huwezi kutumikia mabwana wawili katika Mathayo 6:24?

Jibu


Katika Mathayo 6:24, Yesu alisema, ”Hakuna mtu awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali.” alizungumza maneno haya kama sehemu ya Mahubiri Yake ya Mlimani (Mathayo 5-7), ambapo Alikuwa amesema ni upumbavu kujiwekea hazina duniani ambapo, “nondo na kutu huharibu, nao wevi huvunja na kuiba” (Mathayo 6:19-20); badala yake, alituhimiza tuweke hazina mbinguni ambako itadumu milele. Kikwazo kinachotuzuia uwekezaji wa busara ni moyo. Popote hazina yetu ipo, hapo ndipo mioyo yetu itakapokuwa (Mathayo 6:21). Tunafuata yale ambayo yameteka mioyo yetu, na Yesu alisema wazi kwamba hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili.

Bwana ni kitu chochote ambacho kinatufanya kuwa watumwa (Warumi 6:16). Pombe, tamaa, na pesa zote ni bwana kwa baadhi ya watu. Katika onyo la Yesu kwamba hatuwezi kutumikia mabwana wawili, Anataja pesa kama bwana aliye kinyume na Mungu.

Wito wa Yesu wa kumfuata ni wito wa kuwaacha mabwana wengine wote. Alimwita Mathayo kutoka kwenye kibanda cha ushuru (Mathayo 9:9). Mathayo alitii na kujiepusha na utajiri wa kupita kiasi na mikataba michafu. Yesu alimwita Petro, Yakobo, na Yohana kutoka kwenye vivuko vya wavuvu (Marko 1:16-18). Kutii mwito wa Yesu kulimaanisha kwamba walipaswa kuacha kila kitu walichojua, kila kitu ambacho walikuwa wamefanyia kazi. Yesu alimwita Paulo, Mfarisayo aliyekuwa amefanikiwa, kwa maneno haya, “Nami nitamwonyesha jinsi impasavyo kuteseka kwa ajili ya Jina langu” (Matendo 9:16). Maneno hayo hayatawahi kuifanya kuwa tangazo kubwa sokoni la kampeni ya Ukristo-bali pengine yanafaa, kwa sababu hiyo ndio maana ya kumfuata Yesu (Luka 9:23). Ni lazima tukane kila kitu kingine, bila kujali gharama (Mathayo 10:34-39).

Bwana anajieleza yeye mwenyewe kuwa ni “Mungu mwenye wivu” (Kutoka 34:14). Hii ina maana kwamba Yeye hulinda yale ambayo ni haki yake. Yeye ana wivu na haki kwa ajili ya mapenzi yetu kwa sababu tuliumbwa kumjua na kumpenda (Wakolosai 1:16). Yeye hana wivu kwa ajili yake mwenyewe; Hahitaji chochet (Zaburi 50:9-10). Ana wivu kwa ajili yetu kwa sababu tunamhitaji (Marko 12:30; Mathayo 22:37). Tunapomtumikia bwana mwingine kama vile pesa, tunajinyang’anya kila kitu tulichoumbwa kuwa, na tunamnyang’anya Mungu heshima yake inayostahili.

Tangazo la Yesu kwetu ni la kipekee. Alitununua kwa damu yake mwenyewe na kutukomboa kutoka kwa bwana wetu wa zamani, dhambi (1 Wakorintho 6:20; 7:23; Warumi 6:17). Yeye hashiriki kiti Chacke cha enzi na mtu yeyote. Wakati wa Yesu dunaini, baadhi ya watu walimfuata kwa njia Fulani, lakini ibada yao ilikuwa ya juujuu tu (Luka 9:57-62). Walitaka kitu ambacho Yesu alitoa, lakini hawakujitolea (Marko 10:17-22). Mambo mengine yalikuwa muhimu zaidi. Walitaka kuwatumikia mabwana wawili.

Hatuwezi tumikia mabwana wawili kwa sababu, kama Yesu alivyoonyesha, tunaishia kumchukia mmoja na kumpenda mwingine. Ni asili tu. Mabwana wanaopinga wanadai vitu tofauti na kuongoza njia tofauti. Bwana anaelekea upande mmoja, na mwili wetu na ulimwengu unaelekea upande mwingine. Uchaguzi lazima ufanywe. Tunapomfuata Kristo, lazima tufe kwa kila kitu kingine, au hatutafanikiwa. Tutakuwa kama baadhi ya mbegu hizo katika mfano wa Yesu (Luka 8:5-15)-ambazo sehemu yake ndizo zilizaa matunda. Zingine ziliota mwanzoni lakini zikanyauka na kufa. Hazikuwa na mizizi katika udongo mzuri.

Tukijaribu kuwatumikia mabwana wawili, tutakuwa na uaminifu uliogawanyika, na, matatizo ya uanafunzi yanapogongana na mvuto wa anasa ya kimwili, mvuto wa sumaku wa utajiri na mafanikio ya kidunia utatuondoa kutoka kwa Kristo (ona 2 Timotheo 4:10). Wito wa kumcha Mungu unakwenda kinyume na asili yetu ya dhambi. Ni kwa msaada wa Roho Mtakatifu tu tunaweza kubaki wakfu kwa Bwana mmoja (Yohana 6:44).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ina maana gani kuwa huwezi kutumikia mabwana wawili katika Mathayo 6:24?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries